Unakumbuka kweli unachokisimamia
Kwa mujibu wa Isaya ulidai Yesu ndiye mwana, ndiye Roho na ndiye Baba yaani kwa maana yako Yesu anajibadilishabadilisha
Sasa hapa andiko linasema wapo watatu nafsi ambazo ni independent siyo mmoja kubadilikabadilika
Nimekujibu ila huenda hujaelewa. Umeshindwa kabisa kutoa maana ya hiyo Isaya 9, unahamisha tu goli. Sasa nitakuoa ufafanuzi wa 1 Yoh 5.
Kwanza ni vema kuelewa Yohana hapa anazungumza nini? Hoja ya msingi, HAKUNA KISA CHA UTATU HAPO!! Yohana anathibitisha kuwa YESU NI MWANA WA MUNGU na kwamba ndani yake mna uzima wa milele.
Tuanze na hao WATATU wanaoshuhudia mbinguni:
1. Baba - ukirejea ubatizo wa Yesu sauti ya Baba ilitoka katika wingu jeupe, huyu ni mwanangu mpendwa wangu...
Tena wakati Yesu anageuka sura bustanini Gethsemani sauti hiyo ilisikika, huyu ni mwanangu mpendwa...
2. Neno - rejea Yoh 1:1 Kristo ni Neno la Mungu, hakuna wakati hata mmoja Kristo aliongea ama kufanya kwa fikra zake mwenyewe isipokuwa alimsikia na kumwona Baba. Maana yake ni kwamba Kristo kama mwanadamu kamili hakutenda lolote kwa ufahamu wa kibinadamu bali kila alichofanya ni Baba ndiye alikuwa anatenda ndani yake, total surrender.
Yohana 5 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁹ Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile.
Kwa hiyo basi, yote aliyofundisha Kristo hapa duniani ni USHUHUDA wa Baba kwetu kupitia mwanaye wa pekee.
3. Roho Mtakatifu - wakati wa kubatizwa Yesu, Roho Mtakatifu alishuka na kukaa juu yake. Yohana Mbatizaji ndiye aliyeshuhudia hilo kwani alipewa ishara hiyo na Mungu jinsi ya kumtambua Mwana wa Mungu.
Siku ya Pentekoste Roho al8shuka na tazama Petro alivyo mshuhudia Kristo kuwa ni mwana wa Mungu akiwa amejaa Roho Mtakatifu.
Huo ni ushuhuda toka mbinguni, na hao wote washuhudiao wanakubaliana (hawatofautiani) katika huo ushuhuda.
Kristo alisema hapokei ushuhuda wake mwanadamu:
Yohana 5 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
³¹ Mimi nikijishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu si kweli.
³²
Yuko mwingine anayenishuhudia; nami najua ya kuwa ushuhuda wake anaonishuhudia ni kweli.
³³ Ninyi mlituma watu kwa Yohana, naye akaishuhudia kweli.
³⁴ Lakini mimi siupokei ushuhuda kwa wanadamu; walakini ninasema haya ili ninyi mpate kuokoka.
Kumbe yuko MMOJA TU amshuhudiaye wala si wengi, naye ushuhuda wake ni wa kweli. Huyu ndiye aliyeshuhudia kwanza kama Baba, halafu kama Neno kisha kama Roho Mtakatifu. Ushuhuda qnaoutoa ni Roho kamili ndio maana hata Neno la Mungu li hai, ndio kusema WAKO WATATU. Muhimu ni kwamba hawa wote ni mmoja tu. Ndipo nalikuandikia kwamba Waebrania 1:1 inarejwa hapa, kwamba zamani Baba alinena na baba zetu kwa njia mbalimbali, lakini sasa ananena nasi kupitia Mwana (Neno). Hapo mwanzoaoinena kupitia kijiti cha moto, wingu, nk. Lakini sasa hatuhitaji kumsikia Mungu kupitia njia hizo kwani amelituma Neno lake kwa njia ya Kristo.
Hapa pia ni muhimu kutambua, Yohana alikuwa akijenga hoja yake kupitia kanuni ya kimaandiko kwamba jambo huthibitika kwa ushuhuda wa watu wawili ama watatu.
Hebu tuone wanaoshuhudia duniani:
1. Roho - huyu hata sasa yupi baada ya kuwa amevuviwa kwa waamini. Yeye anaendelea kumshuhudia Kristo ulimwenguni hata sasa. Ndio maana ukisoma Neno la Mungu bila Roho Mtakatifu hutoambulia kitu.
2. Maji - maji yanatupa uzima. Tukioshwa kwa damu ya Yesu tunapokea uzima kwa maji. Kumbuka alichomwa mkuki ubavuni yakatoka maji na damu? Maji ni ishara ya uzima katika Yesu.
3. Damu - tumekombolewa kwa damu ya Yesu Kristo, hata sasa damu iliyomwagika msalabani ni ushuhuda mkubwa wa Kristo kama mwana wa Mungu. Damu inatusafisha dhambi na kutuleta kwa Baba.
Nimeandika kwa haraka kwa sababu nimetingwa, lakini nadhani umrpata picha halisi. Sura hiyo haihusiani na habari ya Utatu Mtakatifu bali ukitaka kuielewa zaidi soma pia Yohana 5.