Dondosha mstari wowote wa Biblia unaoupenda leo ni Ijumaa

Dondosha mstari wowote wa Biblia unaoupenda leo ni Ijumaa

Biblia haina tofauti na zile hadithi za akina Abunuwasi. Uongo mtupu, cha ajabu utakuta mtu msomi kabisa anaamini yaliyoandikwa humo.

1 Kor 6:9-11​

Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi. Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.
"Mungu akusamehe maana hujui ulitendalo"
 
Mwache akasome koroani kwa kiarabu na haelewi🤣🤣🤣
Iko hivi.
Ili watu wajue kweli na wafuate neno lake inabidi watu wahubiriwe neno la Mungu kwa lugha zao ili wajue kweli.
Ndiyo maana tunapata Biblia zilizo kwenye lugha zote duniani. Lengo la Mungu, watu waache dhambi na watende matendo mema yanayompendeza Mungu.
Sasa kama Biblia tungekuwa tunasoma kwa kiingereza halafu kuna watu wengine hawajui kiingereza sasa watapataje kujua kweli? Mungu anajua lugha zote na atakusikia.
Ndiyo maana wale wa dini zingine, badala ya kukuambia ya dini zao watakimbilia kwenye Biblia kwasababu hawajui yaliyoandikwa. Ukiwafuata vijana wengi wa dini ile hawajui kitabu chao.
Hapa wenyewe wanashangaa inakuwaje vijana wanajua maandiko yaliyoko kwenye Biblia namna hii.
 
Mkuu nimekuelewa sana
 
IMG_0799.jpg

1korintho 15:24-28
28 “Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana (yesu) mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.”

Efeso 4:6
“Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.”

Zekaria 14:9
“Naye Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo Bwana atakuwa mmoja, na jina lake moja.”

Ufunuo 21:3
“Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.”
 
Isaya 61:
1 - Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.
 
Kuna maamuuzi mawili tuu!kuifuata au kuikataa na kila maamuzi yana cv zake!

Kum 30:19 SUV​

Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako
 
Isaya 61:
1 - Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.
Hii hata Yesu aliinukuu😍😍😍
 
Isaya 61:
1 - Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.
Na kuwatangazia mateka uhuru wao😀
 
Tusaidie andiko,

Hesabu 23:19

Mungu si mtu

Yesu Amekuwepo Kabla Ya Ibrahimu​

48 Wakamjibu, “Tulitamka sawa tuliposema kuwa wewe ni Msa maria na tena umepagawa na pepo.” 49 Yesu akawajibu, “Sina pepo. Mimi namheshimu Baba yangu bali ninyi mnanivunjia heshima yangu. 50 Hata hivyo mimi sitafuti utukufu wangu binafsi; yuko anayetaka niheshimiwe na ndiye atakayekuwa mwamuzi. 51 Ninawaam bia wazi kwamba, mtu ye yote anayetii mafundisho yangu hatakufa kamwe.” 52 Wakasema, “Sasa umetuhakikishia kabisa kwamba una wazimu! Ikiwa Ibrahimu alikufa na Manabii nao walikufa, utase maje, ‘mtu akitii mafundisho yangu hatakufa?’ 53 Je, wewe ni mkuu zaidi ya baba yetu Ibrahimu ambaye alikufa? Na Manabii ambao nao walikufa? Hivi unajifanya wewe kuwa nani?” 54 Yesu akawa jibu, “Kama nikijisifu mwenyewe sifa hiyo itakuwa haina maana. Anayenipa heshima ni Baba yangu, huyo ambaye ninyi mnamwita Mungu wenu. 55 Lakini ninyi hamumfahamu. Mimi namfahamu. Nikisema sim fahamu nitakuwa mwongo kama ninyi. Mimi namfahamu na ninatii maneno yake. 56 Baba yenu Ibrahimu alishangilia alipojua kuwa atashuhudia siku ya kuja kwangu. Aliiona siku hiyo na akafurahi sana.” 57 Wayahudi wakamwambia, “Wewe hujatimiza hata miaka hamsini, itawezekanaje uwe umemwona Ibrahimu?” 58 Yesu akawa jibu, “Nawaambia wazi, kabla Ibrahimu hajazaliwa, ‘Mimi nipo.’ ” 59 Ndipo wakainua mawe wamwue; lakini Yesu akajificha wasim wone; akatoka Hekaluni.

Yohana 14:8-12​

Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha. Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba? Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe. Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.
 
Biblia haina tofauti na zile hadithi za akina Abunuwasi. Uongo mtupu, cha ajabu utakuta mtu msomi kabisa anaamini yaliyoandikwa humo.
Ufunuo wa Yohana 21:
8 - Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
 
Hizi namba unazotumia Kila siku,,,,1,2,3,4,,,,,,,,,,ni za kiarabu.
Cha kushangaza Mimi na wewe tunazitumia.[emoji15][emoji15][emoji15]
Hizi ni namba za kiarabu🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 so dunia nzima tunasoma kiarabu
 
Back
Top Bottom