Tusaidie andiko,
Hesabu 23:19
Mungu si mtu
Yesu Amekuwepo Kabla Ya Ibrahimu
48 Wakamjibu, “Tulitamka sawa tuliposema kuwa wewe ni Msa maria na tena umepagawa na pepo.” 49 Yesu akawajibu, “Sina pepo. Mimi namheshimu Baba yangu bali ninyi mnanivunjia heshima yangu. 50 Hata hivyo mimi sitafuti utukufu wangu binafsi; yuko anayetaka niheshimiwe na ndiye atakayekuwa mwamuzi. 51 Ninawaam bia wazi kwamba, mtu ye yote anayetii mafundisho yangu hatakufa kamwe.” 52 Wakasema, “Sasa umetuhakikishia kabisa kwamba una wazimu! Ikiwa Ibrahimu alikufa na Manabii nao walikufa, utase maje, ‘mtu akitii mafundisho yangu hatakufa?’ 53 Je, wewe ni mkuu zaidi ya baba yetu Ibrahimu ambaye alikufa? Na Manabii ambao nao walikufa? Hivi unajifanya wewe kuwa nani?” 54 Yesu akawa jibu, “Kama nikijisifu mwenyewe sifa hiyo itakuwa haina maana. Anayenipa heshima ni Baba yangu, huyo ambaye ninyi mnamwita Mungu wenu. 55 Lakini ninyi hamumfahamu. Mimi namfahamu. Nikisema sim fahamu nitakuwa mwongo kama ninyi. Mimi namfahamu na ninatii maneno yake. 56 Baba yenu Ibrahimu alishangilia alipojua kuwa atashuhudia siku ya kuja kwangu. Aliiona siku hiyo na akafurahi sana.” 57 Wayahudi wakamwambia, “Wewe hujatimiza hata miaka hamsini, itawezekanaje uwe umemwona Ibrahimu?” 58 Yesu akawa jibu, “Nawaambia wazi, kabla Ibrahimu hajazaliwa, ‘Mimi nipo.’ ” 59 Ndipo wakainua mawe wamwue; lakini Yesu akajificha wasim wone; akatoka Hekaluni.
Yohana 14:8-12
Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha. Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba? Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe. Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.