Donor Fatigue: Wazungu wametuchoka, sisi tunanunua ma VX!

Uliona wapi mwizi wa mali za nchi anaitwa majina mazuri, mjanja, boss, mkuu, comredi nk. China ni kifo, ulaya ni kifungo, ila Africa hasa Tanzania huyo ni mwekezaji,.mfadhili wa chama/vyama nk. Balaa.
Mkuu unidai Cognac!
Umenena mpaka Raha. Eti mwizi anajenga misikiti na makanisa! Mwizi na fisadi eti anaabudiwa! Fisadi na mwizi wa mali za umma anaombewa makanisani?! Fisadi na mwizi wa hela za umma anatangazwa na kuujulisha umma anajenga vituo vya watoto yatima??
Only in Africa 🌍!
Wacha Trump atutukane na viongozi wetu!
 

Tunajiibia wenyewe kodi. Hatuna nidhamu na hela za walipa kodi. Sasa hivi tumegeukia mikopo na kuomba misaada.

Tumekwama. Na hali ya dunia inavyoenda, tutakwama kabisa. Marekani wameanza, na hakika wengine watafuatia. Ni suala la muda.

Sijui kwanini tuliamua kupiga chini kila kitu cha awamu ya kwanza ya Nyerere. Tulikosea sana. makosa yake tungeyarekebisha. mazuri tungeendeleza.

Kulikuwa na shida gani kwenye siasa ya kujitegemea? Kulikuwa na shida gani kujenga utaifa? Kulikuwa na shida gani katika kujenga uwajibikaji kwenye vijiji ambao kama tungeboresha, pengine ile dhana nzima ya kujitegemea ingeanzia chini kabisa ikafika mpaka levels za juu.

Kuna watu wametutapeli na wanaendelea kututapeli kwa kutumia fursa na nafasi walizonazo kujineemesha na kutuingiza chaka la kuwa ombaomba na wakopaji tusioweza kulipa.
 
Kwa upumbavu kama huu Trump yuko sahihi 100%
 

Attachments

  • Screenshot_20241116-162911.jpg
    173 KB · Views: 4
Umenena vema mkuu.
Mwalimu tunamkumbuka kwa kuona na kuwa na malengo ya mbali.
 
Duh 🙄 !
Trump ni kiboko !
Je ametutukana ?! Au ??! 😳😱
 
Hatuja kuwa tayari muda wote huo sass ni muda wa kulazimishwa.
 
Ni wakati Sasa Kwa nchi zetu kujitegemea Kwa kutumia kikamilifu rasilimali ilizopewa na Mungu ikiwa ni pamoja na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuweka vipaumbele kwenye mambo ya msingi na yenye tija kwa taifa
 
Ni wakati Sasa Kwa nchi zetu kujitegemea Kwa kutumia kikamilifu rasilimali ilizopewa na Mungu ikiwa ni pamoja na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuweka vipaumbele kwenye mambo ya msingi na yenye tija kwa taifa
Ukijizoeza kuishi maisha ya kifahari kuacha inakuwa ni ngumu sana labda ulazimishwe kuacha !
Na ulazimishwe kikweli kweli sio kiuongo uongo 😳!
 
Mgonjwa mwenye akili sasa hivi ndiyo wakati wa kuzoa ARV na kuzisonda nyumbani - mbele giza trump kagusisha nyanya za Betry.
 
Kwa jinsi ulivyo mnafiki eti unamkumbuka Mwl. Nyerere wakati Mwamba Magufuli alikuwa anayasema hayahaya ya kujitegemea mkamfuata Lissu na jamaa zake wa MIGA! PUMBAVU!!
 
Ni lini ccm watatuma watu wa kwenda "kumteka" trump kwa sababu anaongea ukweli mtupu wasioupenda kusikia
 
Kwa jinsi ulivyo mnafiki eti unamkumbuka Mwl. Nyerere wakati Mwamba Magufuli alikuwa anayasema hayahaya ya kujitegemea mkamfuata Lissu na jamaa zake wa MIGA! PUMBAVU!!
Du......mkuu ukiwa pimbi wa kufikiri usijionyeshe hadharani. Kwa Mwalimu nyerere, Magufuli ni mfuta viatu,. Katika nyumba ya Mwalimu , Magufuli hana sifa za kuwa hata mlinzi wa getini.

Akili zako za kijinga zipeleke Chato na ufe kwa covid!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…