Inategemea na hoja.. fergurson na ronaldo ni case tofauti ya diamond na ruge..
Ruge hakumtoa diamond... na hata yeye anathibitisha hilo... why useme ruge ndie sababu ya mafanikio ya diamond?
Diamond amefanikiwa sababu ya hard working, life style yake kama reality show, hata asipoimba maisha yake yanakuvutia kumfatilia kwa vituko, mziki mzuri ambao unachezeka na kuimbwa na mashabiki kiurahisi, kujua kucheza na social media yeye mwenyewe, na wanaomzunguka... pia sio mbahili anakula na wengi.. ana jeshi mitandaoni zaidi ya watu 300 ambao kila mmoja ana mafollowers kibao,, na hilo jeshi anawalipa hela za bundle na soda wampost post... mojawapo wale waliokufa juzi kwa ajali kina plutnumz mondi, ..
ndio maana wimbo diamond akitoa hata sasa hivi unaenea haraka nchi nzima sababu wanaupost post kila sehemu... sasa unaanzia wapi kusema bila ruge diamond asingefanikiwa.. mbona kina barnaba hawafanikiwi kama diamond ? ruge anampenda diamond kuliko nandy ? au barnaba ? au THT yake ?
mbagala imerecordiwa gheto kwa bob juniour... ka studio hakana vifaa vya kuzidi milion 5... hata vocal wanaingiza usiku kuepusha makelele maana hakana sound proof ya kueleweka.. na bado ukawa hit song.. na vocal ameingiza mara moja tu alivyokuwa serious na kazi...
kina ruby ruge anawaandikia hadi nyimbo ndio maana anawatawala.. ila uwezo wa kumtawala diamond hana....
barnaba na ruge walimponda sana diamond hawezi kuimba na wakamcheka mwaka 2006 alivyoenda kuomba nafasi THT..
na hilo jambo Diamond mpaka leo linamuumiza... na kwa taarifa yako Barnaba alienda omba nafasi WCB wamsaidie promo za soko la nje.. na diamond alimkumbusha hilo jambo la walivyomcheka.. ila akamwambia atamsaidia awezavyo
Ruge katika kosa kubwa analijutia mpaka leo ni kumchukulia poa diamond wakati anatoka....
Mtu ambaye Diamond anasema amemsaidia ni Bob juniur tu japo hawapatani kwa tabia za kike za Bob juniour... ila huyo ndie msaada mkubwa wa diamond.. sababu alimrekodia kwa mkopo ,, na nyimbo za mwanzo alimtengenezea bure kabisa kishkaji tu.. ambapo kina ruge walimtosa kabisa
Ronaldo anaweza kusema Sir Alex Ferguson ndio kila kitu kwenye mafanikio yake ya mpira, sasa wewe utabisha kwasababu Louis Nani hakuweza kufika kiwango kama cha Ronaldo?