Dotto Bulendu: Tathmini yangu juu ya mahojiano kati ya BBC na Rais Samia Suluhu

Tathmini yangu ya juu ya mahojiano kati ya BBC Na Rais Samia Suluhu Hassan.

Na Dotto Bulendu (MwanaPuge).Nikiandika kutoka kijijini Puge........
@@@@@@

BBC wamefanikiwa kuongeza umaarufu wao Kwa Siku ya jana Kwa Maana ya Idadi ya watu wanaowasikiliza na kuwatazama kupitia Vyombo vyao vya Redio,TV na Mitandao ya kijamii,kwani kwenye kujenga umaarufu na kuaminika Kwa chombo na Mwandishi,tunaambiwa Moja ya mbinu ni kuhakikisha unawafikia watu wenye ushawishi Mkubwa ama nafasi kubwa Kwenye jamii,Na ndivyo akina Tim Sebastian,Christian Amanpour,Steven Sucker,Tido Mhando n.k walivyofanya Kwa kulenga zaidi nyakati zao kuwahoji watu wakubwa.

BBC wamefanikiwa kujua hitaji Na takwa la wasikilizaji Na watazamaji wao Kwa wakati huu(Audience needs and wants),jamii ya watanzania Kwa muda Sasa wamekuwa Na hamu ya kuona chombo ama Mwandishi anamhoji Rais wa nchi Na hii Ni kutokana Na mambo yanayoendelea nchini.BBC wamekuwa wa kwanza kumpata Rais Samia,kimkakati wamefanikiwa mbele ya Vyombo vya ndani vikiwemo Vyombo vya Chama Na Serikali.

BBC wamefanikiwa kukidhi matarajio ya watazamaji,wasikilizaji Na wafuatiliaji wa Vyombo vyao(Audience expectation),Kwa mahojiano yaligusa maeneo yote ambayo mtazamaji Na msikilizaji alitarajia aulizwe Rais Samia,mfano,Tozo,Demokrasia,Corona,Sakata la Mbowe na Suala la Watanzania wanaoishi nje.

Sehemu ambayo BBC walipata changamoto Ni Kwenye kumridhisha msikilizaji/mtazamaji (Audience satisfaction).

Kwa kawaida mahojiano Kama hayo yana misingi yake Ili ufike Kule anapotaka "audience" wako Na kutoaacha maswali .

Mahojiano mazuri yanaanza Na maswali ya msingi(Basic questions),na Hapa Mwandishi ama Mtangazaji huuliza maswali yanayolenga 5W+H Kwa Maana ya What,Where,When,Why,Who and how.
Na inashauriwa kuanza interview Hivi Ili kujenga kujiamini Kwa mgeni wako asije akaamini mahojiano hayo Ni vita Na yanaweza kuniangusha.

Wabobezi wa mahojiano wanasema,sehemu hii hupambwa na maswali yanayotokana Na majibu(Follow up questions),Mahojiano ya BBC Bahati mbaya yalikosa "Follow up" questions"

Kwa mfano Samia aliulizwa kuhusu Sakata la Mbowe,ambalo kiufundi Samia alitakiwa alikwepe kwani lipo mahakamani.Kwenye majibu yake Samia alisema Kesi ya akina Mbowe ilianza tangu Mwaka Jana mwezi Sept Na wenzake Mbowe washahukumiwa.

Swali lilitakiwa Ni akina Nani hao?maana taarifa zilizopo Ni Kuwa katika waliokamatwa Baadhi DPP aliwafutia mashtaka,Na wengine wapo Rumande Na Bado Jamhuri haijaanza kupeleka ushahidi,hao anaosema Rais Samia Kuwa wameshahukumiwa Ni akina Nani?BBC wangemuuliza.

Samia alisema Vyama vya Siasa nimekuwa vinafanya maandamano Kwa kuchoma magari Na kuharibu mali,BBC wagemuuliza,Ni Lini Na wapi jambo hilo lilifanyika.

Eneo lingine muhimu Kwenye mahaojiano Ni kuulizwa "Packaging questions" haya Ni maswali ambayo yana nukuu ya Katiba,Sheria,Sera,Kanuni,Taratibu,matamko,takwimu,tafiti Na ripoti.

Bahati mbaya,maswali yote ya BBC hayakuwa Na rejea ya
1.Katiba
2.Sheria
3.Kanuni
4.Sera
5.Takwimu
6.Tafiti
Na hii ilimpa nafasi Rais Samia kujibu maswali kikawaida mfano Swali kuhusu Mikutano ya vyama vya siasa,Swali lilitakiwa kutengenezwa Kwa kutumia rejea Na Katiba Na sheria ya vyama
Vya siasa .

BBC wangemuuliza Samia,kinachotakiwa kusubiri Kipindi cha Uchaguzi Kwa mujibu wao sheria Ni "Civic education" ama "Voters education" ?

Swali Kwa Samia kuhusu Uhuru wa Vyombo vya Habari lilitakiwa Kuwa Na rejea ya sheria ambazo zimekuwa zinalalamikiwa Na Serikali haijazitanyia marekebisho,mfano sheria ya Takwimu,Huduma za Vyombo vya Habari,makosa ya mtandao,Maidhui ya Utangazaji,Usalama wa taifa,Utangazaji,Magazeti,Magereza,Jeshi la polisi,Makosa ya adhabu n.k.

Swali kuhusu Vyombo vya Habari Kuwa huru,lilihitaji rejea ya Kwa nini Mpaka Sasa magazeti ya Mawio,Mseto Na Mwanahalisi ambayo yenyewe hayakufutiwa Usajili Na yalishinda kesi mahakamani hayajatejeshwa Na kuwekwa kapu Moja Na gazeti la Tanzania Daima ambalo lilifutiwa Usajili?

Sehemu ya Mwisho ya mahojiano ambayo ndiyo imewafanya akina Tido Mhando,Tim Sebastian,Aman Pour,Kopp,kuendelea Kuwa magwiji Kwenye mahojiano.

Na inawafanya watangazaji wa Sasa akina Mnete,Chilumba,Khelef,kuna nyakati namuona Nyanda,Yupo Nyoni wakati Fulani nilimuona Mahela Sam Ni sehemu ambayo tunasema Mwandishi ana chunguza (Probe).

Hapa maswali yote yanayoulizwa yanatakiwa kutokana Na nyaraka ulizonazo,mara nyingi utamuona Mwandishi anasema "Hii Ni ripoti ambayo inaonesha" huku akimuonesha mgeni wake Na watazamaji wake.

Wakatibiwa sakata la Escrow,aliyekuwa Mtangazaji wa Star TV Joyce Mwakalinga,alifanya Hiki,alifanya mahojiano Na Prof Tibaijuka,kila Prof alipojaribu kukataa alioneshwa ushahidi.

Eneo hili wengi huwa hatufiki tu napokuwa tunawahoji wageni wetu Na Bahati mbaya jana BBC hawakufika pia.

Mwisho wa yote kumhoji Rais tena Ikulu siyo Kazi Rais ina taratibu nyingi.Hongereni BBC.

Asubuhi njema.
Nguli ni nguli tuu!. Asante Dotto Bulendu kwa unguli huu.
P
 
Hii haikuwa "Hard Talk" iliyofichua hadi vifo vilivyokuwa vimefichika.

"Hard talk" hufanyika nyumbani kwa beberu na mwana habari asiye na cha kupoteza kwenye nchi husika.

Manguli wa "hard talk" huwa ni "wanasheria mahiri" aina za akina Murtaza Lakha (rip), Masumbuko Lamwai (rip), na wa namna hiyo.

Kwani Kikeke hajipendi? Hana ndugu au jamaa hapa nchini ambapo sheria ni ule ulio msimamo wa rais?

Kwani anapopanga kustaafu na kurejea Tanzania atakuwa mgeni wa nani kwenye nchi iliyojaa teuzi:

IMG_20210810_081834_315.jpg

hadi hizi nazo ni rasmi?

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Alipofikia Kikeke panatosha sana mbivu na mbichi mbona zimeanikwa?
 
Dotto Bulendu ni mashine ya kusaga na kukoboa namkubali sn jamaa ana uwezo mkubwa kupita kiasi

1. Dotto Buledu 2. Aloyce Nyanda 3. Paschal Mayala(tamaa tu zimemharibu lakini ni jembe) 4. Odeba wa star TV
Hapo Kwa mayala andika (njaa) alafu endelea na hoja yako sasa
 
Nilikuwa siamini jibu kutoka kwa hajath mh Samia,mbowe hawezi kuwa Gaidi labda bibi wa shungi haelewi maana ya Nemo Gaidi,mbowe hawezi kuua viongozi labda mama angesema kuwa mbowe alimuua kiongozi gani.muda Ni hakimu mzuri.
 
Kila uzi unaandika hivyo.Ndiyo kaulimbiu yako hadi watu waache kuhoji muhojiwa na muhojaji walivyopuyanga?
Wanaouliza kwa nini Mbowe amekamatwa sasa na si vinginevyo wanasahau kuwa Mbowe, Lema, Meya wa zamani Ubungo Boniface walikamatwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa na kabla Rais hajaapishwa kwa kuchochea maandamano yasiyo na kikomo kupinga matokeo. Mambosasa alihojiwa na vituo vya ITV na TBC na kutoa madai hayo hayo ya ugaidi.
 
Dotto Bulendu ni mashine ya kusaga na kukoboa namkubali sn jamaa ana uwezo mkubwa kupita kiasi

1. Dotto Buledu 2. Aloyce Nyanda 3. Paschal Mayala(tamaa tu zimemharibu lakini ni jembe) 4. Odeba wa star TV

Mayalla ni useless
 
Wanaouliza kwa nini Mbowe amekamatwa sasa na si vinginevyo wanasahau kuwa Mbowe, Lema, Meya wa zamani Ubungo Boniface walikamatwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa na kabla Rais hajaapishwa kwa kuchochea maandamano yasiyo na kikomo kupinga matokeo. Mambosasa alihojiwa na vituo vya ITV na TBC na kutoa madai hayo hayo ya ugaidi.
Unaishi kwa kutegemea misafara ya viongozi utajulia wapi mambo msingi?
 
Wanaouliza kwa nini Mbowe amekamatwa sasa na si vinginevyo wanasahau kuwa Mbowe, Lema, Meya wa zamani Ubungo Boniface walikamatwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa na kabla Rais hajaapishwa kwa kuchochea maandamano yasiyo na kikomo kupinga matokeo. Mambosasa alihojiwa na vituo vya ITV na TBC na kutoa madai hayo hayo ya ugaidi.

Kupinga matokeo ya kihuni ya uchaguzi ni ugaidi? Kwa hiyo mpore uchaguzi tukiona kwa macho yetu, kisha tukipinga nyie nyie waporaji mtuite magaidi?
 
Yaani akina sheikh farid na wenzake wake acquitted na ugaidi then mbowe ndie awe gaidi?

Bi mkora anafeli, ila ajue kwamba mdude anao wembe wake
 
Lazima tuelewe mahojiano yale ni baada ya Raisi kama Taasisi kukubali kufanya mahojiano, ili akubali ni lazima aonyeshwe au aelezwe anaenda kuulizwa nini na hapo ndipo tatizo linapoanzia. Kunakuwa na editing ya maswali.

Kikeke hakuwa na uwezo wa kuuliza hayo uliyashauri sababu everything there was pre-planned, publicity stunt.
Sipingi ulichosema, lakini nadhani ni fedheha kubwa kwa shirika kubwa kama BBC na mtangazaji wake kushindwa kabisa kukidhi kiu ya watu wenye kutaka kuelewa kwa kuuliza maswali yenye vielelezo.
 
Tathmini yangu ya juu ya mahojiano kati ya BBC Na Rais Samia Suluhu Hassan.

Na Dotto Bulendu (MwanaPuge).Nikiandika kutoka kijijini Puge.
@@@@@@
Kikeke na samia ni waswahili wazuri. Ungelifahamu hilo usingetaka kikeke amuulize samia lini chadema wameandamana maana muulizaji ameelewa lugha ya samia.
 
Back
Top Bottom