Dotto Bulendu: Tathmini yangu juu ya mahojiano kati ya BBC na Rais Samia Suluhu

Hakuna udikiteta hakuna mabaya yasiyo na mwisho Duniani waliwepo akina magufuli, Bokasa, Gadafi, Sadam Hussein, Elibashiri, Idd Amin dada, chiluba, Abacha na wenzao wapo wapi leo?
 
Usikute Polisiccm walikuwepo jirani wakimsikiliza ateleze tu aone moto wao ndiyo maana kikeke alifanya interview ya uoga mwingi
 
..maswali ya Salim Kikeke yalikuwa marahisi.

..sasa kwanini majibu ya Maza yakakosa weledi na yakawa na mapungufu kiasi kile?
 
Kuna mkoa Fulani miaka kenda,Polisi wakienda kupekua chumba kilichohifadhi pembe za ndovu walikuwa wanakuta mavi,wakikamata gari zake anawachia Polisi na kuahidi atakwenda lipa faini ck inayofuata.
Akienda kulipia faini gari haina matairi.Polisi wakaacha uonevu
 
Sasa how come kukamatwa kulikotokana na "ugaidi" wa kupinga matokeo ya uchaaguzi wa Octoba kesi yake iwe
....ilianza tangu Mwaka Jana mwezi Sept Na wenzake Mbowe washahukumiwa.
Au mimi ndo sielewi?!
 
Nakubaliana na wewe...

Na kimsingi kuna jambo moja la msingi hatufahamu!!

Kujaribu kumshukutumu Kikeke ni sawa na kuhalalisha majibu ya SSH!!

Kwamba, SSH alijibu vile kwavile ndivyo alivyoulizwa kumbe, kama ulivyosema, yeye kama yeye ndie alitakiwa kwenda beyond ya vile alivyoulizwa!!

Yeye ndie alitakiwa kufahamu wenye kiu ya kufahamu anasema nini sio BBC bali ni Watanzania!!!

Sio BBC ndio wenye kiu ya kutaka kufahamu SSH ametowa wapi mamlaka ya kupiga marufuku mikutano ya kisiasa wakati hiyo ni haki ya kisheria, bali ni sisi Watanzania ndio tunaotaka kufahamu SSH anapata wapi mamlaka hayo!
 
Omba fursa, nafasi ya kuandaa maswali umuulize rais hayo maswali.
 
Pale angekuwepo zuhura yunus mamayenu angedata
 
Mambosasa yuleyule wa sakata la Mo? Tangu enzi za Mahita mapolisi walishakaukiwa weledi.
 
Nguli ni nguli tuu!. Asante Dotto Bulendu kwa unguli huu.
P
Nakubali ila kama mwanataaluma naona siku nyingine akumbuke kwamba mwandishi analazimika kusoma sana, kusilikiza sana na kutaka kujua (curious). Hili halikufanywa ipasavyo hivyo haikuwa kama ilvyotarajiwa kutoka kwa mwandishi nguli kama yeye.
 
Ha ha ha Nchi iliyojaa teuzi
 
Unajichanganya sana. Next time jifunze namna nzuri ya kuwasilisha hoja
 
Mkuu Samia angejibuje kitu asichoulizwa? ukweli Salim alipwaya hakufanya Homework yake vzr
 
Mkuu Samia angejibuje kitu asichoulizwa? ukweli Salim alipwaya hakufanya Homework yake vzr

..muuliza maswali huwa na malengo yake.

..muulizwa maswali pia huwa na malengo yake.

..mimi sijasema Raisi alitakiwa kujibu vitu ambavyo hakuuulizwa.

..nilichoshauri ni kwamba Raisi angetoa majibu ya kiufasaha na kisomi zaidi kuliko alivyofanya.

..kwa mfano, Raisi ameonyesha kupinga mikutano na hadhara na maandamano.

..Lakini hakueleza ni sheria gani inayomruhusu kufanya hivyo.

..Raisi pia amedai wako baadhi ya washirika wa Mbowe ktk tuhuma za ugaidi, uhujumu uchumi,..ambao wamekwisha hukumiwa. Maelezo hayo ni ya UONGO.

..Kwa hiyo tuna tatizo la majibu ya UONGO. Pia tuna tatizo la majibu ambayo hayana msingi wa KISHERIA.
 
Mtu ambae hana akili utamjua tu.. kwahiyo Mbowe amekamatwa kwaajili ya maandamano?
 
Shukrani kwa ufafanuzi manake amejionesha alivyo mweupe kichwani
 
Lini wapinzani walihukumiwa kwa kesi za kigaidi? na lini wapinzani waliandamana wakachoma matairi barabarani?
Rais amezungumzia maandamano katika nchi zetu mara nyingi ni yale ya kufanya ghasia hajasema kuna chama kimechoma magari. Ndiyo maana katoa case ya America maandamano yao yalivyo na sisi. Nadhani ugumu ni kuelewa concept ..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…