DOKEZO Dotto Magari atasababisha watoto wengi kukataa shule

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest

Habarini za asubuhi. Kama mdau wa elimu sipendezwi na hawa watengeneza maudhui wa mtandaoni ambao wamekua wakikashifu wasomi na elimu kwa ujumla.

1. Ni ukweli usiopingika kwamba wasanii wengi imeonekana wamefanikiwa kuliko wasomi walio wengi lakini haimaanishi elimu haina umuhimu kwa kizazi chetu cha kitanzania.

2. Tumeona juhudi za serikali kupitia wizara ya elimu ikihamasisha vijana kusoma kwa wajengea mazingira wezeshi lakini wasi wasi unakuja pale anapotokea mtu wa aina hii tena mwenye ushawishi wa mitandao ya kijamii kukashifu elimu. Swali la kujiuliza ni kweli watoto wetu watakubali kuendelea kusoma wakiona maudhui wanayoyatengeneza watu kama Dotto Magari?

3. Kama wasanii hawa wanaona kuna changamoto ya aina yoyote katika mfumo wa elimu yetu ni vyema wakatoa mawazo ya namna ya kuboresha na sio kutoka hadharani na kukashifu waliosoma.

Ombi langu kwa serikali kupitia wizara ya elimu na wizara ya sanaa kuangalia aina ya maudhui wanayotoa hawa wasanii wetu na ikipendeza wapewe onyo hadharani ili kukemea tabia kama hizi zinazoweka elimu ya vijana wetu hatarini.
 
View attachment 3075466

Ngoja siku akiugua na aende hospital akutane na wasomi na itabidi wamuambie aende kwa wasiokuwa na elimu wenzake
 
Sema njia yao ndogo, ni kamishina tu wa TRA na mkurugenzi wa hizo halmashauri wanazotoka.

Yaani kuwapigia mahesabu ya personal income etc, bado pia service levy, leseni za biashara etc, mbona watarudi kuwa wadogo ka pilitoni.

Na uzuri sisi wasomi tumesha wa-note watakoma!
 
wauza madawa ya kulevya akili zao fyatu hawa na wanajua wakisifia serikali wanakamilisha deals zao.
 
Sheria ya kuwapiga viboko hadharani watu kama hawa iletwe tu kwa kweli. Haiwezekani mtu anaishi kiujanja ujanja tu halafu anawakashifu waliosota darasani kisa tu yeye ana vijisenti uchwara
 
Back
Top Bottom