A
Anonymous
Guest
Habarini za asubuhi. Kama mdau wa elimu sipendezwi na hawa watengeneza maudhui wa mtandaoni ambao wamekua wakikashifu wasomi na elimu kwa ujumla.
1. Ni ukweli usiopingika kwamba wasanii wengi imeonekana wamefanikiwa kuliko wasomi walio wengi lakini haimaanishi elimu haina umuhimu kwa kizazi chetu cha kitanzania.
2. Tumeona juhudi za serikali kupitia wizara ya elimu ikihamasisha vijana kusoma kwa wajengea mazingira wezeshi lakini wasi wasi unakuja pale anapotokea mtu wa aina hii tena mwenye ushawishi wa mitandao ya kijamii kukashifu elimu. Swali la kujiuliza ni kweli watoto wetu watakubali kuendelea kusoma wakiona maudhui wanayoyatengeneza watu kama Dotto Magari?
3. Kama wasanii hawa wanaona kuna changamoto ya aina yoyote katika mfumo wa elimu yetu ni vyema wakatoa mawazo ya namna ya kuboresha na sio kutoka hadharani na kukashifu waliosoma.
Ombi langu kwa serikali kupitia wizara ya elimu na wizara ya sanaa kuangalia aina ya maudhui wanayotoa hawa wasanii wetu na ikipendeza wapewe onyo hadharani ili kukemea tabia kama hizi zinazoweka elimu ya vijana wetu hatarini.