DP World anapewa kazi ya kupakua na kupakia Makontena tu, sio Bandari yote ya Dar wala si nje ya Dar

Mkuu, kwa sasa Bandari ndo inachangia pakubwa kwenye pato la taifa yaani 35%-37% ambayo ni Trilioni 7 kwa Mwaka. DP World matarajio ni kwamba bandari itaweza kuingiza Trilioni 26 kwa Mwaka ndo maana nikasema 97%.

Kama Trilioni 7 ni 35%) Je, Trilioni 26 itakuwa ni asilimia ngapi? Nimepiga hesabu hivyo nikapata 97% Makadirio.

MASAHIHISHO

Bandari inachangia 35% kwenye bajeti ya Tanzania na mategemeo ni ichangie 67% kwenye Bajeti
 
Hii ngoma inafanya kila mmoja atoke pangoni kuja kutetea kwa kila namna!! Na ukishaona sintofahamu kama hii, jua tu kuna something wrong!!
 
Kapewa Bandari ngapi Tanganyika? Kapewa Bandari ngapi Zanzibar? Mkataba ni wa miaka mingapi?
 
Swala la bandari ni la muungano sasa mbona Zanzibar haishiriki neema ya dp world
Mkuu, ni kweli swala ni la Muungano. Nami nakuuliza Swali: Mbona TICTS ilikuwa Bandari ya Dar Es Salaam lakini haikuwa Bandari ya Zanzibar wala Mtwara. Nahisi utakuwa nawe umepata taarifa za uongo kwamba DPW anapewa bandari yote. Yule anapewa eneo alipokuwa TICTS baada ya Mkataba wake kuisha.
 
Tanzania maboga mengi.. watu wanahadaika na Hoja zilizojaa siasa na kufungamana na manufaa ya chama. Hii ya DP inechambuliwa na watu kisiasa sana kuliko kiuchumi.. imetumika kikampeni
 
Nilidhani unakuja na kipengele kwenye mkataba kinachosema hawapewi bandali yote au zote.
Pia kinachoonesha ukomo wa mkataba.
Acha uzwazwa
 
Mimi sio chawa na jitambua siwezi ni kapinga kitu cha kjleta manifa katika nchi ili kufurahisha wachache.
Hata Mheshimiwa Mbowe wasaidizi wake walimdanganya sababu walikuwa hawajasoma waelewe wakakurupuka kumpa habari za Uongo. Pia kuna uzembe kwenye vyama vyetu vya Upinzani. Haya makubalinao ya DPW yapo tangu tarehe 25 Oct 2022, hawajajadili chochote wala haikuwa kificho. Baada ya kusikia yanapelekwa Bungeni yapitishwe kama azimio la Bunge ndo wakaanza kutia fitina na kuwapotosha Watanzania ili kutia preaha bunge lisipitishe. Lakini ukweli wlaikuwa na muda wa kutosha kufanya hivyo.
 
Mkuu mbona kama wewe ndiyo unatupotosha? Kila mwenye akili timamu anajua hicho unachokisema wala hakijaonekana hivyo kwenye mkataba.
Jipange unapopiga propaganda zako ziwe na uhusiano japo na ukweli.
Mkuu naomba unisaidie kujua nilipo potosha na unisaidie kunisahihisha ilinami niwe na huo uelewa ulionao. Wapi nimepotosha? Na usahihi ni upi?
 
Acha Kupotosha Poyoyo wewe.
Dpw hawapewi eneo katika bandari Bali wanapewa Bandari yote na nyinginezo katika Nchi Yetu.
Kuna Tofauti Kubwa Kati Mkataba wa Ticts Na Mkataba wa Dpw.
Mkataba wa ticts ulikuwa na ukomo kuanzia eneo la kumiliki mpk muda wakuhudumu.
Huu wa dpw hauna ukomo lkn pia anapewa bandari zote za nchi ya Tanzania Kasoro Zanzibar.
Msituone Tu Watoto Kiasi hicho.
 
Nadhani Uungwana ulitakiwa ulete hoja yako au useme wapi nimedanganya ndo unitukane ili kufurahisha nafsi yako. Mengine unajishushia heshima Mkongwe kama wewe kushindwa kujadiliana kwa hoja.
Umeandika ujinga halafu unaita hoja ambayo unataka ijibiwe.

Ndio maana nikuambia tu tangu awali kuwa huu ni Ujinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…