DP World anapewa kazi ya kupakua na kupakia Makontena tu, sio Bandari yote ya Dar wala si nje ya Dar

Nilidhani unakuja na kipengele kwenye mkataba kinachosema hawapewi bandali yote au zote.
Pia kinachoonesha ukomo wa mkataba.
Acha uzwazwa
Hicho kitu hakipo wala huo Mkataba haupo. Haya yanayojadiliwa ni Maazimio au makubaliano yapi yawekwe kwenye mkataba. Sio Mkataba.

Hayo maneno kwamba kuna mkataba umesainiwa umeyatoa wapi? Usikute umeona makubaliano na maazimio ya Bunge ndo unayoita Mkataba
 
Soma hapo kwenye kifungu cha pili uone kama wameandika posa au mkataba
 
Sawa basi tukubaliane tu kuwa hayo maazimio ni yakipuuzi.
Na walioyapitisha tuwaite tu kuwa ni wapuuzi
 
Kuna kikubdi cha wanasiasa ndo wanapotosha na wala hawana utalaamu wa mambo haya...Eti bandari zinauzwa !

Ujinga tu kuleta hofu kwa watu .
Hata mwinyi tulimtetea sana kwenye sakata la loliondo,hadi pale waarabu walipojitokeza wenyewe na kukiri kuwa mzigo umeenda jumla.
 
Mkuu watu wanasema kuhudu DPW? Tutonye na sisi tujue aisee. Kuna nini huko kwenye huo uchambuzi? Tuwekee hapa tuuone.
embu niachie email yako nikutumie kitu. mm taarifa zao nimezipata siku hizi za karibuni kutoka chanzo kinachoaminika
 
Hahahahah hahahahahhahahah

Imeisha hiyoooooo

Watu wanavurugana tu huku maubongo yao

Ova
DP World anakuja ondoa Mawakala feki

Anakuja ondoa upigaji

Anakuja ondoa wenye magari wapumbavu maana yeye atatumia reli kuondoa msongamano Dsm, maana yake mzigo ukishuka fasta unapelekwa Kwala.

Na huenda akawekeza Tazara pia ili mizigo isafiri kwa reli.
 
Tanganyika sio aridhi ya kugawa Kwa wajomba
 
Ni afadhari ya mzungu kuliko mwarabu.
 
Sasa hivi kila mtu huko serikalini anajibu tu baada ya kuona watu wamecharuka na hawataki ujinga.
Hivyo wanaziba viraka kutokana na maoni ya watu keep sha wanataka wachukue point 3 bila kucheza.
 
Mwaka 2010 gari zetu tatu ilibidi ziuzwe kulipia storage na handling charges hapo bandarini ! Ilinifanya niuchukie hata utawala uliokuwepo !!
 
Ni afadhari ya mzungu kuliko mwarabu.
Umeambiwa mpaka huko kwa wazungu hao waarabu wamepewa Bandari kuziendesha pamoja na timu zao kubwa za mpira zinaendeshwa na waarabu πŸ˜…πŸ˜…πŸ™πŸ™
 
Unadhan mpaka viongoz wa dini wametia shaka kweny hili mpaka wakadiriki kusema ni lazima serikali isikilize na kuangalia maslahi ya Taifa kuna nn? Sio viongoz wa dini pekee bali wengi wakiwemo wanasheria. NB; Kwa walivyo wapitisha miswada yaan piga kelele, ongea mpaka koo lipate tonsils but watapitisha tu!!
 
Mkuu ungeweza kujenga hoja bila kuita mtu poyoyo.

Hayo uliyo yaandika ni Uongo. Ukweli ni anapewa sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam tu.

Nani kakulisha huo uongo? Kichwani wamekujaza taarifa za uongo za Propaganda za Kenya. Tuoneshe waliposema hivyo.
 
Umeandika ujinga halafu unaita hoja ambayo unataka ijibiwe.

Ndio maana nikuambia tu tangu awali kuwa huu ni Ujinga.
Basi ni vyema ungeandika hicho ambacho si ujinga ili watu wajue mbivu na mbichi. Sababu hii post ya tatu hakuna ulichoandika cha kusaidia nchi
 
Hivi zanzibar wao hawataki hayo manufaa?
 
Wanachosubiri ni kusikia nani kateuliwa wapi nani katoswa huku wakiishi kwa matumaini kuwa zamu yao itafika wakisahau umri unasogea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…