DP World inatisha 2: Tazama bandari inazozihudumia Uingereza

DP World inatisha 2: Tazama bandari inazozihudumia Uingereza

Tupe mfano wa nchi masikini kama ya kwetu iliyopata faida na maendeleo kwa uwekezaji wa DP katika bandari zao.Huko Uingereza DP hajaenda kuongeza chochote zaidi ya pesa za gesi.
Na mkataba uwekwe humu
 
DP World wameunda biashara iliyounganishwa kwa ubora wa hali juu - bandari mbili za kina kirefu zenye vituo vya reli ya mizigo huko London Gateway na Southampton, kituo cha vifaa (logistics park) inayopanuka kwa kasi na biashara ya juu ya programu za software zinazotoa viunganisho vya mtandaoni kwa wateja na udhibiti wa usalama.

DP World wamewekeza kwenye miundombinu sahihi ya biashara na masuluhisho mahiri ya vifaa kwa wateja wao wsnaotumia bandari hizo. Kila mwaka, DP World kupitia bandari hizo wanasafirisha takriban kontena milioni 3.6 - bidhaa zenye thamani ya £43 bilioni katika kontena hizi husafirishwa kwenda na kutoka nchi zilizo nje ya EU.

DP World wanaamini katika soko la Uingereza wana matarajio na rasilimali za kutosha kuhimili na kuboresha ukuwaji, kusaidia biashara, kuunda nafasi za kazi na kuboresha viwango vya maisha. Utaalam wao wa biashara unaoongoza katika sekta ya bandari, unatambuliwa kwa kutoa ushauri wa kiufundi na wa kimkakati mara kwa mara kwa Serikali ya Uingereza.

Chanzo: DP World in the UK

Waarabu wa Dubai wanatisha kwenye biashara.

Mama Samia hujakosea kabisa kuamuwa kuwaleta DP World Tanzania.

Tupo na wewe 100%.
Tatzo sio waarabu....tatzo ni hizo terms za mkataba..Yani ni kama hati ya ndoa
 
Una hisa gani na dp?badla ya kuangalia mapagufu ya mkataba ww umekomalia dp.sisi hatuna shda na dp bali tuna shda na AINA YA mkataba wa dp na bandar yetu....

Credits GEBA2013
 
Wewe maslahi gani ya nchi unayoyajuwa wewe zaidi ya Mama Samia Suluhu Hassan?

Wacha upoyoyo wewe.
Kwahiyo kwa akilizako mwenye kujua maslahi ya nchi ni mama samia pekee cyo? Hivi kwa umri ulio nao hapo ndo mwisho wako wakufikiri au matumizi ya kichwa umehamishia tumboni ....... Time will tell
 
Ndugu zanguni

Naomba niwakumbushe tu kua huduma za Uwanja wa ndege wa Dar zinaendeshwa na Swissport ambayo ni kampuni ya Switzerland toka mwaka 1985 ambapo wengi mnaopiga mayowe mlikua bado hata haijuilikani kama mtakuaja Duniani. Lakini kwa kua utendaji wao ni wa kiwango cha juu ndio maana wako mpaka leo pale

Haya tusitokwe mapovu. Swissport wanahudumia viwanja zaidi ya 200 duniani. Kwa wale mliowahi safiri lazima umeona mabango yao

TICTS wako bandarini miaka 33 sasa na hawajawahi nunua hata crane moja na utendaji wao umekutuumiza sana Wafanya biashara. Yaani mara kwa mara tumezoea kumuona Mh Waziri Mkuu akienda pale kuwahimiza wafanye kazi kwa bidii makontena yatoke. Hata hii ya masaa 24 ni baada ya Mh Waziri Mkuu kuwaambia wafanye kazi masaa 24 kuondoa msongamano port

Ndugu zanguni , sijawahi sikia mtu akilalamika kuhusu Swissport sababu utendaji wao ni wa kiwango cha juu sana.

Tumechoka hii aibu ya meli kukwepa bandari ya Dar sababu ya miundombinu mibovu.

NB: Natoa kauli hii nikiwa mmoja wa watumiaji wakubwa wa bandari na sio chawa asiejua hata meli ina magurudumu mangapi.

Niko tayari kukaa meza moja na Rafiki yangu wa Zamani Lema tulijadili hili ili wazi na kwa Data. Juzi nimemsikia akiongea kwa data za kupotosha. Ili mwananchi wa kawaida aelewe ninaomba niwekwe uwanja mmoja nae tujadiliane kwa hoja. Naamini hata yeye atanielewa na atakubaliana nami
Hizi zote sisi tunaita ni MBA MBA MBA.... jikite kwenye hoja ya mikataba hakuna kati yetu asiye jua umuhimu wa uwekezaji na hakuna asiye penda wawekezaji mbona swisport wapo tangu 1985 na hatuwasemi
 
Kwahiyo kwa akilizako mwenye kujua maslahi ya nchi ni mama samia pekee cyo? Hivi kwa umri ulio nao hapo ndo mwisho wako wakufikiri au matumizi ya kichwa umehamishia tumboni ....... Time will tell
Wewe unayajuwa zaidi ya mama Samia.

Maslahi yako umejitimizia?
 
Hizi zote sisi tunaita ni MBA MBA MBA.... jikite kwenye hoja ya mikataba hakuna kati yetu asiye jua umuhimu wa uwekezaji na hakuna asiye penda wawekezaji mbona swisport wapo tangu 1985 na hatuwasemi
Bendera yao ina msalaba.
 
Mkataba upi unaouzungumzia wewe, wa Kuendesha bandari?
Kivyovyote utakavyouita...wa kuendesha...kuuza...kubinafsisha...makubaliano...ni sawa..ila Kuna mapungufu....na Kuna haja ya kurekebisha au kutoa maelezo sahihi kwa kutumia watu sahihi...(sio wanasiasa)...binafsi Sina shaka na DPW kama Wana uwezo wa kuendesha bandar zetu...wanao Tena sana tu...tatzo lililopo ni hizo terms za mkataba/makubaliano/IGA..
 
Huu ujinga wa waislam mkiona mwarabu mna m treat kama ndugu yenu sijui utaisha lini
mnamtetea mpaka basi
ungetuwekea mkataba wa huko nchi zenye akili tulinganishe na huu wa kwetu
Kila Muislam akiunga Mkono Mkataba wa DP World lazima muunganishe uungaji wake mkono na dini yake, Mkiitwa Wadini mnalalamika
mbona Mie Muislam na siungi mkono kwa vyovyote vile Mkataba wa DP World?
 
DP World wameunda biashara iliyounganishwa kwa ubora wa hali juu - bandari mbili za kina kirefu zenye vituo vya reli ya mizigo huko London Gateway na Southampton, kituo cha vifaa (logistics park) inayopanuka kwa kasi na biashara ya juu ya programu za software zinazotoa viunganisho vya mtandaoni kwa wateja na udhibiti wa usalama.

DP World wamewekeza kwenye miundombinu sahihi ya biashara na masuluhisho mahiri ya vifaa kwa wateja wao wsnaotumia bandari hizo. Kila mwaka, DP World kupitia bandari hizo wanasafirisha takriban kontena milioni 3.6 - bidhaa zenye thamani ya £43 bilioni katika kontena hizi husafirishwa kwenda na kutoka nchi zilizo nje ya EU.

DP World wanaamini katika soko la Uingereza wana matarajio na rasilimali za kutosha kuhimili na kuboresha ukuwaji, kusaidia biashara, kuunda nafasi za kazi na kuboresha viwango vya maisha. Utaalam wao wa biashara unaoongoza katika sekta ya bandari, unatambuliwa kwa kutoa ushauri wa kiufundi na wa kimkakati mara kwa mara kwa Serikali ya Uingereza.

Chanzo: DP World in the UK

Ila inatumika nguvu kubwa
 
Kivyovyote utakavyouita...wa kuendesha...kuuza...kubinafsisha...makubaliano...ni sawa..ila Kuna mapungufu....na Kuna haja ya kurekebisha au kutoa maelezo sahihi kwa kutumia watu sahihi...(sio wanasiasa)...binafsi Sina shaka na DPW kama Wana uwezo wa kuendesha bandar zetu...wanao Tena sana tu...tatzo lililopo ni hizo terms za mkataba/makubaliano/IGA..
Mapungufu "hewa"?

Wanasheria wameshapeleka kesi mahakamani. Hamuwaamini wasomi wenu? Waliopeleka malalamiko na wanaotetea na watao amuwa?

Sasa hii tunataka serikali iwachane na kupeleka pesa taasisi za kidini.
 
Back
Top Bottom