DP World kuanza kuendesha bandari ya Dar es Salaam tarehe 01 Novemba 2023

Vibaraka mbatumwa kuja ku- test upepo wa jamii humu?
DP-WORLD ikiingia Bandarini na CCM ndio itatokea nchi kavu Tanganyika kuingia Kaburini.
 
Na warabu wenyewe wakiwa wanasimamia bandari yao kwa njia ya Bluetooth, au vipi? 😆
 
Nilikuwa siungi mkono suala la DP world lakini upumbavu wa TEC umenifanya niiunge mkono Serikali.

Serikali haipaswi kubadili maamuzi yake kwa mashinikizo na vitisho kutoka kwenye vikundi vya dini.
 
Nguvu ya umma itumike kukidosha Chama Chakavu na serikali yake

TEC hawawezi kuwa tayari kuiona CCM inaanguja hata siku moja maana ni chama kinachoweza kulinda maslahi ya kanisa Cathoric na ni ngumu kukiamini chama kingine.

Ni watanzania pekee kwa nguvu moja na akili moja bila mashinikizo yakipumbavu nyuma ya pazia bali dhana ya dhati kwenye mioyo yao kuitetea Tanzania yao.
 
CCM ya sasa sio kama ile ya Nyerere, hata TEC hawapendezwi nayo
 
Hujatueleza kama hao DP World wanaokuja ndio wale wale wa IGA; pamoja na kwamba umejitahidi kutufafanulia ni akina nani wahusika na DP World unayoizungumzia wewe.

Huyo DP World wa rangi yoyote ile, bila ya IGA anayoambatana nayo, huyo tunaweza kukabiliana naye baada ya kuwashughulikia hawa watwana wao waliotaka kutuuza huko utumwani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…