DP World kuanza mchakato wa kuajiri, Wafanyakazi wa TPA wadaiwa kutakiwa kuchagua kwenda DPW au kubaki TPA

DP World kuanza mchakato wa kuajiri, Wafanyakazi wa TPA wadaiwa kutakiwa kuchagua kwenda DPW au kubaki TPA

Mkuu mbona tangazo lipo wazi au mimi ndio sielewi? Huwezi kuwa mtumishi wa serikali halafu hapo hapo ukawa mtumishi wa DPW. Mumishi anachagua abaki TOA au aende DPW na huo ndio utaratibu na hao watumishi wamepewa elimu na muda wa kuchakata suala hili tangu mapema sana.

Kwa ninachofahu na nilichoelewa ni kuwa Ukiamua kwenda DPW utapewa terminal benefits zote kisha unaajiririwa DPW ambapo huko ni private sector na tunajua huko hakuna mbambamba ni kazi kwa kwenda mbele tofauti na serikalini ambako hata uharibu vipi basi unaangaliwa au watakuhamisha kitengo. Lakini private sector huwa wapo strictly.

Sasa hapo ni uamuzi na uchaguzi wa mwajiriwa mwenyewe abaki au aende lakini hakuna aliyetimuliwa wala kulazimishwa kuchagua atakacho
Mleta mada ana upoyoyo fulani hivi.
 
Kwahyo hakutakuwa na wajiriwa wapya??
Watanzania sasa hivi kila fani professional mtu atafute International certification iwe ualimu nk tuache uswahili dunia kijiji sasa hivi mwekezaji akija au kijana akitafuta ajira kimataifa vizuri ajitahidi kwenye fani yake apate International certification kuuzika kiajira kimataifa tuache utoto

Soko la kimataifa la ajira kubwa kuliko local kwa wenye International certification iwe soko la wawekezaji wa nje wajao nchini au kimataifa nje ya nchi Vijana wasomi tafuteni International certification kwenye fani zenu
 
Wanakuwepo critical areas
Ujue wawekezaji wakija huja na teknolojia mpya ambazo huhitaji wanaozijua na serikali haiwezi kubali waje nao wakati watanzania wapo wanaozijua wakati TPA ilikuwa ikiendeshwa teknolojia za zamani hawakuhitaji vijana wajua teknolojia mpya

Aliyesoma mfano computer technology miaka ya 1980 huwezi linganisha na aliyesoma computer technology na kumaliza digrii mwaka jana Wa mwaka jana yuko more current na yuko advanced kuliko obsolete technology ya TPA iliyopo hivyo wataajiri vijana wapya

Pili wa marketing wengi wa TPA mfano wamesoma kingereza tu na digrii za kingereza tu hawana third language kama kifaransa .Soko la TPA liko hadi Central Africa nchi ya kongo ambako lugha kuu kifaransa
Definitely wataajiri watanzania vijana wapya marketing officers wenye digrii za marketing lakini wanajua kifaransa kwa ajili ya kuwa marketing officers wao soko la Kongo tofauti na TPA ambayo ilikuwa haijali hilo kuwa na maafisa masoko wajua kifaransa ambako kuna wateja wengi mizigo ipitayo bandarini

Wapya wataajiriwa wala sio siri.Kuna maeneo wafanyakazi wa TPA waliopo hawawezi enea hata wajitutumue vipi
Degree zao na uzoefu wao haywezi fit kwenye teknolojia za kisasa na utendaji wa kibiashara za kimataifa wa kisasa uletwao na DP World

Mfano Dp world ni kampuni ya kimataifa Auditor na wahasibu wakuu lazima wawe na certification za kimataifa ili wakusaini document wanahisa wa DP World wawe na confidence ya kuanzia mhasibu mkuu au mkrugenzi wa fedha sio awe na Sifa za CPA ya Tanzania awe mhasibu au Auditor wanatakiwa wenye certification za kimataifa kama ACCA nk sio CPA (T) International shareholders wa kampuni yeyote ya kimataifa huhitaji wenye certification za kimataifa.Na wapo na serikali haiwezi kubali waajiri wa nje wakati Tanzania wapo.TPA ilikuwa haiwahitaji hao wenye certification za kimataifa .Hiivyo ajira mpya zitakuwepo

Watanzania wenye sifa za kimataifa ajira zitakuwepo nyingi vitengo vyote iwe IT ,uhasibu,masoko,procurements,Engineering,Port operations etc wataajiri tu hawana ujanja
Aisee nimekuelewa sana sana na umenitolea mifano
 
😂😂😂 Mshambuliaji namba 9
a.k.a Mzee wa minyama
89A8C0A0-6FD2-46C5-A4DC-C6A23A93F455.jpeg
 
Back
Top Bottom