DP WORLD: Mkataba wa Bandari kwa Kiswahili (tafsiri isiyo rasmi)

Unajidanganya,ukiondoa watu wachache tuliopo mitandaoni na wajaa chuki za kibaguzi wa huku mtaani,basi raia wengi wapo na shughuli zao na hawana hata 1 la kuongea juu ya mkataba huu.
 
Uislam ni mwema sana.

Si unaona mama Samia anavyofanya mambo makubwa kwa faida ya Tanzania.


Mama anaupiga mwingi Kimataifa.
Kwani kuna mtu kabisha?? Lakini mama hana huo uvaaji wa mabomu, labda kama anauficha
 
Sijakuelewa.


Mama anaupiga mwingi Kimataifa.
Tuweke ushabiki wetu pembeni na mambo mengine yasiyo na tija. We need investors. Ila lazima kuweka vizuri mikataba yetu. Tuache kuchumia tumboni kwa gharama za wengi.

Halafu wananchi wa Tanzania, wengi sio wa kuhangaika kusoma. Wanapenda simulizi wakiwa wanakunywa gahawa. Unachowaambia ndio wanavyochukulia. Wasomi watanzania waanze kuelimisha watu kwa staha na bila kuweka agenda zenye utata
 
Mleta mada hii tunayojadili alisema Mwalimu alikuwa kiongozi mbovu na akamfungilia uzi. Nilisikitika sana.
Msamehe hajui anachofanya. Kimeumana sasa. Ndio akili zitakaa sawa. Mwalimu sio wa kuchukuliwa kispotspot...na waliojaribu kufanya hivyo, sasa hivi wanabaki kujitetea wakipewa platform waseme walichofanya
 
Nikitulia nitausoma vizuri alafu ndio nitajua nisimame na Mama au la
 
nani aliyekudanganya? Tumkamate achapwe viboko?
 
Mkataba upo vizuri sana, one of the best. Mengineyo ni chuki, husda na jakamoyo.

Mama anaupiga mwingi na tunampa maua yake.
Unaonekana hujausoma huo mkataba umekimbilia kwenye comment tu.
 
Jibu wewe Dubai Ni Nchi?
Dubai ni sehemu ya nchi inayoitwa UAE, kuna Abu Dhabi na majimbo mengine matano yanaunda kwa pamoja nchi inayotwa UAE. United Arab Emirates

Dubai ina mamlaka kamili ya kufanya shughuli za nchi kama ilivyo Zanzibar au Tanzania Bara.

Ni sawa na USA inavyotoa uhuru kwa majimbo yake kufanya biashara na mataifa mengine. United States of America
 
Kwa wanaohitaji mkataba wa DP world, kwa kiswahili nimeuweka hapa, tafsiri imetokana na mkataba ulioandikwa kwa lugha ya kiingereza lengo ni kila mtanzania asome na kutoa maoni kwa maslahi mapana ya Taifa.
Mbona haujasainiwa? Hivi wanatuona sisi mazuzu...hii si tafsiri tu waliyofanya ili kudanganya wabongo. Mkataba unaotufunga ni ule uliosainiwa na Mbarawa na yule Mzanziabr mwingine ambao ni wa kiingereza.
 
Kwa wanaohitaji mkataba wa DP world, kwa kiswahili nimeuweka hapa, tafsiri imetokana na mkataba ulioandikwa kwa lugha ya kiingereza lengo ni kila mtanzania asome na kutoa maoni kwa maslahi mapana ya Taifa.
Mmeanza brainwashing 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mbona haujasainiwa? Hivi wanatuona sisi mazuzu...hii si tafsiri tu waliyofanya ili kudanganya wabkngo. Mkataba unaotufunga ni ule uliosainiwa na Mbarawa na yule Mzanziabr mwingine ambao ni wa kiingereza.
exactly....... ukisoma takataka hii unaon imeandikwa kijuml jumla bila specifiction. Inatoa mamlaka kwa DPw kufanya lolote analotaka mfano, ardhi...imewekwa kuwa atapaha haki za ardhi, haki gani? lazima zitajwe
 
Haya ni Madhara makubwa ya dini zilizoletwa na wazungu na waarabu.

Mmatumbi mweusi ambaye ni muislamu anajiona yuko karibu sana na mwarabu wa dubai kuliko mdengereko mweusi vivyo hivyo mdengereko mkatoriki anajiona yupo karibu sana na mzungu kutoka vatican kuliko mmatumbi mweusi.

Kwa sasa kinachoendelea kuhusu mkataba wa DP ni ushabiki wa kidini. Muislam anaikubali dp mkristu anaikataa.

Tukiachana na ushabiki wa kidini, huo mkataba wao ushavuja na ni mbovu sana. Hata kama wakijaza shingo na kuwekeza, hawatafikia mbali.
 
Mbona haujasainiwa? Hivi wanatuona sisi mazuzu...hii si tafsiri tu waliyofanya ili kudanganya wabongo. Mkataba unaotufunga ni ule uliosainiwa na Mbarawa na yule Mzanziabr mwingine ambao ni wa kiingereza.
Mkataba original ni ule uliosainiwa huu wa kiswahili umetafsiriwa kutoka ule wa kiingereza kwa malengo ya kuwafanya watanzania wengi wauelewe.
 
Kwnye mkataba wamesema wanawekeza shilingi ngapi??
Huo uboreshaji ni wa aina gani, mbona haujaainishwa maeneo na muda wa uboreshwaji?
Mbona mkataba hausemi mwekezaji akizingua tu, anatimuliwa? Yaani mkataba unaonyesha kumfeva zaidi mwekezaji kuliko nchi ya wenye bandari ?
Sijaona mkataba unaanza lini na unaisha lini, kwa maana ya timeframe ya mkataba. Mkataba upo hadi maekezezaji aamue yy basi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…