DP WORLD: Mkataba wa Bandari kwa Kiswahili (tafsiri isiyo rasmi)

Wamepiga kelele weeee kuhusu mkataba, haya sasa umewaletea, sijui watataka nini tena 😁
 
Tony! Punguza mihemko kwenye mambo makubwa ya kitaifa
 
Huo mkataba hauna mantiki yoyote, hatuhitaji mikataba ya kuifunga nchi kwenye masharti ya hovyo kwa jambo dogo la kuendesha bandari.
 
Hii tafsiri imefanywa na artificial intelligence (eg Google Translator) etc na sio salama kuitumia tafsiri hii sisisi kuuelewa mkataba halisi kwani hizo mashine za kutafsiri haziwezi kutoa tafsiri sahihi ya kimantiki (contextual translation). Sijui kwanini watanzania tunatetea sana mambo tusiyoyajua vizuri? Na tunaongozwa katika hili na wabunge wetu vilaza waliopita bila kupingwa!


😊😊
Kwa nini Watu hawaamini Akili na maamuzi ya viongozi wao?


Nguvu kubwa inatumika kutetea hili jambo la DP World.. Na watu wengi wanapinga .. Ni ishara ya kwamba kuna vitu havipo sawa.. ni swala la mda tu

Ubovu wake uko wapi?

Mimi nakubali serikali waingie mkataba na hii kampuni ya kitapeli sina tatizo, ombi langu tu waondolewe kinga za kutoshitakiwa kwa maamuzi ya hovyo hapo baadae.

Huu mkataba siyo wa kampuni, usome hata mwanzo wake tu, unaonesha kuwa ni mkataba wa nchi na nchi.

Wacha kusema uongo.


Mama anaupiga mwingi Kimataifa.

Bandari siyo jambo la Muungano

1. Uhuru umepitiliza
2. Ujuaji mwingi
3. Njaa (Kuna wakosoaji wengine wanatumika na maadui zetu kuhakikisha hatupigi hatua) rejea battle la Bwawa la mwl Nyerere na ujasiri wa mwendazake.
4. Kutafuta kutrend na kuonekana (wanasiasa wanaingia hapa)
 
Uliona wapi watu mnaingia kwenye mkataba halafu unazuiwa hata kununa ukitendewa vibaya?
 
Hatari sana..... tumekwisha kwa kweli.
 
Halafu kuna mimbuzi inaunga mkono hilo

Walahi bora tuandamane tu Samia Out
 
Kifungu kipi kimr+eondoa bandari za Zanzibar? Usiseme uongo. Mkataba huo hapo post #1. Tuoneshe.


Mama anaupiga mwingi Kimataifa.
Mkataba unataja TPA pekee na Zanzibar ina mamlaka yake inaitwa ZPA. Na wiki iliyopita Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar alitamka hadharani mkataba wa DPW hauihusu Zanzibar. Waziri Mbarawa pia amesema hadharani. Wewe uko juu ya hao wawili ili tupuuze maneno yao?
 
kanda maalum za kiuchumi, mbuga....?..mpaka mbuga zetu watu wanapewa....hatari sana
 
Bora ulinge kaa kwa kimombo
Swali fikiri kirishi je huu mkata ni kati ya nchi na nchi ama kampuni na nchi,

Swali fikirishi je mkataba ni kati ya nchi na nchi?, (IGA), ama kati ya kampuni na nchi ya Tanzania
 
SWALI ambalo hadi leo najiuliza,binafsi

Hiii nchi tangu ipate uhuru kuna mikataba mingi imefanywa,mibovu kwa mizuri,mingi sana

mibovu hadi ikaja ikavunjwa mingine kesi mahakamani hadi na leo,Mizuri ipo na mafanikio yake tunayaona wote.

Mikataba yote huko nyuma mizuri kwa mibaya ilifanywa kwa siri Watanzania tulishirikishwa kwenye Matokeo ya mikataba hiyo,ila mwanzoni mwa mikataba ni kimya.

SWALI : Kwanini DP WORLD uwekwe open kiasi hiki kuna nini hatukioni? Kwani tangu Rais huyu aingie madarakani kama nchi ni mkataba wake wa kwanza huu? si kweli ipo mingine mingi,Je mbona hatukushirikishwa?

Kwanini huu tu ndio una makelele mengi? Haya makelele yawe mazuri yawe mabaya naamini kuna ambacho kinaendelea ambacho hatukioni.

Hiii MASS AWARENESS naamini DP WORLD ndio kashauri ifanywe maana anataka akiingia kusiwe na kisingizio cha eti mkataba ulikua siri, yani Huu mkataba kuna BOMU liko hidden kuliko mkataba wenyewe.

Siamini kama shida ni mkataba tu,naamini ipo shida nyingine tusioijua ila shida kubwa ipo ki ufupi hawa DP WORLD kuna jambo wameazimia (tusilolijua)wakiingia, hapa ni wanaendelea kujiwekea maushahidi tu.

Kuna wakati tunatakiwa kujiuliza Kwanini DP WORLD kwanini? si kweli ishu ya vipengele hiyo ishu inarekebishika ila naamini kuna mzinga unakuja na matokeo yake nayaona si mazuri,sijui kama naeleweka,any way yawezekana nisieleweke leo ila nitaeleweka in 10yrs to come,hii comment itafukuliwa tu.
 
Controla! Usiwe na hofu
 
Ibara ya 20 inasemaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…