DP WORLD: Mkataba wa Bandari kwa Kiswahili (tafsiri isiyo rasmi)

DP WORLD: Mkataba wa Bandari kwa Kiswahili (tafsiri isiyo rasmi)

Hakuna mkataba mbovu umewahi kutokea kama huu duniani

Samia akishirikiana na waziri na katibu mkuu wameiuza Tanganyika kwa waarabu

Watanganyika amkeni muitete nchi yenu wajukuu na vitukuu vyenu vitazaliwa km watumwa chini ya nchi ya waarabu ambao wameuziwa nchi

Mkumbuke viongozi waliofanya haya wananufaika na uuzwaji huu wa nchi
Umefanya utafiti kwa mikataba mingapi
Unataka kutudanganya watu wazima?
Hebu kafanya kazi upate mafuta ya kuweka kwenye vibatali vyako leo
 
Nguvu kubwa inatumika kutetea hili jambo la DP World.. Na watu wengi wanapinga .. Ni ishara ya kwamba kuna vitu havipo sawa.. ni swala la mda tu
Wanaopinga wanadanganywa na wenye maslahi yao binafsi
 
Mkataba nimeuweka kwa Kiswahili kwa msaada wa tafsiri ya Google, kama ulivyo.

Kama kuna makosa ni ya kimtandao, muyaainishe tutayafanyia marekebisho (editing) kidogo kidogo.


Naona Watanzania tunadanyana sana hapa JF. Sasa kila mmoja wetu avione na avisome vipengele vyote walivyokubaliana serikali mbili na tutowe maoni yetu. Tuyajadili kiheshima.

Binafsi nauunga mkono huu mkataba wa maendeleo.


Mama anaupiga mwingi Kimataifa.
Shukran sana ukht
Jazakallahu khayran
 
Hiki kipengere ni hatari kuliko hatari yenyewe, yaani hata isipo perform hakuna mtu kujitoa, ni kama ndoa ya kikristo hadi kifo kiwatenge.

“Nchi Wanachama hazitakuwa na haki ya kukemea, kujiondoa, kusimamisha au kusitisha Mkataba huu katika hali yoyote, ikiwa ni pamoja na katika tukio la uvunjaji wa nyenzo, mabadiliko ya msingi ya hali, kukatizwa kwa uhusiano wa kidiplomasia au wa kidiplomasia, au sababu nyingine yoyote inayotambuliwa chini ya sheria ya kimataifa. Bila kujali yaliyotajwa hapo juu, mgogoro wowote kati ya Nchi Wanachama kuhusiana na hali kama hizo utashughulikiwa kulingana na mahitaji ya Ibara ya 20 ya Mkataba huu.”.
Hiki ni kipengele muhimu sana ili tuendelee kunifaika mpaka mwisho wa mkataba
 
Ubovu wake uko wapi?
Ubovu wa huu mkataba ni obligation za dubai hakuna ila kwa upande wa Tanzania kila kitu ni shall. Na pia mkataba hauna muda maalum wa ukomo na pia mkataba huu umegeuka ibara ya 63(3)(e) huu ni just mkataba tuu siyo treaty kwahiyo bunge halina mamlaka ya kuratify na bunge liki ratify treaty inamana inakuwa sheria binding. Pia mkataba umejichanganya haweki wazi kati ya mahakama na bunge ni kipi kiuchambue huu mkataba vitu ni vingi in short mkataba huu uliandaliwa na upande mmoja alafu sisi viongozi wa Tanzania tuka weka sahihi kwa maelezo ya Mkataba huu hata ikitokea dp world wakavunja masharti ya mkataba Nchi ya Tanzania haina mamlaka ya kujitoa kwenye mkataba huo. Ndugu kwani huu ni mkataba tuu au ndoa ya kikatoliki?
Huu mkataba ni tricky na una loop holes kibao za kuleta migogoro mfano sheria itakayo tumika ni ya uingereza hapo hapo unaambiwa mgogoro ukitokea tuta utatua kwa njia ya arbitration Nchini south Afrika swali langu ni moja kwa wataalamu wa private international law hii ni sawa? mgogoro lazima utatuliwe pale ulipo anzia. Haya ndiyo mavitu ya rushwa kusafiri hovyo kutatua migogoro ya Tanzania kwenye nchi za watu. Sheria itumike ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Neno shall limetumika hapa kuikandamiza Tanzania kama sisi ndiyo weaker party kwenye mkataba yani shall limetumika mpaka nashangaa tunapelekeashwa vp na hawa mabedui? Tanzania sio nchi dhaifu kiasi hicho neno shall litumike kutudhoofisha
 
Huu mkataba unakwenda kuingia kwenye vitabu vya kihistoria.
Mkataba wa Kilaghai wa Chifu Hangaya
Yaani ni aibu hata kuutazama
Nawe ni thinker. Ukitaka ku comment kitu uliza kwanza kwa wenye akili
 
Tusisahau kuwa Dubai si nchi bali ni sehemu ya nchi iitwayo Umoja wa Falme za Kiarabu au kwa Kiswahili hufupishwa Himarati (United Arab Emirates).

Dubai ni jiji kubwa la biashara na anasa kama kwetu ilivyo Dar es Salaam. Tanzania ni nchi na dola kamili, ni kebehi na dharau kuingia mkataba na jimbo au sehemu tu ya nchi nyingine badala ya nchi yenyewe.
 
Huu mkataba siyo wa kampuni, usome hata mwanzo wake tu, unaonesha kuwa ni mkataba wa nchi na nchi.

Wacha kusema uongo.


Mama anaupiga mwingi Kimataifa.
Bibi unazeeka vibaya, tangu lini Dubai ikawa nchi? Sema mkataba kati ya nchi na jimbo. Yani wewe ukiingia mkataba wa kuzoa taka na jiji la Newyork utasema umeingia mkataba na USA?. Dubai iko chini ya UAE, ili uwe wa nchi na nchi ilibidi thingies na UAE sio Dubai
Acheni kujitoa ufahamu, huu mkataba umekaa kikanjanja sana, uhuni upo wa kutosha.
 
Back
Top Bottom