CT0007
Member
- Oct 11, 2022
- 20
- 16
Kuhusu bandari mimi siungi mkono ubinafsishaji wake hata kidogo! Ibinafsishwe ili sisi tufanye nini? Kwani uendeshaji wake unagharimu nini ambacho hatukimudu kama nchi? Mbona ATCL inapewa ndege mpya na serikali na bado inapata hasara ila haibinafdishwi?
Bandari inaingiza hasara gani mpaka tuone inatuelemea? Kama Nyerere aliacha madini tuje kuchimba, sisi tukikua kiakili na kiteknolojia, sisi tunashindwaje kutunza bandari tuje kurithisha wanetu?
Naunga mkono uwekezaji wa bandari ila ufanywe na serikali yenyewe au ishirikishe sekta binafsi ya ndani. Sekta binafsi ikajifunze Kwa waliofanikiwa, kisha ije iendeleze bandari ikishirikiana na serikali!( Kama NMB Bank ilivyo, serikali ina hisa na private sekta nayo ipo).
Kwani ni lini serikali ili tangaziaumma na dunia kwamba bandari inabinafsishwa ili umma utume maombi? DP World walishindanishwa na nani kwenye tenda? DP World walijuaje kwamba bandari Dar es Salaam inabinafsishwa? Wamepatikanaje sasa?
Ndugu mdau wa JF, toa ushauri wako nami nijifunze.