DP World walipatikanaje kama hatukuona tenda ikitangazwa?

DP World walipatikanaje kama hatukuona tenda ikitangazwa?

Kwa ufahamu wangu mdogo, sheria(bila shaka ya manunuzi), inataka utaratibu wa kutangaza tender utumike na kisha wahusika waombe na mchujo ufanyike kwa kuzingqtia vigezo vilivyoweka then mshindi apatikane na atangazwe.

Saaa najiuliza huyu DP WORLD alishindanishwa na nani na tangazo la tender liliandikwa au kutolewa kwenye gazeti/ chombo gani cha habari?

Tunaomba majibu kutoka kwa wahusika.
Closed circuit/circus deal

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhusu bandari mimi siungi mkono ubinafsishaji wake hata kidogo! Ibinafsishwe ili sisi tufanye nini? Kwani uendeshaji wake unagharimu nini ambacho hatukimudu kama nchi? Mbona ATCL inapewa ndege mpya na serikali na bado inapata hasara ila haibinafdishwi?

Bandari inaingiza hasara gani mpaka tuone inatuelemea? Kama Nyerere aliacha madini tuje kuchimba, sisi tukikua kiakili na kiteknolojia, sisi tunashindwaje kutunza bandari tuje kurithisha wanetu?

Naunga mkono uwekezaji wa bandari ila ufanywe na serikali yenyewe au ishirikishe sekta binafsi ya ndani. Sekta binafsi ikajifunze Kwa waliofanikiwa, kisha ije iendeleze bandari ikishirikiana na serikali!( Kama NMB Bank ilivyo, serikali ina hisa na private sekta nayo ipo).

Kwani ni lini serikali ili tangaziaumma na dunia kwamba bandari inabinafsishwa ili umma utume maombi? DP World walishindanishwa na nani kwenye tenda? DP World walijuaje kwamba bandari Dar es Salaam inabinafsishwa? Wamepatikanaje sasa?

Ndugu mdau wa JF, toa ushauri wako nami nijifunze.
Utaitwa Muhaini Bure!!
 
Kwa ufahamu wangu mdogo, sheria(bila shaka ya manunuzi), inataka utaratibu wa kutangaza tender utumike na kisha wahusika waombe na mchujo ufanyike kwa kuzingqtia vigezo vilivyoweka then mshindi apatikane na atangazwe.

Saaa najiuliza huyu DP WORLD kuna makamouni 8 alishindanishwa na nani na tangazo la tender liliandikwa au kutolewa kwenye gazeti/ chombo gani cha habari?

Tunaomba majibu kutoka kwa wahusika.
Waziri Mbarawa alisema Kuna makampuni 8 yalijitokeza, then Dpw akashinda tenda. Hakusema tenda ilitangazwa lini na wapi, wala hakusema tenda ilfunguliwa lini na wapi.
Kwenye mkataba inaonyesha Dpworld ilpatikana kufuatia ziara ya rais Dubai. (Contradiction)
Tunasikia habari za wabunge wanahabari, wasanii walienda/walipelekwa Dubai. Hawa sio wataalamu wa masuala ya bandari, wala miundombinu, wala masuala ya uwekezaji. Walienda Kwa gharama za nani na kwa nia gani, hilo ni fumbo kama like la gharama za Royal tour.
Inaonyesha kuna makandokando mengi.
 
Dp walipatikanaje????Walijuaje bandari ya DSM inatafutiwa MTU??? Ni maswahili yananisumbua sana akilini .....

Viongozi katika huu mkataba wa Bandari kutakuwa na donge nono la Rushwa kila Mwezi watakuwa wamecheza sio kwa kelele hizi na bado watu wanatiwa ndani kwa sababu ya Kupinga........

Ya pili ni huo uwekezaji wa joint venture.Ili kuifanya Serikali iweze kufanya monitoring ya ndani KABISA kuepuka kuhujumiwa kiuchumi kama unavyosema

Watu wanajificha kwenye kichaka Cha gharama ila wanaogopa kusema Kwani ni Hela inayolipika.
Gharama za uwekezaji bandari ni shilingi ngapi?

Hivi kweli tunaweza kumkodi MTU wa kutukamulia ng'ombe wetu mwenye maziwa mengi eti kwa sababu ng'ombe anarusha mateke sana?
Kwani kumfunga miguu inagharimu nini?

Si mwenye ng'ombe anaita majirani 2 anashirikiana nao kumfunga miguu , Kisha yeye ( mwenye ng'ombe) anaenda kumkamua???

Serikali iwekeze kuendeleza bandari, Mbona Magufuli alirudusha Heshima ya Serikali na hata mianya ya Rushwa yalipungua alituma njia gani kufanya Monitoring? Seriously, Mbaya zaidi aliyeko kwenye hicho kiti ndiyo analiyekuwa kaimu wake.

Kwa nini kila waziri/ wabunge/ Vibaraka WA utawala kama wabunge wote pomoja na machawa kama Kitenge na wezio- walihongwa wanatetea issue ya Bandari kuna nini hapa?
Hili swali ukimuuliz mabarawa na waziri mkuu huwa wanakuwa n majibu tofauto kama vile ni serikal mbili tofauti
 
Hujui sheria inatambua utaratibu wa single source?

Kwani zile shule zilizojengwa nchi nzima zilitangazwa tenda watu waombe?

Mnajitafanya mnajua kupost kumbe mnapost maujinga tu.
expand...Waziri Mbarawa alisema Kuna makampuni 8 yalijitokeza, then Dpw akashinda tenda. Hakusema tenda ilitangazwa lini na wapi, wala hakusema tenda ilfunguliwa lini na wapi.
Kwenye mkataba inaonyesha Dpworld ilpatikana kufuatia ziara ya rais Dubai. (Contradiction)
Tunasikia habari za wabunge wanahabari, wasanii walienda/walipelekwa Dubai. Hawa sio wataalamu wa masuala ya bandari, wala miundombinu, wala masuala ya uwekezaji. Walienda Kwa gharama za nani na kwa nia gani, hilo ni fumbo kama like la gharama za Royal tour.
Inaonyesha kuna makandokando mengi.
 
Dp walipatikanaje????Walijuaje bandari ya DSM inatafutiwa MTU??? Ni maswahili yananisumbua sana akilini .....
Mbarawa: Tulishindanisha kampuni nane toka nchi tofauti
Pm: Mama alipoenda Dubai, akampata Dpw.
🤣🤣🤣🤣🤣
 
expand...Waziri Mbarawa alisema Kuna makampuni 8 yalijitokeza, then Dpw akashinda tenda. Hakusema tenda ilitangazwa lini na wapi, wala hakusema tenda ilfunguliwa lini na wapi.
Kwenye mkataba inaonyesha Dpworld ilpatikana kufuatia ziara ya rais Dubai. (Contradiction)
Tunasikia habari za wabunge wanahabari, wasanii walienda/walipelekwa Dubai. Hawa sio wataalamu wa masuala ya bandari, wala miundombinu, wala masuala ya uwekezaji. Walienda Kwa gharama za nani na kwa nia gani, hilo ni fumbo kama like la gharama za Royal tour.
Inaonyesha kuna makandokando mengi.
Kama wamefanya utaratibu wa single source ambao unaruhusiwa kisheria shida iko wapi?
 
Back
Top Bottom