Hamna chochote cha kufurahia hapo, hiyo ni michezo ya Samia kutaka kuhalalisha kwamba mwarabu alipewa bandari baada ya taratibu zote kufuatwa.
Mwanzo walilazimisha kubadili sheria ili iwanufaishe waarabu, wakaona mambo magumu, bunge likagoma na serikali ikakubali yaishe.
Sasa wamekuja na hii mbinu ya kutanganza tender, kwasababu wengi walilalamika mwarabu amepewa bila kushindanishwa, hapo wanamtengenezea mazingira mwarabu ashinde ili wapate uhalali wa kumpa bandari.
Lakini pia, hata ukisoma objectives za IGA, mwarabu amepewa aendeshe bandari zote Tanganyika, tena kwa muda usiojulikana, hivyo hata kama hiyo terminal 2 akiendesha mwingine, itakuwa ni kwa muda tu, kwasababu hiyo terminal 2 bado ipo ndani ya bandari ya Dsm ambayo mwarabu ameshakabidhiwa milele, msidanganyike.
Serikali ya Samia inatakiwa kuvunja ule mkataba wa hovyo wa IGA walioingia na mwarabu, wasitudanganye kwa hii michezo ya kitoto wanayocheza, ni utapeli mtupu.