DP World wameachia Bandari? TPA yatangaza kutafuta Mzabuni kuhudumia Makasha katika Terminal II

DP World wameachia Bandari? TPA yatangaza kutafuta Mzabuni kuhudumia Makasha katika Terminal II

Terms ziko wazi nenda kasome ! DPW wanajulishwa na tenda inatangazwa na wao ndio wanahamua nani awe mwekezaji na kwa aina hii ya tenda ni wazi kuwa DPW wanaweza kushinda kupitia wao direct au kampuni yao ili kuendelea na kiini macho ..kama umesoma IGA uwezi shangaa TPA kutangaza tenda lakini kwa ile IGA hii ni kiini macho 😎😎😎😎
Tumetia sana chumvi huu mkataba wa serikali na DP World. Upotoshaji ni mwingi sana lakini tatizo haswa ni elimu zetu za masuala ya mikataba kuwa duni.

IGA ya DPW inajitegemea haihusiani na IGA itakayokuwa mpya kati ya muendeshaji mpya ya magati namba 8-11. Haitahusiana na muendeshaji wa bandari ya Mbamba Bay kule Ziwa Nyasa na pia itakuwa tofauti na kule Ziwa Tanganyika.

Hili suala la DP World limetuumbua uwezo wetu wa elimu kitaifa, kuanzia maprofesa kina Shivji na Lipumba mpaka wanafunzi wa vyuo vikuu mwaka wa kwanza.
 
Wewe una akili ndogo unatakiwa kujua kulingana na ile IGA DPW ndio wenye mamlaka ya bandari yote na Tanzania wakitaka kufanya lolote watawajuza kwa hiyo kwakifupi DPW wamepewa taarifa na wameruhusu kutangazwa kwa tenda na sitoshangaa na wao wakawa wahusika wa kuomba hiyo tenda na kushinda!

Tunajua serikali inajaribu kujitekenya halafu baadae icheke😂😂😂😂
Waliokupotosha wanastahili malipo makubwa sana, kazi yao wameifanya vizuri sana, na kibaya zaidi kama wewe mmejaa huko mitaani mnafanya kazi ya kusambaza huo upotoshwaji mliopotoshwa nyinyi.

IGA ya DP World inajitegemea yenyewe, sawa sawa na IGA za waendelezaj wengine wanaotafutwa muda huu na TPA.

Hapo pia kuna wazalendo wenye uwezo wameombwa kupeleka maombi yao ya kazi bandarini, na wao IGA yao itakuwa tofauti kulingana na mikataba watakayoisaini kwa ajili ya kufanya kazi.
 
Kwanini isiaminike iwapo unalala unaamka na kufanya shughuli zako chini ya ulinzi wa JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA na majeshi yake?
Ulinzi ni wa Mungu. Tunalala na kuamka kwa neema ya Mungu pekee yake. Acha kumkufuru Mungu.
 
Ulinzi ni wa Mungu. Tunalala na kuamka kwa neema ya Mungu pekee yake. Acha kumkufuru Mungu.
Acha mbwembwe na vitisho vya kijinga. Kwamba hii nchi jeshi halina nafasi kwenye ulinzi wa nchi? Embu nenda mipakani huko ujionee kazi za jeshi la nchi yako.

Kama wewe ni mlokole Umewahi wasikia wana wa Israeli? Walipewa nchi ya ahadi na MUNGU kupitia jeshi au walikaa MUNGU akaenda kupigana? Mnazitumia imani vibaya mnakuwa mazombi mpaka mnazalisha wasioamini uwepo wa MUNGU.
 
Profesa Assad alisema kwamba afrika inao upungufu wa nguvu kazi yenye elimu, huyo ni CAG mstaafu ambaye lazima ni mtu wa TISS pia.

Na yeye aliongea akiwa anafurahia uwezo wetu wa kuendesha bandari kuwa mdogo?, ukweli siku zote unaposemwa huwa ni tiba kwa yule anayeusikia ndio maana ya msemo usemao ukweli unauma.
Suluhisho la kuwa na uwezo mdogo wa kuendesha bandari ni nini? Ni kuendelea kufurahi?
 
Chenga ya mwili hiyo.... Watakuja kwa mlango wa uwani.....
 
Dp world tayari ni janga hawawezi kuachia kwasbb viongozi washakula kichwa kichwa, sasa itawabidi wa balance mambo na matakwa ya wananchi pamoja na dp world, hivyo watajadili wagawe vipande kama watatokea wawekezaji wengine.

Ila sasa wasije wakasema dp world kashinda tender zote ?!
 
Mengi hatuyajui tena yale ya kitaalam. DPW anatarajia kuja na ufanisi wa mapato ya trilioni 28 kwa mwaka pesa atakayokusanya TRA, sidhani kama tunanyonywa na hawa waarabu.

Kwasasa ni 7T hiyo 28 mnaitoa wapi? kati ya hiyo 28 Serikali nachukua ngapi na DPW ngapi?
 
Back
Top Bottom