DP World wawepo Uingereza kwa wanaojitambua halafu Waswahili wa Tanzania tuikatae?

Kichwa kikubwa ubongo wa sisimizi
 
Rwanda mna bandari we mkimbizi
 
umewaambia ukweli
 
We endelea na hizi mbanga, tutakuvua cheo cha upopoma with immediate effect😆
 
Issue sio kutowataka DP acha kuchanganya mambo...watu wanahoji namna mkataba ulivyo na mashariti yake ikiwemo duration sawa?....wewe umeuona mkataba wa DP na UK?....
Punguza mdomo....fuatilia mambo kabla ya kukurupuka
 


Shida sio asipewe au apewe bandari bali shida ni namna mkataba ulivyoingiwa mazingira yake na baadhi ya vipengele vyake, mfano mkataba unasema bandari ZOTE za nchi hii apewe lakini bandari za Zanzibar tu hazihusiki, muda wa mkataba sio specified na inapotokea dispute usuluhishi ufanywe kwa sheria za kimataifa wakati Tz ni nchi na Dubai sio nchi nk, kifupi mkataba umekuwa ni siri mno na wa harakaharaka mno kiasi kwamba unatia mashaka, na mikataba ya aina hiyo imekuwepo nchini mwetu ambapo mwisho wa siku ni sisi "tuliopigwa" refer; TICKS, NET group solution nk. Wasiwasi baada ya kung'atwa na nyoka ndio akili, katika jambo hili la Bandari zetu nina wasiwasi mkubwa sana kwamba Madam president kaingizwa chaka na watendaji wake, maskini hajui hatari ya huo mkataba, wewe kwanini huoni kateua washauri wapya hivi karibuni ?!!.

Ingekuwa vizuri utuletee hapa huo mkataba kati ya DP world na Uingereza (nchi inayojitambua) ili tuuone ukoje na tupate kujifunza.
 
Tatizo MKATABA....
 
Dpw hawawezi kuiharibu UK kwa kuwa si mbumbumbu, na mifumo (sheria)yao inajisimamia. Mkataba wetu unaona dhahiri, dpw wanatoa maagizo, sisi hatuonekani hata kutoa maagizo kwao.
Toka lini muuzaji akatoa maagizo kwa mnunuzi ? Ulisikia wapi ?
 
Acha UJINGA terms and conditions za UK na TZ unazijua?😡😡😡
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…