DPP awafutia Tundu Lissu na Wahariri wa Gazeti la Mawio kesi ya Uchochezi

DPP awafutia Tundu Lissu na Wahariri wa Gazeti la Mawio kesi ya Uchochezi

1632307496739.jpeg


Criminal Case No.208/2016 iliyokuwa ikimkabili Tundu Lissu na wenzake watatu katika Mahakama ya Kisutu, imefutwa na DPP kwa mujibu wa Kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo ya Makosa ya Jinai. Watuhumiwa wote wako huru.

Mbali na Lissu washtakiwa wengine walikuwa ni Mhariri wa Gazeti la Mawio, Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh

Washtakiwa hao kwa pamoja Walikuwa wanakabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na sheria ya magazeti ya mwaka 2002.

Patrick Mwita wakili wa serikali mbele Thomas Simba Hakimu Mkazi Mkuu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alisoma shitaka la kwanza na tano.

Mwita alidai kuwa shitaka la kwanza ni la kupanga njama za kutoa chapisho la uchochezi, kosa linalodaiwa kutendwa kati ya tarehe 12 na 14 Januari mwaka 2016 ambapo;

Idrissa, Mkina na Lissu katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam walipanga njama za kuchapisha taarifa za uchochezi.

Katika kosa la tano, mshitakiwa namba moja (Idrissa), namba mbili (Mkina) na namba nne (Lissu), wanatuhumiwa kuchochea hofu miongoni mwa wananchi kwa kuchapisha habari “Machafuko yaja Zanzibar” na kwamba, ingeweza kuzua vita au umwagaji damu.

Shitaka pili likimkabili Jabir, Mkina na Lissu, wakidaiwa kuchapisha chapisho la uchochezi katika Gazeti la MAWIO, toleo Na. 182 la tarehe 14-20 Januari 2016.

Shitaka la tatu linamuhusu Ismail akidaiwa kuchapisha chapisho la uchochezi katika gazeti hilo lenye kichwa cha Habari ‘Machafuko yaja Z’bar’.

Shitaka la nne linamkabili Ismail akidaiwa kuchapisha gazeti bila kupeleka kiapo kwa Msajili wa Magazeti.
 
mtu ukiwa na makesi kama lissu lazima ujitafakari kuwa una shida sehemu haiwezekani usingiziwe wewe tu au uonewe wewe tu lissu angekuwa mtulivu ni kiongozi mzuri lakini atashangaa taaluma yake na uwezo wake kiuongozi hautumii anabaki kushindana na makesi kila siku
Jua hili. It is very dangerous when you are right and the Government is wrong
 
mtu ukiwa na makesi kama lissu lazima ujitafakari kuwa una shida sehemu haiwezekani usingiziwe wewe tu au uonewe wewe tu lissu angekuwa mtulivu ni kiongozi mzuri lakini atashangaa taaluma yake na uwezo wake kiuongozi hautumii anabaki kushindana na makesi kila siku

Kasome histori ya Rais wa sasa wa Zambia,
Alikuwa na Kesi lisu cha mtoto na hata kukaa jela
 
Baada ya kutusumbua kwa miaka 5 kwa kesi ya uongo ya uchochezi, DPP ameifuta kesi hiyo. Lakini bado kuna kesi nyingine 5 za uongo dhidi yangu & mamia nyingine dhidi ya viongozi, wanachama & Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe. Zote hizo zinatakiwa kufutwa bila masharti yoyote- Tundu Lissu

After five years of purposelessly persecuting me & four journalists with baseless sedition charges, Tanzania's DPP has dropped the case. Five more equally frivolous cases remain & hundreds more still face our members, including Chairman Mbowe. It's past time they're all withdrawn- Tundu Lissu


View attachment 1948307
Huyu ndo mh lissu ninaemfaham
Hamungunyi maneno , anasema kilee jamii wanakijua na kwa wepesi sana
 
mtu ukiwa na makesi kama lissu lazima ujitafakari kuwa una shida sehemu haiwezekani usingiziwe wewe tu au uonewe wewe tu lissu angekuwa mtulivu ni kiongozi mzuri lakini atashangaa taaluma yake na uwezo wake kiuongozi hautumii anabaki kushindana na makesi kila siku
Nakushauri uende Zambia,ukawaambie wazambia,kwanini wamekubali HH apewe urais badala ya Edgar Lungu,kwani HH alikua na utitiri wa makesi meengii.... wakati Lungu hata hakua na makesi,nadhani HH amewahi hadi kufungwa,Lissu nadhani bado hajafungwa,inaonesha kesi zake ni za kubumba.
 
Criminal Case No.208/2016 iliyokuwa ikimkabili Tundu Lissu na wenzake watatu katika Mahakama ya Kisutu, imefutwa na DPP kwa mujibu wa Kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo ya Makosa ya Jinai. Watuhumiwa wote wako huru...
Kuanzisha kesi kama hizi kunasaidia nini? Maana zinafutwa juu kwa juu 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂
 
Mtu ukiwa na makesi kama Lissu lazima ujitafakari kuwa una shida sehemu haiwezekani usingiziwe wewe tu au uonewe wewe tu Lissu angekuwa mtulivu ni kiongozi mzuri lakini atashangaa taaluma yake na uwezo wake kiuongozi hautumii anabaki kushindana na makesi kila siku
Na jama huna kesi pia ujitafakari huna impact yeyote kwa jamii
 
Labda ili kuiepusha serikali yake na aibu inayoendelea mahakamani!

Vinginevyo, sio kazi ya Samia.
Wanasiasa aina ya Samia huwa hawana na hawaogopi aibu, sababu wanajiamini! JPM alikuwa hana confidence, aliuficha udhaifu huo kwa kuwa na ubabe wa kibwege! So wanaodhani yanayoendelea Mahakamani yanamnyima Samia usingizi wanajidanganya sana
 
Back
Top Bottom