DPW Special Thread: Uzi maalumu kuhusu kampuni ya DP World

DPW Special Thread: Uzi maalumu kuhusu kampuni ya DP World

SOMENI COMMENT HII
👇🏽
Hili siyo swala la muarabu peke yake bali ni dili kubwa la viongozi waandamizi wa ccm la kutuuza sisi kwa manufaa ya vizazi vyao, fikiria mbuga za Loliondo na Ngorongoro wanazimiliki kwa mikataba ya siri na wenyeji wote wamehamishiwa Msomera na maeneo mengine, nani alitoa pesa za kuwajengea nyumba, usafiri wao na mifugo yao zimetoka kwenye bajeti gani? Nani aligharimia upimaji wa ardhi kule Msomera na gharama za kutoa hati miliki, leo maeneo ya Loliondo na Ngorongoro ukiingia simu yako inakukaribisha kwenye himaya ya Falme za kiarabu. Sakata la bandari ni zaidi ya tunavyoliona kwa sababu tayari waarabu wapo bandarini tangu mwaka jana hata kabla TICTS hajaondoka ndiyo maana mkataba wa IGA unalazimisha kutambuliwa kwa shughuli zilizofanyika kabla ya kusainiwa kwa IGA, kimsingi wanaposema DP World and affiliates wanamaanisha kuwa kutakuwa na makampuni mengi toka Dubai yatafanya shughuli mbalimbali na yatasajiliwa hapa Tanganyika yakiwa na local content ya wanahisa vigogo wa ccm na jamaa zao hasa wanaopiga debe kuelezea mafanikio bila kujibu hoja ya matatizo ya IGA wakijua kuwa watoto wao, wajukuu na vitukuu watamiliki Tanganyika milele.

Kwa muktadha huo sisi wazalendo wana wa Tanganyika tupambane kufa na kupona kuokoa rasilimali zetu zikiwemo, bandari zetu za bahari, maziwa na6mito, miundombinu yetu, mipaka yetu, viwanja vya ndege, (logistic infrastructures collectively) maeneo maalumu ya uwekezaji (special economic zones), hata mapato yetu kwa sababu mkataba unatulazimisha kutoa misamaha ya kodi wakati tuna mkopo wa trillion moja toka worlBank.

Ndugu zangu inatia uchungu kuona viongozi waliojitwalia madaraka kwa kuvunja Katiba wanaendelea kuvunja Katiba hata katika maeneo mengine bila woga wakisaidiwa na Bunge haramu.

Hakuna jambo linafanyika kwa bahati mbaya, kila tukio limepangwa kwa ustadi wa vipofu na tukilegea kwenye haya mambo wataendelea kurithishana utawala wa nchi hii na huku wakilindwa na TISS waliopewa ulinzi kisheria kwa kinga yenye malengo mabaya kwenye jamii ya wastaarabu.

MUNGU IBARIKI TANGANYIKA, MUNGU IBARIKI AFRIKA - UMUKHONTHOOO, WESIZWEEEE
 
Inashangaza sana ila ndio ukweli kwa sasa.

Nyuzi nyingi zimeanzishwa kuhusu DP World, kuna wanaounga mkono na kuna wanaopinga.

Cha ajabu nimechunguza sana na kuona kuwa asilimia kubwa ya wanaopinga au kuanzisha uzi za kupinga ni new member JF, kwanini?
 
Inashangaza sana ila ndio ukweli kwa sasa

Nyuzi nyingi zimeanzishwa kuhusu dp world, kuna wanaounga mkono na kuna wanaopinga,
Cha ajabu nimechunguza sana na kuona kuwa asilimia kubwa ya wanaopinga au kuanzisha uzi za kupinga ni new member jf, kwanini?
Una uhakika ?
 
Inashangaza sana ila ndio ukweli kwa sasa

Nyuzi nyingi zimeanzishwa kuhusu dp world, kuna wanaounga mkono na kuna wanaopinga,
Cha ajabu nimechunguza sana na kuona kuwa asilimia kubwa ya wanaopinga au kuanzisha uzi za kupinga ni new member jf, kwanini?
Kwani wew upo upande gani., maana hii ni kama debate
 
Unataka kutuaminisha kwamba Mama ni mwaminifu hachepuki ??
 
Nasapoti,
na kama kuna marekebisho yafanywe
Ila kupinga kibugusa hapana
Halafu mkuu kwa nini mpaka bandari za maziwa makuu nazo ziwemo., au ndiyo yale ya kipindi kile bandari ya bagamoyo kusiwepo na bandari pinzani kwa miaka ....., TRA asikusanye Maputo kwa miaka ...., maana swala la mikataba ni sensitive sana sema tu watawala hawana umakini.
 
Halafu mkuu kwa nini mpaka bandari za maziwa makuu nazo ziwemo., au ndiyo yale ya kipindi kile bandari ya bagamoyo kusiwepo na bandari pinzani kwa miaka ....., TRA asikusanye Maputo kwa miaka ...., maana swala la mikataba ni sensitive sana sema tu watawala hawana umakini.
Zote ni mali ya tanzania, kama kuna maslahi sawa, kama marekebisho yafanywe, kama hakuna maslahi, no
 
Back
Top Bottom