Dr. Bashiru, If you are a man of Principles, Hata Wakushukie vipi Stand Firm!, Don't Apologize!, Utaheshimika Zaidi na Zaidi!

Hana lolote ameshiriki kuua watu 2020 na kuwafunga acha ashughulikiwe ikibidi hata wamuue kabisa ni msaliti mkubwa hafai
 
Paschal, Bashiru, Polepole, Kabudi, Mkumbo na wengine wasaka tonge usiwaamini hata kwa dak 1
 
Its a good advice but...... nachokiona mimi ni kuwa yupo nje ya Team ndio maana ya yote haya ila na yeye alipokuwa kwenye awamu iliyopita alishiriki kwenye ''praise team'' na hakukosolewa. Aliendesha/kuratibu magenge ya hatari na nguvu ya dola kuwatesa sana wapinzani wa utawala ule. Anapaswa kusoma alama za nyakati, he should not play hero.
 
Shida ya DR. Bashiru ni kuyakana maneno yake mwenyewe. ivi kuna kipindi mtawala alisifiwa kama kipindi cha magufuli na yeye akiwa katibu mkuu? raisi yule alifikia kusema akifa sijui hiki atajenga nani na ujinga mwingi tu.... yote yalifanyika Bashiru akiwa katibu mkuu. leo inakuwa nongwa kusema mama anaupiga mwingi ambayo kimsingi siyo kauli ya serikali ........ tuache unafiki, bashiru huyu alinajisi ofisi kwa kununua wabunge ati wanaunga mkono juhudi? kisha wanarudishwa kwenye majimbo yaleyale tena kwa gharama za kodi zetu
 
Sitegemei Bashiru afanye huo ujinga alioufanya Ndugai, kama akifanya hivyo atakuwa mtu wa ajabu zaidi asiyejifunza kwa lolote, hizi kelele kwa namna moja au nyingine naamini lazima alizi anticipate hivyo sioni kama zitamsumbua kwa vyovyote.
Mwanasiasa awe na msimamo?
 
It's you Pascal Mayalla again!

Kilichochangia huyu Bashiru ashukiwe kama mwewe ni baadhi ya matendo na matamshi yake wakati mkono wake ulipokuwa unachovya kwenye buyu la asali enzi za utawala wa jiwe. Hiyo "Moral Authority" anaitowa wapi wakati alifanya ya hovyo enzi za utawala wa jiwe? Angeyasema haya enzi zile akiwa pale Mlimani usingesikia kelele zote hizi.
 
Majizi ndio yaliyomjia juu.
kwa hoja ndogo kama hii wanachanganyikiwa basi chama kipo hatua za mwishoni katika enzi
 
Hawezi Rudi kuomba radhi.

Ana backup ya watu wazito, CCM halisi. Warithi wa Babu.

Tulikuwa na kiapo chetu Cha TANU, " Nitasema KWELI daima, FITINA kwangu MWIKO".
 
Pascal pascal ukirudi kwenye ubora wako.
Bill ya wine kila wekend count on me bablai.

Nimekupenda tena🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…