Dr. Bashiru: Wale wote waliomtukana Rais Magufuli bado wana mashtaka ya kujibu mbele ya CCM, msamaha waliopata ni wa Dr Magufuli siyo CCM

Dr. Bashiru: Wale wote waliomtukana Rais Magufuli bado wana mashtaka ya kujibu mbele ya CCM, msamaha waliopata ni wa Dr Magufuli siyo CCM

Dr Bashiru achana na issues hizo, ili mradi Mwenyekiti CCM kasamehe na ni boss wetu sote, na ww Katibu Mkuu waache wenzako hakuna asiyekosea, hii itaonyesha kuwa msamaha walioupata kwa Mh. Rais hauna maana. Plse tunakuomba msamaha ulitoka, basi acha kuwafunga kamba shingo tena waliokosea na wamepata msamaha.
 
Kiranga,
Reverend Jesse Jackson alikuwa Mmarekani Mwafrika aliyekuwa anaheshimika sana miongoni mwa Wamarekani Waafrika wenzake, chama chake cha Democratic pamoja na Amerika kwa ujumla. Baada ya Obama kuteuliwa kuwa Rais wa Marekani, aliwahi kuhojiwa na kituo kimoja cha habari na kumsifia sana Barack Obama. Baada ya mahojiano na akijua yuko " off air" kumbe mike iliyokuwa kwenye koti ilikuwa bado "on air" akaanza kumsema vibaya Obama huku anasikika America nzima!
Ulizia sasa hivi heshima yake ikoje miongoni mwa Waamefrika Waafrika, ndani ya chake na Amerika kwa ujumla.
 
Matusi ni nini? Kipi ni tusi na kipi ni ukweli tu ambao rais hataupenda?

Unajuaje nikisema "John Magufuli ni mshamba wa kutupwa" hilo ni tusi la kumvunjia heshima mkuu wa nchi na ni haki nifungwe jela au ni ukweli ambao ni haki yangu ya kikatiba kuueleza?

Kati ya serikali na mwananchi, nani ana mzigo wa kuonesha hili ni tusi na hii ni haki ya kikatiba ya kujieleza tu?
Na mimi ninasema ''wewe ni mshamba wa kutupwa'' kwa sababu hujui tusi ni lipi!

Backwoodsman!
 
Katibu mkuu wa CCM, Dr Bashiru Ally amesema wale wote waliomtukana Mwenyekiti wa CCM, Dr. Magufuli bado wana kesi ya kujibu mbele ya kamati ya nidhamu ya chama.

Dr. Bashiru amesema wale walioomba msamaha na kusamehewa walifanya hivyo kama watu binafsi na Dr. Magufuli aliwasamehe kama mzazi lakini kwenye chama mashtaka yao yapo palepale na muda ukifika wataitwa kujieleza na kuchukuliwa hatua " rasmi" kwa namna itakavyoonekana inafaa kwa mujibu wa katiba ya chama.

Chanzo: ITV habari!
Kwani si wamesamehewa na mwenyekiti wa chama. Huyu katibu amekurupuka. Mzigo uko kwa mwenyekiti kuthibitisha kama ni kweli hayo anayoyasema katibu wake.

Je katibu mkuu wa ccm ametumia vigezo gani kufikia hiyo conclusion? Mwenyekiti wake alitakiwa atoe msamaha kwa namna gani ambayo siyo kinyume na taratibu za chama?
 
Reverend Jesse Jackson alikuwa Mmarekani Mwafrika aliyekuwa anaheshimika sana miongoni mwa Wamarekani Waafrika wenzake, chama chake cha Democratic pamoja na Amerika kwa ujumla. Baada ya Obama kuteuliwa kuwa Rais wa Marekani, aliwahi kuhojiwa na kituo kimoja cha habari na kumsifia sana Barack Obama. Baada ya mahojiano na akijua yuko " off air" kumbe mike iliyokuwa kwenye koti ilikuwa bado "on air" akaanza kumsema vibaya Obama huku anasikika America nzima!
Ulizia sasa hivi heshima yake ikoje miongoni mwa Waamefrika Waafrika, ndani ya chake na Amerika kwa ujumla.
Kama heshima ya Rev. Jackson imeshuka, si kwa sababu ya kumsema vibaya Obama.

Nimeishi Marekani kipindi chote cha urais wa Obama, na hata kabla yacho.

Kuna watu waliheshimika sana katika jamii ya watu weusi Marekani.

Namumbuka Cornel West, mhadhiri Profesa mweusi aliyefundisha Ivy League, Princeton University. Na mwingine Travis Smiley, muendesha kipindi wa televisheni ya jamii PBS.

Wawili hawa walimshambulia Rais Obama sana kwa namna ambayo mwanzo sikuielewa wala kuitarajia.

Kwa sababu walikiwa ni weusi na wana watu wengi wanawafuatilia, mmoja akitoka academia, muandiahi wa vitabu vingi ambavyo nilikwishasoma na kujua msimamo wake (Cornel West) na mwingine mtangazaji wa TV ambaye karibu kila wiki nilikuwa namtizama, wote walitaka maendeleo kwa watu weusi na masikini.

Wote walitaka mtu kama Obama awe rais.

Nikashangaa sana, imekuwaje Obama kawa rais, halafu wanamswma vibaya badala ya kumuunga mkono?

Nikagundua kitu.

Marekani hata watu wanaokuunga mkono wanaweza kukushambulia.

Ni kwa mujibu wa kanuni ya rais Frank Delano Roosevelt ya "Go and Make Me Do It".

Rais Roosevelt alifuatwa na jamaa mmoja mtu wa vyama vya wafabyakazi. Jamaa alikuwa na malalamimo kibao. Akamlalamikia sana rais Roosevelt, akimtaka rais awafanyie hili na lile.

Rais akamwambia, malalamiko yako nimeyasikia. Ila, sitayafanyia kazi.

Ili niyafanyie kazi, nakutaka uende tena uraiani huko, unipigie kelele, unitake niyafanyie kazi, Marekani nzima iyajue malalamiko yako, ukiyapigia kelele hivyo, yakijulikana, nayafanyia kazi.

Alimwambia "Go and make me do it".

Marekani hatupendi hagiography. Mtu anaweza kumsema vibaya Obama kwamba hajafanya hiki na lile, si kwa sababu hamoendi Obama. Hasha.

Bali kwa sababu anampenda sana Obama na anatamani Obama angefanya zaidi, pakubwa kupita alipofanya.

obama-family-thanksgiving.jpeg
 
Kwani si wamesamehewa na mwenyekiti wa chama. Huyu katibu amekurupuka. Mzigo uko kwa mwenyekiti kuthibitisha kama ni kweli hayo anayoyasema katibu wake.

Je katibu mkuu wa ccm ametumia vigezo gani kufikia hiyo conclusion? Mwenyekiti wake alitakiwa atoe msamaha kwa namna gani ambayo siyo kinyume na taratibu za chama?
Amesema Mwenyekiti alisamehe kama mzazi!
 
Bashiru Ally ndio maana huelewani na Pole pole kwa kujifanya mbabe uchwara hao unaotaka kuwa block uwe makini nao ndio ma mafia wa ccm michezo ya hatari yote wanaijua haswa huyo Nape ni mtoto wa mjini takecare.
 
Vendetta za kishamba tu. Viongozi wanapaswa kuwa thick skinned, wanaongoza watu wengi na hawawezi kuwafurahisha wote. Nilisikiliza hizo voice notes or whatever they are, hazina matusi na mbaya zaidi hazikupatikana kwa njia halali. Common sense tu, hauwezi kuvamia faragha ya mtu,ukadukua maongezi yake kinyume cha sheria halafu eti ukasema amekutukana na unapanga kumwadhibu! Hizi akili za wapi?
 
Back
Top Bottom