Dr. Bashiru: Wale wote waliomtukana Rais Magufuli bado wana mashtaka ya kujibu mbele ya CCM, msamaha waliopata ni wa Dr Magufuli siyo CCM

Kama heshima ya Rev. Jackson imeshuka, si kwa sababu ya kumsema vibaya Obama.

Nimeishi Marekani kipindi chote cha urais wa Obama, na hata kabla yacho.

Kuna watu waliheshimika sana katika jamii ya watu weusi Marekani.

Namumbuka Cornel West, mhadhiri Profesa mweusi aliyefundisha Ivy League, Princeton University. Na mwingine Travis Smiley, muendesha kipindi wa televisheni ya jamii PBS.

Wawili hawa walimshambulia Rais Obama sana kwa namna ambayo mwanzo sikuielewa wala kuitarajia.

Kwa sababu walikiwa ni weusi na wana watu wengi wanawafuatilia, mmoja akitoka academia, muandiahi wa vitabu vingi ambavyo nilikwishasoma na kujua msimamo wake (Cornel West) na mwingine mtangazaji wa TV ambaye karibu kila wiki nilikuwa namtizama, wote walitaka maendeleo kwa watu weusi na masikini.

Wote walitaka mtu kama Obama awe rais.

Nikashangaa sana, imekuwaje Obama kawa rais, halafu wanamswma vibaya badala ya kumuunga mkono?

Nikagundua kitu.

Marekani hata watu wanaokuunga mkono wanaweza kukushambulia.

Ni kwa mujibu wa kanuni ya rais Frank Delano Roosevelt ya "Go and Make Me Do It".

Rais Roosevelt alifuatwa na jamaa mmoja mtu wa vyama vya wafabyakazi. Jamaa alikuwa na malalamimo kibao. Akamlalamikia sana rais Roosevelt, akimtaka rais awafanyie hili na lile.

Rais akamwambia, malalamiko yako nimeyasikia. Ila, sitayafanyia kazi.

Ili niyafanyie kazi, nakutaka uende tena uraiani huko, unipigie kelele, unitake niyafanyie kazi, Marekani nzima iyajue malalamiko yako, ukiyapigia kelele hivyo, yakijulikana, nayafanyia kazi.

Alimwambia "Go and make me do it".

Marekani hatupendi hagiography. Mtu anaweza kumsema vibaya Obama kwamba hajafanya hiki na lile, si kwa sababu hamoendi Obama. Hasha.

Bali kwa sababu anampenda sana Obama na anatamani Obama angefanya zaidi, pakubwa kupita alipofanya.

View attachment 1274876
Kwanza ahsante kwa ufafanuzi wako. Pili, context ya uliowataja na content ya Reverend Jesse Jackson ni tofauti. Hawa walifanya openly as American democracy wants. Na ni sahihi kabisa. Reverend yeye alikuwa ana m back bite Obama. Na hii ndio hoja inayowakumba aliowasema Dk. Bashiru.
 
Vendetta za kishamba tu. Viongozi wanapaswa kuwa thick skinned, wanaongoza watu wengi na hawawezi kuwafurahisha wote. Nilisikiliza hizo voice notes or whatever they are, hazina matusi na mbaya zaidi hazikupatikana kwa njia halali. Common sense tu, hauwezi kuvamia faragha ya mtu,ukadukua maongezi yake kinyume cha sheria halafu eti ukasema amekutukana na unapanga kumwadhibu! Hizi akili za wapi?
Ndo wasomi wetu Hawa,Bora niliishia la Saba,ningemaliza hela bure kulipa karo
 
Kwanza ahsante kwa ufafanuzi wako. Pili, context ya uliowataja na content ya Reverend Jesse Jackson ni tofauti. Hawa walifanya openly as American democracy wants. Na ni sahihi kabisa. Reverend yeye alikuwa ana m back bite Obama. Na hii ndio hoja inayowakumba aliowasema Dk. Bashiru.
Context yako ya Rev Jackson na hao aliowasema Bashiru ni tofauti.

Rev. Jackson alifanya makosa mwenyewe kuongea kwenye open mic.

Hao anaowasema Dr. Bashiru wamedukuliwa.

Unaelewa kwamba hata mahakamani ushahidi unaopatikana kwa mtu kudukuliwa bila court order haukubaliki? Unaelewa kama hawa watu wanafunguliwa mashtaka, huo ushahidi utatupwa kama inadmissible kwa sababu umepatikana kinyume na sheria?

CCM inataka kitumia ushahidi uliopatikana kinyume cha sheria, usio na chain of custody wala forensic veracity?

Unaelewa kwamba kama kuna malalamiko hapa yanatakiwa kuwa ni ya hao waliodukuliwa na kuvunjiwa haki zao za msingi za kikatiba?

Unaelewa katiba ya Tanzania inakataza mtu kudukuliwa bila court order and specific procedure?

Unaelewa Dr. Bashiru kushupalia hili ni kushupalia jambo lililoanzia kwenye uvunjwaji wa sheria?

Unaelewa Dr. Bashiru kushupalia hili baada ya rais kutoa msamaha ni kudharau msamaha wa rais?

Unaelewa Dr. Bashiru kushupalia hili ni kubariki udukuaji na kuchochea uendelee?

Unaelewa kufanya hivyo ni kinyume na utawala bora na uongozi wa kufuata sheria?
 
Context yako ya Rev Jackson na hao aliowasema Bashiru ni tofauti.

Rev. Jackson alifanya makosa mwenyewe kuongea kwenye open mic.

Hao anaowasema Dr. Bashiru wanedukuliwa.

Unaelewa kwamba hata mahakamani ushahidi unaopatikana kwa mtu kudukuliwa bila court order haukubaliki? Unaelewa kama hawa watu wanafunguliwa mashtaka, huo ushahidi utatupwa kama inadmissibke kwa sababu umepatikana kinyume na sheria?

CCM inataka kitumia ushahidi uliopatikana kinyume cha sheria, usio na chainnif custody wala forensic veracity?

Unaelewa kwamba kama kuna malalamiko hapa yanatakiwa kuwa ni ya hao waliodukuliwa na kuvunjiwa haki zao za msingi za kikatiba?

Unaelewa katiba ya Tanzania inakataza mtu kudukuliwa bila court order and specific procedure?

Unaelewa Dr. Bashiru kushupalia hili ni kushupalia jambo lililoanzia kwenye uvunjwaji wa sheria?

Unaelewa Dr. Bashiru kushupalia hili baada ya rais kutoa msamaha ni kudharau msamaha wa rais?

Unaelewa Dr. Bashiru kushupalia hili ni kubariki udukuaji na kuchochea uendelee?

Unaelewa kufanya hivyo ni kinyume na utawala bora na uongozi wa kufuata sheria?
Saed Kubenea na Anthony Komu nao waliitwa kwenye Kamati Kuu ya Chadema na taarifa za kudukuliwa. Ilikuwa sahihi? Kama haikuwa sahihi, walishtaki wapi? Mbona mwisho wa siku wao ndio walioomba msamaha? Au unataka kunithibitishia kuwa hawa wawili ni naïve katika kutambua na kutetea haki zao za msingi ndio maana waliomba msamaha badala ya kuwashtaki?
 
Saed Kubenea na Anthony Komu nao waliitwa kwenye Kamati Kuu ya Chadema na taarifa za kudukuliwa. Ilikuwa sahihi? Kama haikuwa sahihi, walishtaki wapi? Mbona mwisho wa siku wao ndio walioomba msamaha? Au unataka kunithibitishia kuwa hawa wawili ni naïve katika haki zao za msingi ndio maana waliomba msamaha badala ya kiwashtaki?
Tanzania ni nchi inayokwenda kwa misingi ya hewala hewala. Mwenye nguvu mpishe. Si misingi ya haki.

Ndiyo maana wanaodukuliwa badala ya kushtaki na kudai fidia, wao ndio wanaomba msamaha.

Kuanzia CCM kina Makamba na Nape mpaka huko CHADEMA kwa hao kina Kubenea unaowasema.

Tuna tatizo la utamaduni lililovuka tofauti za vyama na elimu.

Ndiyo maana unaona CHADEMA kinajiita Chama Cha Demokrasia na Maendeleo lakini Mbowe anang'ang'ania uenyekiti miaka nenda rudi.

Tatizo letu si vyama, si siasa, tuna tatizo kwenye utamaduni.

Ndiyo maana kina Kubenea na kina Makamba wameomba msamaha, licha ya wao kudukuliwa.

Kihaki, wao ndio walitakiwa kuombwa msamaha na kushtaki watu kwa kudukuliwa.
 
Rais anatakiwa kuwa ni mtu anayeweza kutukanwa sana bila anayetukana kufunguliwa mashtaka.

Yani, katika watu ambao mtu anaweza kuwatukana vibaya sana, bila kufunguliwa mashtaka, wa kwanza kabisa anatakiwa kuwa rais.

Wananchi wengine wote wanatakiwa kuwa na kinga ya kisheria dhidi ya kutukanwa kumpita rais.

Kwa nini?

Kuna msemo mmoja wa Kifaransa, wanasema "Noblesse Oblige". Maana yake ni kwamba, wanaopewa nafasi kubwa za kuongoza jamii, wanawajibika kubeba mzigo mkubwa zaidi".

Msemo huu unatoka katika Biblia. Bwana Yesu (namuongelea kama mwanafalsafa, si Mungu wala Mtume, kwa wale ambao watataka kurukia hili kuonesha namuamini kidini) alitoa mfano wa talanta katika kitabu cha Mathayo 25: 14 - 30.

Kwa kifupi, alisema kwamba, kama kuna watu vijakazi kadhaa, wamepewa mtaji na bwana wao wakafanyie kazi, wengine wamepewa mtaji mkubwa, wengine wamepewa mtaji mdogo, wakimaliza kufanya kazi zao, nani atadaiwa marejesho zaidi?

Aliyepewa mtaji mdogo atadaiwa arejeshe mapato zaidi ya aliyepewa mtaji mkubwa?

La hasha.

Aliyepewa mtaji mkubwa atadaiwa kurejesha mapato makubwa zaidi.

Kupewa uongozi wa nchi ni kupewa mtaji, mtaji mkubwa. Ukipewa mtaji mkubwa, utadaiwa kuleta mapato makubwa zaidi.

Unapogombea uongozi, inabidi ujitafakari. Ujiulize, mimi naweza mikiki ya public life? Nawez akuwa na ngozi ya mamba ya kutotetereka nikitupiwa mawe? Nina kifua cha kukaa na maneno? Kutojibu matusi kwa matusi?

Kama huwezi, usigombee uongozi.

Waswahili wanasema "ukubwa gunia la chawa". Walielewa kwamba ukubwa unamletea mtu matusi na kejeli, kufanya kazi bila kushukuriwa, lawama n.k.

Noblesse Oblige.

Hizi sheria za kukingia viongozi matusi (Lese Majeste), ni sheria za zama za kisultani an kifalme. Enzi za demokrasia, sheria hizi zimepitwa na wakati.

Hizi ni zama za uhuru wa kujieleza, si zama za censorship.

Rais anatakiwa kuwa mtu w amwisho kabisa kulindwa na sheria dhidi ya matusi.

Lese Majeste is not protection of leaders against insults.

No.

Lese Majeste is an insult to freedom of speech.

Hilo linatakiwa lianzie kwenye familia yako,kma wewe ni baba wa familia ruhusu utukanwe na familia yako, na kama bado upo kwa wazazi wako,anza kutukana babako maana wakati mwingine anakuzuia kufanya jambo ambalo unaona ni haki yako kufanya au kushindwa kutimiza mahitaji yako. Hata mungu pamoja na yote yanayotokea ya kupoteza mali na wapendwa wetu inagawa ana uwezo wa kuzuia, lakini tunamsifu na kusema ni mapenzi yake. Huku unalia kwa maumivu.
 
Kwani baba anapigiwa kura kuwa baba?

Unaelewa kwamba rais ni kijakazi wa wananchi kwa namna ambayo baba si kijakazi wa familia?

Mbona unachanganya madawa?
 
Tanzania ni nchi inayokwenda kwa misingi ya hewala hewala. Mwenye nguvu mpishe. Si misingi ya haki.

Ndiyo maana wanaodukuliwa badala ya kushtaki na kudai fidia, wao ndio wanaomba msamaha.

Kuanzia CCM kina Makamba na Nape mpaka huko CHADEMA kwa hao kina Kubenea unaowasema.

Tuna tatizo la utamaduni lililovuka tofauti za vyama na elimu.

Ndiyo maana unaona CHADEMA kinajiita Chama Cha Demokrasia na Maendeleo lakini Mbowe anang'ang'ania uenyekiti miaka nenda rudi.

Tatizo letu si vyama, si siasa, tuna tatizo kwenye utamaduni.

Ndiyo maana kina Kubenea na kina Makamba wameomba msamaha, licha ya wao kudukuliwa.

Kihaki, wao ndio walitakiwa kuombwa msamaha na kushtaki watu kwa kudukuliwa.
Hapo nimekuelewa mkuu.
 
Katibu mkuu wa CCM, Dr Bashiru Ally amesema wale wote waliomtukana Mwenyekiti wa CCM, Dr. Magufuli bado wana kesi ya kujibu mbele ya kamati ya nidhamu ya chama.

Dr. Bashiru amesema wale walioomba msamaha na kusamehewa walifanya hivyo kama watu binafsi na Dr. Magufuli aliwasamehe kama mzazi lakini kwenye chama mashtaka yao yapo palepale na muda ukifika wataitwa kujieleza na kuchukuliwa hatua " rasmi" kwa namna itakavyoonekana inafaa kwa mujibu wa katiba ya chama.

Chanzo: ITV habari!
Ushindi hewa umewapa kibri
 
Vendetta za kishamba tu. Viongozi wanapaswa kuwa thick skinned, wanaongoza watu wengi na hawawezi kuwafurahisha wote. Nilisikiliza hizo voice notes or whatever they are, hazina matusi na mbaya zaidi hazikupatikana kwa njia halali. Common sense tu, hauwezi kuvamia faragha ya mtu,ukadukua maongezi yake kinyume cha sheria halafu eti ukasema amekutukana na unapanga kumwadhibu! Hizi akili za wapi?
Kwanza kwani wale jamaa walisema CCM 'mshamba' au walisema mzee mshamba? Sasa mzee kawasamehe baada ya kujua walisema kweli. Sasa hapo CCM inahusikaje na kadhia hiyo?
 
Ndiyo maana unaona CHADEMA kinajiita Chama Cha Demokrasia na Maendeleo lakini Mbowe anang'ang'ania uenyekiti miaka nenda rudi.
Kama Mbowe anachaguliwa na wanachama pasipo mizengwe tatizo liko wapi, si ndiyo demokrasia hiyo kuwapa uhuru wanaochagua kuchagua wanachokitaka?!
 
Kama heshima ya Rev. Jackson imeshuka, si kwa sababu ya kumsema vibaya Obama.

Nimeishi Marekani kipindi chote cha urais wa Obama, na hata kabla yacho.

Kuna watu waliheshimika sana katika jamii ya watu weusi Marekani.

Namumbuka Cornel West, mhadhiri Profesa mweusi aliyefundisha Ivy League, Princeton University. Na mwingine Travis Smiley, muendesha kipindi wa televisheni ya jamii PBS.

Wawili hawa walimshambulia Rais Obama sana kwa namna ambayo mwanzo sikuielewa wala kuitarajia.

Kwa sababu walikiwa ni weusi na wana watu wengi wanawafuatilia, mmoja akitoka academia, muandiahi wa vitabu vingi ambavyo nilikwishasoma na kujua msimamo wake (Cornel West) na mwingine mtangazaji wa TV ambaye karibu kila wiki nilikuwa namtizama, wote walitaka maendeleo kwa watu weusi na masikini.

Wote walitaka mtu kama Obama awe rais.

Nikashangaa sana, imekuwaje Obama kawa rais, halafu wanamswma vibaya badala ya kumuunga mkono?

Nikagundua kitu.

Marekani hata watu wanaokuunga mkono wanaweza kukushambulia.

Ni kwa mujibu wa kanuni ya rais Frank Delano Roosevelt ya "Go and Make Me Do It".

Rais Roosevelt alifuatwa na jamaa mmoja mtu wa vyama vya wafabyakazi. Jamaa alikuwa na malalamimo kibao. Akamlalamikia sana rais Roosevelt, akimtaka rais awafanyie hili na lile.

Rais akamwambia, malalamiko yako nimeyasikia. Ila, sitayafanyia kazi.

Ili niyafanyie kazi, nakutaka uende tena uraiani huko, unipigie kelele, unitake niyafanyie kazi, Marekani nzima iyajue malalamiko yako, ukiyapigia kelele hivyo, yakijulikana, nayafanyia kazi.

Alimwambia "Go and make me do it".

Marekani hatupendi hagiography. Mtu anaweza kumsema vibaya Obama kwamba hajafanya hiki na lile, si kwa sababu hamoendi Obama. Hasha.

Bali kwa sababu anampenda sana Obama na anatamani Obama angefanya zaidi, pakubwa kupita alipofanya.

View attachment 1274876
Daaah Sasha kawa mrefu na mrembo kweli kweli

Kalikuwa katoto saivi kawa binti mkubwa [emoji2]
 
Rais anatakiwa kuwa ni mtu anayeweza kutukanwa sana bila anayetukana kufunguliwa mashtaka.

Yani, katika watu ambao mtu anaweza kuwatukana vibaya sana, bila kufunguliwa mashtaka, wa kwanza kabisa anatakiwa kuwa rais.

Wananchi wengine wote wanatakiwa kuwa na kinga ya kisheria dhidi ya kutukanwa kumpita rais.

Kwa nini?

Kuna msemo mmoja wa Kifaransa, wanasema "Noblesse Oblige". Maana yake ni kwamba, wanaopewa nafasi kubwa za kuongoza jamii, wanawajibika kubeba mzigo mkubwa zaidi".

Msemo huu unatoka katika Biblia. Bwana Yesu (namuongelea kama mwanafalsafa, si Mungu wala Mtume, kwa wale ambao watataka kurukia hili kuonesha namuamini kidini) alitoa mfano wa talanta katika kitabu cha Mathayo 25: 14 - 30.

Kwa kifupi, alisema kwamba, kama kuna watu vijakazi kadhaa, wamepewa mtaji na bwana wao wakafanyie kazi, wengine wamepewa mtaji mkubwa, wengine wamepewa mtaji mdogo, wakimaliza kufanya kazi zao, nani atadaiwa marejesho zaidi?

Aliyepewa mtaji mdogo atadaiwa arejeshe mapato zaidi ya aliyepewa mtaji mkubwa?

La hasha.

Aliyepewa mtaji mkubwa atadaiwa kurejesha mapato makubwa zaidi.

Kupewa uongozi wa nchi ni kupewa mtaji, mtaji mkubwa. Ukipewa mtaji mkubwa, utadaiwa kuleta mapato makubwa zaidi.

Unapogombea uongozi, inabidi ujitafakari. Ujiulize, mimi naweza mikiki ya public life? Nawez akuwa na ngozi ya mamba ya kutotetereka nikitupiwa mawe? Nina kifua cha kukaa na maneno? Kutojibu matusi kwa matusi?

Kama huwezi, usigombee uongozi.

Waswahili wanasema "ukubwa gunia la chawa". Walielewa kwamba ukubwa unamletea mtu matusi na kejeli, kufanya kazi bila kushukuriwa, lawama n.k.

Noblesse Oblige.

Hizi sheria za kukingia viongozi matusi (Lese Majeste), ni sheria za zama za kisultani an kifalme. Enzi za demokrasia, sheria hizi zimepitwa na wakati.

Hizi ni zama za uhuru wa kujieleza, si zama za censorship.

Rais anatakiwa kuwa mtu w amwisho kabisa kulindwa na sheria dhidi ya matusi.

Lese Majeste is not protection of leaders against insults.

No.

Lese Majeste is an insult to freedom of speech.
Mtukufu Kiranga Shikamoo! Shikamoo kaka mkubwa!
 
Hivi king Swahili kimetushinda sikuhizi mtu akisema/kukusengenya anakuwa amekutukana? Hebu titofautishe neno tusi na neno kusemwa
Naunga mkono hoja, ila kanuni ya kutukana kwanza ni mtu yoyote anayemtukana mwingine, lazima huyu aliyetukanwa alalamike

Pili hilo linaloitwa ni tukano lazima liwe tukano kweli, mimi nimezisikiliza zile voice notes, kuna wengine wameomba tuu msamaha kwa vile wamemzungumzia rais na voice notes zao zika leak lakini hazina matukano yoyote.

Kwa vile aliyedai kutukanwa kesha samehe, who is he kuendelea kuwahoji?. Na kamati ya maadili inaweza kwanza ku establish matukano kwanza ndipo iwaite?.

P
 
Nani kawambia mzee huwa anamoyo wa kusamehe? Jamaa hawezi kuficha sura yake,ni bingwa wa kulipiza
 
Rais anatakiwa kuwa ni mtu anayeweza kutukanwa sana bila anayetukana kufunguliwa mashtaka.

Yani, katika watu ambao mtu anaweza kuwatukana vibaya sana, bila kufunguliwa mashtaka, wa kwanza kabisa anatakiwa kuwa rais.

Wananchi wengine wote wanatakiwa kuwa na kinga ya kisheria dhidi ya kutukanwa kumpita rais.

Kwa nini?

Kuna msemo mmoja wa Kifaransa, wanasema "Noblesse Oblige". Maana yake ni kwamba, wanaopewa nafasi kubwa za kuongoza jamii, wanawajibika kubeba mzigo mkubwa zaidi".

Msemo huu unatoka katika Biblia. Bwana Yesu (namuongelea kama mwanafalsafa, si Mungu wala Mtume, kwa wale ambao watataka kurukia hili kuonesha namuamini kidini) alitoa mfano wa talanta katika kitabu cha Mathayo 25: 14 - 30.

Kwa kifupi, alisema kwamba, kama kuna watu vijakazi kadhaa, wamepewa mtaji na bwana wao wakafanyie kazi, wengine wamepewa mtaji mkubwa, wengine wamepewa mtaji mdogo, wakimaliza kufanya kazi zao, nani atadaiwa marejesho zaidi?

Aliyepewa mtaji mdogo atadaiwa arejeshe mapato zaidi ya aliyepewa mtaji mkubwa?

La hasha.

Aliyepewa mtaji mkubwa atadaiwa kurejesha mapato makubwa zaidi.

Kupewa uongozi wa nchi ni kupewa mtaji, mtaji mkubwa. Ukipewa mtaji mkubwa, utadaiwa kuleta mapato makubwa zaidi.

Unapogombea uongozi, inabidi ujitafakari. Ujiulize, mimi naweza mikiki ya public life? Nawez akuwa na ngozi ya mamba ya kutotetereka nikitupiwa mawe? Nina kifua cha kukaa na maneno? Kutojibu matusi kwa matusi?

Kama huwezi, usigombee uongozi.

Waswahili wanasema "ukubwa gunia la chawa". Walielewa kwamba ukubwa unamletea mtu matusi na kejeli, kufanya kazi bila kushukuriwa, lawama n.k.

Noblesse Oblige.

Hizi sheria za kukingia viongozi matusi (Lese Majeste), ni sheria za zama za kisultani an kifalme. Enzi za demokrasia, sheria hizi zimepitwa na wakati.

Hizi ni zama za uhuru wa kujieleza, si zama za censorship.

Rais anatakiwa kuwa mtu w amwisho kabisa kulindwa na sheria dhidi ya matusi.

Lese Majeste is not protection of leaders against insults.

No.

Lese Majeste is an insult to freedom of speech.
You are correct! Lakini nadhani hawa CCM ni kama familia. Ndani ya familia haitakuwa na sheria inayotoa nafasi kwa baba au mama kutukanwa na wana familia. Wana CCM walioamua kumtukana M/kiti wao waliyafanya wakijua yuko kwenye uongozi wa familia. Let them be reprimanded, internally.

Sasa acha wapewe adhabu ya kifamilia.
 
Naiona "Membe effect is alarming within the party" tuelekeapo 2020.
 
Back
Top Bottom