Dr. Bashiru: Wale wote waliomtukana Rais Magufuli bado wana mashtaka ya kujibu mbele ya CCM, msamaha waliopata ni wa Dr Magufuli siyo CCM

Dr. Bashiru: Wale wote waliomtukana Rais Magufuli bado wana mashtaka ya kujibu mbele ya CCM, msamaha waliopata ni wa Dr Magufuli siyo CCM

Mimi nilikunukuu tu ulivyosema Rais au mtu akiwa kiongozi wa watu anatakiwa atukanwe sana na aweze kuvumilia "matusi" kuliko mtu wa kawaida.

Sasa tafsiri yoyote ya matusi uliyokuwa ukimaanisha hapo, ndipo hoja yangu ilipo.

Matusi ni matusi. Hata ukileta ujanja ujanja wa maneno hakuna mtu timamu asiyeelewa matusi ni yapi.

Kuna muda unakera sana unavyojitoa fahamu kwa makusudi mzee wangu.
Unaelewa kwamba hakuna nilipoandika mtu akiwa kiongozi wa watu anatakiwa atukanwe sana?

Unaelewa kwamba ukinisoma kwamba nimeandika hivyo, utakuwa umeshindwa kusoma kwa ufahanu?

Unaelewa kwamba mpaka hapo tu hujaelewa nimeandika nini?
 
Sasa makes sense Jmakamba aliposema nadhani Kama atagombea Tena ubunge wa bumbuli.

Cheche kibua Nazi. CCM oyeeeee
 
Naunga mkono hoja, ila kanuni ya kutukana kwanza ni mtu yoyote anayemtukana mwingine, lazima huyu aliyetukanwa alalamike

Pili hilo linaloitwa ni tukano lazima liwe tukano kweli, mimi nimezisikiliza zile voice notes, kuna wengine wameomba tuu msamaha kwa vile wamemzungumzia rais na voice notes zao zika leak lakini hazina matukano yoyote.

Kwa vile aliyedai kutukanwa kesha samehe, who is he kuendelea kuwahoji?. Na kamati ya maadili inaweza kwanza ku establish matukano kwanza ndipo iwaite?.

P

Pascal wengine tumekulia Seminari naomba niorodheshee matusi aliyotukanwa Baba nami niyajue
 
Dr Bashiru achana na issues hizo, ili mradi Mwenyekiti CCM kasamehe na ni boss wetu sote, na ww Katibu Mkuu waache wenzako hakuna asiyekosea, hii itaonyesha kuwa msamaha walioupata kwa Mh. Rais hauna maana. Plse tunakuomba msamaha ulitoka, basi acha kuwafunga kamba shingo tena waliokosea na wamepata msamaha.
Kwanini usiamini kwamba mwenyekiti anaweza kupitia kwa katibu kuwanyoosha waomba msamaha
 
Nadhani hapa ndipo mnapokosea kazi ya Uma ni tofauti na familia yako ni hivi unapokuwa kiongozi unakuwa unaongoza watu ambao kula kwako na kustarehe kwako ni kodi zao so unapofanya ujinga wakukopa hela kwenye taasisi za kifedha duniani nakuiongezea deni nchi na pesa zenyewe unanunulia wanasiasa njaa ili uonekane unakubalika nivipi watu wasikutukane ingawa kusema ukweli sidhani kama ni tusi au wenzetu ndio mmefanya rais kama anaongoza familia yake badala ya Taifa
Hilo linatakiwa lianzie kwenye familia yako,kma wewe ni baba wa familia ruhusu utukanwe na familia yako, na kama bado upo kwa wazazi wako,anza kutukana babako maana wakati mwingine anakuzuia kufanya jambo ambalo unaona ni haki yako kufanya au kushindwa kutimiza mahitaji yako. Hata mungu pamoja na yote yanayotokea ya kupoteza mali na wapendwa wetu inagawa ana uwezo wa kuzuia, lakini tunamsifu na kusema ni mapenzi yake. Huku unalia kwa maumivu.
W
 
Atatuumiza sana mwamba. Na kosa kila mtu anaogopa.
Wale wa enzi ya Nyerere angalau walijaribu kumpinga waziwazi. Sie waoga wengi ngoja tuendelee kuvuna woga.
 
Kama heshima ya Rev. Jackson imeshuka, si kwa sababu ya kumsema vibaya Obama.

Nimeishi Marekani kipindi chote cha urais wa Obama, na hata kabla yacho.

Kuna watu waliheshimika sana katika jamii ya watu weusi Marekani.

Namumbuka Cornel West, mhadhiri Profesa mweusi aliyefundisha Ivy League, Princeton University. Na mwingine Travis Smiley, muendesha kipindi wa televisheni ya jamii PBS.

Wawili hawa walimshambulia Rais Obama sana kwa namna ambayo mwanzo sikuielewa wala kuitarajia.

Kwa sababu walikiwa ni weusi na wana watu wengi wanawafuatilia, mmoja akitoka academia, muandiahi wa vitabu vingi ambavyo nilikwishasoma na kujua msimamo wake (Cornel West) na mwingine mtangazaji wa TV ambaye karibu kila wiki nilikuwa namtizama, wote walitaka maendeleo kwa watu weusi na masikini.

Wote walitaka mtu kama Obama awe rais.

Nikashangaa sana, imekuwaje Obama kawa rais, halafu wanamswma vibaya badala ya kumuunga mkono?

Nikagundua kitu.

Marekani hata watu wanaokuunga mkono wanaweza kukushambulia.

Ni kwa mujibu wa kanuni ya rais Frank Delano Roosevelt ya "Go and Make Me Do It".

Rais Roosevelt alifuatwa na jamaa mmoja mtu wa vyama vya wafabyakazi. Jamaa alikuwa na malalamimo kibao. Akamlalamikia sana rais Roosevelt, akimtaka rais awafanyie hili na lile.

Rais akamwambia, malalamiko yako nimeyasikia. Ila, sitayafanyia kazi.

Ili niyafanyie kazi, nakutaka uende tena uraiani huko, unipigie kelele, unitake niyafanyie kazi, Marekani nzima iyajue malalamiko yako, ukiyapigia kelele hivyo, yakijulikana, nayafanyia kazi.

Alimwambia "Go and make me do it".

Marekani hatupendi hagiography. Mtu anaweza kumsema vibaya Obama kwamba hajafanya hiki na lile, si kwa sababu hamoendi Obama. Hasha.

Bali kwa sababu anampenda sana Obama na anatamani Obama angefanya zaidi, pakubwa kupita alipofanya.

View attachment 1274876
ila huku kusiko marekani vipi??

lengo ni hilo hilo?
 
Pascal wengine tumekulia Seminari naomba niorodheshee matusi aliyotukanwa Baba nami niyajue
Nimeorodhesha hapa

P
 
Unaelewa kwamba hakuna nilipoandika mtu akiwa kiongozi wa watu anatakiwa atukanwe sana?

Unaelewa kwamba ukinisoma kwamba nimeandika hivyo, utakuwa umeshindwa kusoma kwa ufahanu?

Unaelewa kwamba mpaka hapo tu hujaelewa nimeandika nini?

Umekwepa hoja ya matusi. Kwaheri.
 
Nimeorodhesha hapa

P

Asante mkuu na kama kawaida nimekuelewa kuliko mamama chanja wako wanavyokuelewaga....tuendelee na mijadala poa
 
Kiranga,
Uhuru wa kujieleza tusiujenge kwenye dhana hiyo. Utakuwa ni ujinga!

Matusi hayaleti masikilizano bali mifarakano tu. Mtu akikutukana maana yake hakuheshimu na hakuthamini, sasa nani anakusikiliza ukimtukana?

Hata humu JF tunajadiliana na kukosoana kwa hoja, siyo matusi. Sheria za hapa zenyewe haziruhusu lugha za hivyo kwa sababu hazina muafaka.

Matusi sio hoja wala shauri. Ni matusi. HAYAFAI.
Katika mfumo wa ubepari rais anatukanwa kadri watu wanavyojisikia.

Lakini sisi kuupokea mfumo huo sio kigezo cha mila na maadii yetu kusalimu amri.

Unaweza kweli kumtukana Baba nyumbani ambaye ndio anayeshinda juani akitafuta riziki ya nyumbani?.
 
Katika mfumo wa ubepari rais anatukanwa kadri watu wanavyojisikia.

Lakini sisi kuupokea mfumo huo sio kigezo cha mila na maadii yetu kusalimu amri.

Unaweza kweli kumtukana Baba nyumbani ambaye ndio anayeshinda juani akitafuta riziki ya nyumbani?.
Rais si baba. Rais ni kijakazi.

Wewe ulipiga kura kumchagua baba yako?
 
Rais si baba. Rais ni kijakazi.

Wewe ulipiga kura kumchagua baba yako?
Rais ni nembo ya taifa ndio maana nyuma yake anasimama mwanajeshi.

Angekuwa ni mtu baki tu yasingetumika mamilioni katika kumlinda.

Sisi sio wamarekani wenye maadili na tamaduni zisizofanana na nchi za kiafrika.
 
Kwanza kwani wale jamaa walisema CCM 'mshamba' au walisema mzee mshamba? Sasa mzee kawasamehe baada ya kujua walisema kweli. Sasa hapo CCM inahusikaje na kadhia hiyo?
Mkuu haya mambo ni kukosa busara na utoto tu. Pia ni kutafuta kiki kama wanavyosema watu siku hizi, ni wazi CCM haihusiki. Kudukua maongezi ya mtu bila kibali cha mahakama ni uhalifu na kukiuka haki ya faragha ya mtu kinyume na katiba. Sasa huwezi kutumia ushahidi uliopatikana kwa njia za kihalifu kumuadhibu mtu hata kwa ngazi ya chama. Hata kangaroo courts kwenye failed states hawawezi kufanya huu ujinga.
 
Back
Top Bottom