Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 89,019
- 156,726
Unaelewa nilichoandika ni nini?"Rais anatakiwa kuwa ni mtu anayeweza KUTUKANWA sana bila anayetukana kufunguliwa mashtaka".
"Yani, katika watu ambao mtu anaweza KUWATUKANA vibaya sana, bila kufunguliwa mashtaka, wa kwanza kabisa anatakiwa kuwa rais".
"Wananchi wengine wote wanatakiwa kuwa na kinga ya kisheria dhidi ya KUTUKANWA kumpita rais."
"Unapogombea uongozi, inabidi ujitafakari. Ujiulize, mimi naweza mikiki ya public life? Naweza kuwa na ngozi ya mamba ya kutotetereka nikitupiwa mawe? Nina kifua cha kukaa na maneno? Kutojibu MATUSI kwa MATUSI?"
"Hizi sheria za kukingia viongozi MATUSI (Lese Majeste), ni sheria za zama za kisultani an kifalme. Enzi za demokrasia, sheria hizi zimepitwa na wakati."
"Rais anatakiwa kuwa mtu wa mwisho kabisa kulindwa na sheria dhidi ya MATUSI."
------
Ndio maana nasema unajidhalilisha tu.
I refer matusi hayo uliyomaanisha hapo kwenye maelezo yako ya awali.
Najua huyapendi tena kwa sababu uliyaandika kwa mihemko bila kufikiria. Sasa hivi yanakuchoma.
Unajichoresha!
Unaelewa kwamba nikiandika kwamba rais anatakiwa kuwa ni mtu anayeweza kutukanwa sana bila anayemtukana kufunguliwa mashtaka naongelea a legal matter? Naongeleea potential? Unaelewa potential ni nini?
Unaelewa naongelea Lese Majeste?
Unaelewa Lese Majeste ni nini?
Unaelewa kwamba naongelea relativity?
Unaelewa kwamba nikisema rais anatakiwa kuwa ni mtu anayelipwa mshahara mdogo kabisa katika nchi, kauli hiyo haimaanishi anyimwe mshahara wa kukidhi mahitaji yake?
Unajua kusoma kwa ufahamu?
Nimekuuliza, nikisema Magufuli ni mshenzi mwenye majibu ya kunya, kwa sababu kamwambia mwanamme aliyemuuliza kwa nini mtaani hakuna hela aolewe, utasema namtukana Magufuli au nasema ukweli tu?
Wewe unayejinadi kupenda ustaarabu, unaona hayo maneno ya Magufuli kumwambia mwanamme aolewe ni ustaarabu?
Nikisema huyo rais wenu Magufuli ni mshenzi mwenye majibu ya kunya, nitakuwa nimemtukana au nimesema ukweli tu?
Mbona hujibu swali hili?