Dr. Bashiru: Wale wote waliomtukana Rais Magufuli bado wana mashtaka ya kujibu mbele ya CCM, msamaha waliopata ni wa Dr Magufuli siyo CCM

Dr. Bashiru: Wale wote waliomtukana Rais Magufuli bado wana mashtaka ya kujibu mbele ya CCM, msamaha waliopata ni wa Dr Magufuli siyo CCM

Nakumbuka enzi zile za Kaisari mtu akisamehewa na Kaisari hakuna wa kumhukumu kwa lolote mtu yule rejea Baraba na Masii Kristo.
CCM kutokuwasamehe waliokwisha samehewa na Mwenyekiti wao ni kumpiga Mwenyekiti.
 
Naunga mkono hoja, ila kanuni ya kutukana kwanza ni mtu yoyote anayemtukana mwingine, lazima huyu aliyetukanwa alalamike

Pili hilo linaloitwa ni tukano lazima liwe tukano kweli, mimi nimezisikiliza zile voice notes, kuna wengine wameomba tuu msamaha kwa vile wamemzungumzia rais na voice notes zao zika leak lakini hazina matukano yoyote.

Kwa vile aliyedai kutukanwa kesha samehe, who is he kuendelea kuwahoji?. Na kamati ya maadili inaweza kwanza ku establish matukano kwanza ndipo iwaite?.

P
Nape alikuwa kambale ndani ya chama alijifanya ccm ya kwake na team ile kumbe asijue ccm imesharudi kwa wananchi siyo Mali ya familia au kundi fulani Mimi naona tu wasulubiwe hamna namna wajifunze chama ni zaidi ya wao
 
Unavyojitahidi kukwepa hoja yako wakati uliileta mwenyewe, inadhihirisha wazi kuwa hata we mwenyewe unaona kabisa matusi sio jambo jema.

Wakubwa tunaelewana. Umechutama.
Hoja yangu ipi?

Utajuaje hoja yangu ni ipi wakati si tu hujui kusoma kwa ufahamu, huna hata utashi wa kutaka kufundishwa?
 
Wewe ambaye si tu hujui kusoma, bali pia hata hutaki kujua kusoma, umejivua nguo kabisa, si kujidhalilisha tu.

Jadili hoja, usipayuke.

Argue, don't shout.
Tunajadilije hoja ambayo unaikataa wakati uliileta wewe mwenyewe?

Eti "Yani, katika watu ambao mtu anaweza kuwatukana vibaya sana, bila kufunguliwa mashtaka, wa kwanza kabisa anatakiwa kuwa rais".

Hakuna namna utaweza kujustify matusi/kutukana, ukaeleweka kwa watu wanaojali ustaarabu. Hakuna.

Unazidi kujichoresha tu hapa!
 
Wewe huelewi tofauti ya ku protest Lese Majeste na ku justify matusi.

Huelewi au hutaki kukubali kwamba, katika nchi yenye Lese Majeste, hata constitutionally protected free speech inaweza kuitwa matusi.

Nikisema Magufuli ni mshenzi, kwa sababu kaulizwa na mtu mwanamme, kwa heshima tu, kwa nini watu hawana hela mtaani? Kwa nini mzunguki wa fedha umebanwa hivi? Magufuli akajibu akasema huyo mtu afanye kazi, ama sivyo aolewe.

Mtu mwanamme!

Hapo nikisema Magufuli ni mshenzi mwenye majibu ya kunya, nitakuwa nimemtukana au nimesema ukweli tu kwa sababu ni kweli Magufuli ni mshenzi ana majibu ya kunya?

Unatenganishaje hapa nimesema ukweli tu, na hapa ninemtukana rais, katika nchi top down kama Tanzania?

The world is full of counterintuitive notions.

It is quite possible, a country in which there us ni Lese Majeste, and the citizens are allowed to trash their leadership, is more civikized than a country in which there is Lese Majeste and the citizens are not allowed to trash their leaders.

In fact thus us the case now. All advanced demicracrues did away with Lese Majeste.

While all dictatorships enforce Lese Majeste.
 
Rais anatakiwa kuwa ni mtu anayeweza kutukanwa sana bila anayetukana kufunguliwa mashtaka.

Yani, katika watu ambao mtu anaweza kuwatukana vibaya sana, bila kufunguliwa mashtaka, wa kwanza kabisa anatakiwa kuwa rais.

Wananchi wengine wote wanatakiwa kuwa na kinga ya kisheria dhidi ya kutukanwa kumpita rais.

Kwa nini?

Kuna msemo mmoja wa Kifaransa, wanasema "Noblesse Oblige". Maana yake ni kwamba, wanaopewa nafasi kubwa za kuongoza jamii, wanawajibika kubeba mzigo mkubwa zaidi".

Msemo huu unatoka katika Biblia. Bwana Yesu (namuongelea kama mwanafalsafa, si Mungu wala Mtume, kwa wale ambao watataka kurukia hili kuonesha namuamini kidini) alitoa mfano wa talanta katika kitabu cha Mathayo 25: 14 - 30.

Kwa kifupi, alisema kwamba, kama kuna watu vijakazi kadhaa, wamepewa mtaji na bwana wao wakafanyie kazi, wengine wamepewa mtaji mkubwa, wengine wamepewa mtaji mdogo, wakimaliza kufanya kazi zao, nani atadaiwa marejesho zaidi?

Aliyepewa mtaji mdogo atadaiwa arejeshe mapato zaidi ya aliyepewa mtaji mkubwa?

La hasha.

Aliyepewa mtaji mkubwa atadaiwa kurejesha mapato makubwa zaidi.

Kupewa uongozi wa nchi ni kupewa mtaji, mtaji mkubwa. Ukipewa mtaji mkubwa, utadaiwa kuleta mapato makubwa zaidi.

Unapogombea uongozi, inabidi ujitafakari. Ujiulize, mimi naweza mikiki ya public life? Nawez akuwa na ngozi ya mamba ya kutotetereka nikitupiwa mawe? Nina kifua cha kukaa na maneno? Kutojibu matusi kwa matusi?

Kama huwezi, usigombee uongozi.

Waswahili wanasema "ukubwa gunia la chawa". Walielewa kwamba ukubwa unamletea mtu matusi na kejeli, kufanya kazi bila kushukuriwa, lawama n.k.

Noblesse Oblige.

Hizi sheria za kukingia viongozi matusi (Lese Majeste), ni sheria za zama za kisultani an kifalme. Enzi za demokrasia, sheria hizi zimepitwa na wakati.

Hizi ni zama za uhuru wa kujieleza, si zama za censorship.

Rais anatakiwa kuwa mtu w amwisho kabisa kulindwa na sheria dhidi ya matusi.

Lese Majeste is not protection of leaders against insults.

No.

Lese Majeste is an insult to freedom of speech.
Tupo pamoja
 
Anataka utukufu wake uwe wa umalaika mkuu.
Bwana yule kawageuka na ni wazi amegundua bado hawataki kumlamba miguu.
IMG_20191127_114040_634.JPG
View attachment 1277444
 
Magufuli ndiye CCM. Bashiru anajifurahisha tu hapa. Wale jamaa "waliomtukana" Meko na kumuita mshamba walifanya hivyo in an individual capacity, not as mwenyekiti wa CCM. Kwa akili hizi za Bashiru maana yake hata AG nae awaite basi na kuwafungulia mashtaka. CDF (au IGP) nae awakamate na kuwashtaki kwa kumtukana Amiri Jeshi Mkuu.
 
Hivi "aliyetukanwa" ni John Magufuli, Rais wa Tanzania au Mwenyekiti wa CCM? Wanaosemwa waliotukana, walimtukana kama nani?

Na aliyesamehe, amesamehe kama nani? Rais, John au Mwenyekiti wa CCM? Dr. Bashiru anaweza kujikuta anatakiwa pia kumwajibisha mwenyekiti wa CCM kwa kosa la kutofuata katiba ya CCM katika kusamehe!
 
Magufuli ndiye CCM. Bashiru anajifurahisha tu hapa. Wale jamaa "waliomtukana" Meko na kumuita mshamba walifanya hivyo in an individual capacity, not as mwenyekiti wa CCM. Kwa akili hizi za Bashiru maana yake hata AG nae awaite basi na kuwafungulia mashtaka. CDF (au IGP) nae awakamate na kuwashtaki kwa kumtukana Amiri Jeshi Mkuu.
Kwanza kabisa, mkubwa wako wa kazi akishatoa msamaha, halafu wewe usiukubali ule msamaha, ukashindwa kuongea naye aubatilishe, ukaanza kuutengua wewe hadharani, katika maadili ya kazi hiyo ni insubordination.

Umempinga mkubwa wako wa kazi wazi na hadharani. Umemfanya yeye ni mjinga hana akili kutoa huo msamaha, umejifanya wewe ndiye unajua zaidi.

Mwenyekiti wa chama katoa msamaha, Katibu Mkuu kakaidi kuheshimu msamaha.

CCM haina dira wala muelekeo kama alivyosema Horace Kolimba.
 
Magufuli the way nimwonavyo, sio mtu wa kusamehe ni mtu wa visasi sana. Usijekuta yeye ndio amemwagiza huyo Bashiru ajiandae kuwachukulia hao hatua.

Wanaong'ang'ania kuwa ccm ni sawa na wana wa Israel waliokuwa wanadai heri wangerejea Misri.

Akina Nape wana wakati mgumu sana, wanapitia kipindi kigumu mno ktk maisha yao ya kisiasa. Watakuwa wanajuta kumfanyia Lowassa hila.
 
Wewe huelewi tofauti ya ku protest Lese Majeste na ku justify matusi.

Huelewi au hutaki kukubali kwamba, katika nchi yenye Lese Majeste, hata constitutionally protected free speech inaweza kuitwa matusi.

Nikisema Magufuli ni mshenzi, kwa sababu kaulizwa na mtu mwanamme, kwa heshima tu, kwa nini watu hawana hela mtaani? Kwa nini mzunguki wa fedha umebanwa hivi? Magufuli akajibu akasema huyo mtu afanye kazi, ama sivyo aolewe.

Mtu mwanamme!

Hapo nikisema Magufuli ni mshenzi mwenye majibu ya kunya, nitakuwa nimemtukana au nimesema ukweli tu kwa sababu ni kweli Magufuli ni mshenzi ana majibu ya kunya?

Unatenganishaje hapa nimesema ukweli tu, na hapa ninemtukana rais, katika nchi top down kama Tanzania?

The world is full of counterintuitive notions.

It is quite possible, a country in which there us ni Lese Majeste, and the citizens are allowed to trash their leadership, is more civikized than a country in which there is Lese Majeste and the citizens are not allowed to trash their leaders.

In fact thus us the case now. All advanced demicracrues did away with Lese Majeste.

While all dictatorships enforce Lese Majeste.
Ruka utakavyoruka, matusi ni matusi.

Unajaribu kuremba maneno hapa na kuandika misamiati mingi bila sababu za msingi, ili mradi tu ionekane ni sawa mtu fulani kutukanwa kwa sababu fulani.

Kama ni kweli unaheshimu utu wa mtu, utaona hatia kwenye maneno yako. Lakini kama lengo ni kuwin this argument, well, go on and take it all.

Unaonekana ni mtu dhaifu sana wewe. Pole.
 
"Matusi ni matusi" is a tautology.

It doesn't tell us anything on what matusi is.

Nimekuuliza swali very specific.

Umeshindwa kujibu.

Kwa sababu hujui unaenda mbele au unarudi nyuma.
 
"Matusi ni matusi" is a tautology.

It doesn't tell us anything on what matusi is.

Nimekuuliza swali very specific.

Umeshindwa kujibu.

Kwa sababu hujui unaenda mbele au unarudi nyuma.
"Rais anatakiwa kuwa ni mtu anayeweza KUTUKANWA sana bila anayetukana kufunguliwa mashtaka".

"Yani, katika watu ambao mtu anaweza KUWATUKANA vibaya sana, bila kufunguliwa mashtaka, wa kwanza kabisa anatakiwa kuwa rais".

"Wananchi wengine wote wanatakiwa kuwa na kinga ya kisheria dhidi ya KUTUKANWA kumpita rais."

"Unapogombea uongozi, inabidi ujitafakari. Ujiulize, mimi naweza mikiki ya public life? Naweza kuwa na ngozi ya mamba ya kutotetereka nikitupiwa mawe? Nina kifua cha kukaa na maneno? Kutojibu MATUSI kwa MATUSI?"

"Hizi sheria za kukingia viongozi MATUSI (Lese Majeste), ni sheria za zama za kisultani an kifalme. Enzi za demokrasia, sheria hizi zimepitwa na wakati."

"Rais anatakiwa kuwa mtu wa mwisho kabisa kulindwa na sheria dhidi ya MATUSI."
------

Ndio maana nasema unajidhalilisha tu.

I refer matusi hayo uliyomaanisha hapo kwenye maelezo yako ya awali.

Najua huyapendi tena kwa sababu uliyaandika kwa mihemko bila kufikiria. Sasa hivi yanakuchoma.

Unajichoresha!
 
Back
Top Bottom