Dr. Bashiru: Wale wote waliomtukana Rais Magufuli bado wana mashtaka ya kujibu mbele ya CCM, msamaha waliopata ni wa Dr Magufuli siyo CCM

Dr. Bashiru: Wale wote waliomtukana Rais Magufuli bado wana mashtaka ya kujibu mbele ya CCM, msamaha waliopata ni wa Dr Magufuli siyo CCM

Wewe ngumbaru usiyejua kusoma kwa ufahamu hoja ya matusi ukiiona utaijua?
"Rais anatakiwa kuwa ni mtu anayeweza kutukanwa sana bila anayetukana kufunguliwa mashtaka.

Yani, katika watu ambao mtu anaweza kuwatukana vibaya sana, bila kufunguliwa mashtaka, wa kwanza kabisa anatakiwa kuwa rais"

Huoni hata aibu!
 
Unajua kusoma? Kwa ufahamu?

Nilichoandika mimi na unachonikashifu kuandika ni vitu viwili tofauti.

Unaelewa hilo?

Unataka tujadili neno kwa neno?

Do you understand that a protest against Lese Majeste is not necessarily an act to incite the populace to trash the national leadership?

Unaelewa kwamba nikitetea haki yako ya kupiga kura, hilo halimaanishi kwamba nakushurutisha wala nakutaka upige kura?
 
Rais ni nembo ya taifa ndio maana nyuma yake anasimama mwanajeshi.

Angekuwa ni mtu baki tu yasingetumika mamilioni katika kumlinda.

Sisi sio wamarekani wenye maadili na tamaduni zisizofanana na nchi za kiafrika.
Jibu swali! Ni lini ulipanga foleni kumpigia kura baba yako? Au kwenye tumbo la mama yaku kulikuwa na sanduku ya kupigia kura? Usijitoe fahamu kwa hizo ngonjera za ulinzi ili kukwepa swali.
 
Jibu swali! Ni lini ulipanga foleni kumpigia kura baba yako? Au kwenye tumbo la mama yaku kulikuwa na sanduku ya kupigia kura? Usijitoe fahamu kwa hizo ngonjera za ulinzi ili kukwepa swali.
Mkuu Right Guy rais wa nchi sio sawa na admin wa kundi la whatsapp ukimdharau hadharani jiandae kwa lolote.

Hao mambo ya Baba na Mama ni irrelevant.
 
Rais anatakiwa kuwa ni mtu anayeweza kutukanwa sana bila anayetukana kufunguliwa mashtaka.

Yani, katika watu ambao mtu anaweza kuwatukana vibaya sana, bila kufunguliwa mashtaka, wa kwanza kabisa anatakiwa kuwa rais.

Wananchi wengine wote wanatakiwa kuwa na kinga ya kisheria dhidi ya kutukanwa kumpita rais.

Kwa nini?

Kuna msemo mmoja wa Kifaransa, wanasema "Noblesse Oblige". Maana yake ni kwamba, wanaopewa nafasi kubwa za kuongoza jamii, wanawajibika kubeba mzigo mkubwa zaidi".

Msemo huu unatoka katika Biblia. Bwana Yesu (namuongelea kama mwanafalsafa, si Mungu wala Mtume, kwa wale ambao watataka kurukia hili kuonesha namuamini kidini) alitoa mfano wa talanta katika kitabu cha Mathayo 25: 14 - 30.

Kwa kifupi, alisema kwamba, kama kuna watu vijakazi kadhaa, wamepewa mtaji na bwana wao wakafanyie kazi, wengine wamepewa mtaji mkubwa, wengine wamepewa mtaji mdogo, wakimaliza kufanya kazi zao, nani atadaiwa marejesho zaidi?

Aliyepewa mtaji mdogo atadaiwa arejeshe mapato zaidi ya aliyepewa mtaji mkubwa?

La hasha.

Aliyepewa mtaji mkubwa atadaiwa kurejesha mapato makubwa zaidi.

Kupewa uongozi wa nchi ni kupewa mtaji, mtaji mkubwa. Ukipewa mtaji mkubwa, utadaiwa kuleta mapato makubwa zaidi.

Unapogombea uongozi, inabidi ujitafakari. Ujiulize, mimi naweza mikiki ya public life? Nawez akuwa na ngozi ya mamba ya kutotetereka nikitupiwa mawe? Nina kifua cha kukaa na maneno? Kutojibu matusi kwa matusi?

Kama huwezi, usigombee uongozi.

Waswahili wanasema "ukubwa gunia la chawa". Walielewa kwamba ukubwa unamletea mtu matusi na kejeli, kufanya kazi bila kushukuriwa, lawama n.k.

Noblesse Oblige.

Hizi sheria za kukingia viongozi matusi (Lese Majeste), ni sheria za zama za kisultani an kifalme. Enzi za demokrasia, sheria hizi zimepitwa na wakati.

Hizi ni zama za uhuru wa kujieleza, si zama za censorship.

Rais anatakiwa kuwa mtu w amwisho kabisa kulindwa na sheria dhidi ya matusi.

Lese Majeste is not protection of leaders against insults.

No.

Lese Majeste is an insult to freedom of speech.
Matusi angestahili endapo angeshindwa Ku deliver. Lakini huyu anatukanwa kwa kudeliver.
 
Matusi angestahili endapo angeshindwa Ku deliver. Lakini huyu anatukanwa kwa kudeliver.

Nadhani hatukanwi kwa ku deliver. Anatukanwa kwa sababu ya ku-infringe upon the rights of his citizens, which is mostly felt by those who are his detractors.
Lakini hata hilo halikustahili lugha za matukano na kejeli kwa watu waungwana kama watanzania.
Sema tu matusi na kejeli ndio lugha iliyobaki kwa wanasiasa wa kizazi hiki kama ambavyo hata yeye mwenyewe hayuko nyuma sana kutuonesha.
 
Matusi angestahili endapo angeshindwa Ku deliver. Lakini huyu anatukanwa kwa kudeliver.
That is a matter of perspective.

Mapato ya bidhaa za kilimo kwa mwaka unaoishia Agosti 2019 yameporomika kwa asilimia 55.

Ripoti ya BOT ya Oktoba 2019 inaonesha hili.

Kwa kiasi kikubwa kutokana na serikali kuingilia biashara ya korosho, zao la kwanza kwa kuleta fedha za kigeni nchini.

Sasa hapo rais ana deliver nini?

Poromoko la mapato ya kilimo la asilimia 55, ndiyo unaita ku deliver?

Yani, kwa kila shilingi 1000 tuliyopata mwaka wa kabla ya huu uliopita, mwaka huu uliopita tumepata shilingi 450.

That is a decline of more than half, in the period of 12 months.

Katika kilimo, jambo la msingi kabisa kwenye uchumi wetu.

Hapo bado unajigamba rais ana deliver?
 
Katibu mkuu wa CCM, Dr Bashiru Ally amesema wale wote waliomtukana Mwenyekiti wa CCM, Dr. Magufuli bado wana kesi ya kujibu mbele ya kamati ya nidhamu ya chama.

Dr. Bashiru amesema wale walioomba msamaha na kusamehewa walifanya hivyo kama watu binafsi na Dr. Magufuli aliwasamehe kama mzazi lakini kwenye chama mashtaka yao yapo palepale na muda ukifika wataitwa kujieleza na kuchukuliwa hatua " rasmi" kwa namna itakavyoonekana inafaa kwa mujibu wa katiba ya chama.

Chanzo: ITV habari!
Nape Nnauye njoo huku comrade uwasikie wambea wanataka kukutilia mchanga kitumbua chako!!
 
Katibu mkuu wa CCM, Dr Bashiru Ally amesema wale wote waliomtukana Mwenyekiti wa CCM, Dr. Magufuli bado wana kesi ya kujibu mbele ya kamati ya nidhamu ya chama.

Dr. Bashiru amesema wale walioomba msamaha na kusamehewa walifanya hivyo kama watu binafsi na Dr. Magufuli aliwasamehe kama mzazi lakini kwenye chama mashtaka yao yapo palepale na muda ukifika wataitwa kujieleza na kuchukuliwa hatua " rasmi" kwa namna itakavyoonekana inafaa kwa mujibu wa katiba ya chama.

Chanzo: ITV habari!

Spinning Dr At Work.

Nawakumbusha habari za Mjini.
==UCHAFUZI WA SIRIKALI ZA MITAA
==LISSU INTERVIEW NAIROBERIA NI FIRE
 
Nadhani hatukanwi kwa ku deliver. Anatukanwa kwa sababu ya ku-infringe upon the rights of his citizens, which is mostly felt by those who are his detractors.
Lakini hata hilo halikustahili lugha za matukano na kejeli kwa watu waungwana kama watanzania.
Sema tu matusi na kejeli ndio lugha iliyobaki kwa wanasiasa wa kizazi hiki kama ambavyo hata yeye mwenyewe hayuko nyuma sana kutuonesha.
Kingine, heshima anaheshimiwa mtu anayejiheshimu.

Magufuli kaulizwa swali kwa heshima kabisa, mtu ana shida kauliza mbona mtaani hela hazipatikani?

Very simple question.

Rais badala ya kumfariji muuliza swali na kumtia moyo, anamwambia afanye kazi, kama hawezi akaolewe. Mtu aliyeuliza ni mwanamme.

Hapo tunaona.

1. Magufuli hajiheshimu. Hivyo hafai kuheshimiwa. Kitaka kumuheshimu mtu asiyejiheshimu yeye mwenyewe ni ujinga.

2. Magufuli anaona watu walioolewa ni dhaifu na hawawezi kufanya kazi, na kuolewa ni njia ya kuepuka kufanya kazi.

3. Magufuli anahalalisha ushoga wa wanaume kuolewa, kinyume na sheria za Tanzania.

Jamaa mdomo hauna breki, hajiheshimu yeye mwenyewe, mnataka watu wamhehimu kwa minajili gani? Kwa sababu rais tu?
 
That is a matter of perspective.

Mapato ya bidhaa za kilimo kwa mwaka unaoishia Agosti 2019 yameporomika kwa asilimia 55.

Ripoti ya BOT ya Oktoba 2019 inaonesha hili.

Kwa kiasi kikubwa kutokana na serikali kuingilia biashara ya korosho, zao la kwanza kwa kuleta fedha za kigeni nchini.

Sasa hapo rais ana deliver nini?

Poromoko la mapato ya kilimo la asilimia 55, ndiyo unaita ku deliver?

Yani, kwa kila shilingi 1000 tuliyopata mwaka wa kabla ya huu uliopita, mwaka huu uliopita tumepata shilingi 450.

That is a decline of more than half, in the period of 12 months.

Katika kilimo, jambo la msingi kabisa kwenye u humi wetu.

Hapo bado unajigamba rais ana deliver?
Mtaalamu usiumize kichwa kumuelewesha mtu wa lumumba,anajua kila kitu sema ndio hivyo wao wapo kumtetea JPM kwa lolote na wanalipwa kwa kufanya hivyo.

JPM amefeli kwa 100%.
-Barabara,umeme,treni hata wakoloni waliweka........JPM anafanya hiyo miradi coz anapiga cha juu na si kama anataka kuleta maendeleo ya vitu.
 
Mi naona mbinu kamili ya kuwatimua imesukwa maana magu hataki kabisa kuona au kuskia vijana wa jk kwenye awamu yake nabinasemekana ni timu mbeme

Acha ushabiki usikuwa na Tija...embu vaa viatu vya magufuli unasikia watu ulikuwa nao karibu wanakuzungumzia vile utajisikiaje..wanakutukana na kukusengenya uku ukikutana nao wanajionesha ni watu wazuri kwako
 
Mtaalamu usiumize kichwa kumuelewesha mtu wa lumumba,anajua kila kitu sema ndio hivyo wao wapo kumtetea JPM kwa lolote na wanalipwa kwa kufanya hivyo.

JPM amefeli kwa 100%.
-Barabara,umeme,treni hata wakoloni waliweka........JPM anafanya hiyo miradi coz anapiga cha juu na si kama anataka kuleta maendeleo ya vitu.
Na kwa ukondoo wa wabongo, hawezi hata kuulizwa kwa nini kazuia CAG asikague mahesabu ya ATCL ? Kwa nini ananunua midege kwa cash? Kwa nini hafuati tender process wala budget?

Hapo pote pana alama za upigaji.

Lakini wananchi wengi washaleweshwa pombe ya Pombe, hawaelewi kitu.
 
Acha ushabiki usikuwa na Tija...embu vaa viatu vya magufuli unasikia watu ulikuwa nao karibu wanakuzungumzia vile utajisikiaje..wanakutukana na kukusengenya uku ukikutana nao wanajionesha ni watu wazuri kwako
Magufuli mwenyewe ndiye kajitakia kuongeleea alivyoongelewa.

Wewe rais gani anasema atapiga mpaka shangazi za wapinzani wake? Huyo rais au kichaa?

Na pia, kudukua maongezi ya faragha ya watu bila amri ya mahakama ni kinyume na katiba ya Tanzania.
 
Na kwa ukondoo wa wabongo, hawezi hata kuulizwa kwa nini kazuia CAG asikague mahesabu ya ATCL ? Kwa nini ananunua midege kwa cash? Kwa nini hafuati tender process wala budget?

Hapo pote pana alama za upigaji.

Lakini wananchi wengi washaleweshwa pombe ya Pombe, hawaelewi kitu.
Kabisa mkuu 100% JPM anapiga cha juu ndio maana hataki kukaguliwa, hataki wabunge wahoji ,amezuia mafao NSSF/PPF ili apige hela kwa kufanya mambo ya kipuuzi(kununua midege ambayo haina faida yeyote) sasa ameanzisha biashara ya afya(BIMA) kupitia NHIF anakusanya fedha kisha anaenda kujenge white elephants projects huko kwao CHATTLE.
 
Raisi Magufuli aliwasamehe,wale waliokuja kwake kuomba msamaha.
Walikiri kutenda kosa bila kushurutishwa nae akawasamehe kwa roho safi.
Lakini yawezekana pia Magufuli kama kiongozi mkuu namba mmoja hakujua kuwa kilitukanwa kiti cha mamlaka, na mamlaka ndizo zilitakiwa kushughulikia hilo jambo kwanza.
Kwa upande mwingine tena bahati mbaya zaidi watuhumiwa ni vigogo kwenye halmashauri kuu ya chama hicho anachoongoza Mweyekiti Magufuli.
Ni wazi kabisa kamati husika ya maadili itajiridhisha kwanza ili ifunge file. Ni utaratibu tu wala sio mpasuko ndani ya chama.
 
Unajua kusoma? Kwa ufahamu?

Nilichoandika mimi na unachonikashifu kuandika ni vitu viwili tofauti.

Unaelewa hilo?

Unataka tujadili neno kwa neno?

Do you understand that a protest against Lese Majeste is not necessarily an act to incite the populace to trash the national leadership?

Unaelewa kwamba nikitetea haki yako ya kupiga kura, hilo halimaanishi kwamba nakushurutisha wala nakutaka upige kura?
Unavyojitahidi kukwepa hoja yako wakati uliileta mwenyewe, inadhihirisha wazi kuwa hata we mwenyewe unaona kabisa matusi sio jambo jema.

Wakubwa tunaelewana. Umechutama.
 
Back
Top Bottom