kinachoiangamiza Bongo Muvi sio suala la mauzo pekee...wajiulize mbona hata umaarufu wa Wasanii wa Muvi umekwisha kwa muda mrefu sasa...Hakuna wasanii wapya wanaoibuka, zaidi ya kubaki na wale wale wa tangu miaka zaidi ya kumi iliyopita ukilinganisha na wenzao wa Bongo flavour, Majina ni yale yale JB, Ray, Aunty, Wolper, Rose Ndauka, Uwoya n.k.
Na kama hizo kazi zingekuwa zinasambaa kwa njia ya uharamia kama anavyojaribu 'kutujaza' Dr Cheni basi bado tungeona Wasanii wengi wapya wanaibuka na umaarufu wa Bongo muvi ungebakia kama sio kuongezeka...labda ambacho mngekosa ni pesa tu.
Hata Wasanii wa Bongo flavour hawauzi CD, lakini kwa nyimbo zao kuchezwa hovyo na kuchomwa hovyo mitaani ndio tunashuhudia kuibuka kwa Wasanii wapya kila siku.
Kilichoiua bongo Muvi ni ubinafsi ulioendekezwa na hao hao wanaojiita 'Waanzilishi' wa Bongo muvi....wao baada tu ya kuona Watanzania wamewapokea vizuri wao wakajifungia kwenye chumba chao kama Wasanii na kuamini kwamba sasa ndio wakati wa kuchuma mihela..walisahau kabisa kwamba sanaa ya filamu ni matokeo ya team work, kwa maana ya Wapiga picha, Waandishi, Waongozaji n.k ndio maana mlishuhudia kina Ray wakijipa majukumu yote ya kuandaa filamu, muandishi yeye, Cameraman yeye, Muigizaji yeye, na wenzake walifuata mkumbo huo huo.....Wao waliamini kuwa Wasanii wangeweza kusafiri kivyao na kufaidi mihela ya Watanzania milele.
Wana kazi kubwa ya kurudisha imani ya Watanzania tena kwani sio kazi rahisi sana...kuna usemi maarufu kuwa 'bahati huwa haiji mara mbili' ila upo uwezekano wa kurudi tena iwapo tu watakaa chini na kutaka kujifunza Filamu ni nini..
.....Sanaa ya Filamu/burudani huwa haifi, bali husinzia au kuwa kwenye coma hata kwa miaka mia moja iwapo kutakosekana ubunifu na uelewa, mpaka hapo watakapojitokeza watu sahihi wa kuirudishia uhai.