Dr. Cheni aeleza sababu za kutojihusisha tena na filamu nchini

Dr. Cheni aeleza sababu za kutojihusisha tena na filamu nchini

kinachoiangamiza Bongo Muvi sio suala la mauzo pekee...wajiulize mbona hata umaarufu wa Wasanii wa Muvi umekwisha kwa muda mrefu sasa...Hakuna wasanii wapya wanaoibuka, zaidi ya kubaki na wale wale wa tangu miaka zaidi ya kumi iliyopita ukilinganisha na wenzao wa Bongo flavour, Majina ni yale yale JB, Ray, Aunty, Wolper, Rose Ndauka, Uwoya n.k.

Na kama hizo kazi zingekuwa zinasambaa kwa njia ya uharamia kama anavyojaribu 'kutujaza' Dr Cheni basi bado tungeona Wasanii wengi wapya wanaibuka na umaarufu wa Bongo muvi ungebakia kama sio kuongezeka...labda ambacho mngekosa ni pesa tu.

Hata Wasanii wa Bongo flavour hawauzi CD, lakini kwa nyimbo zao kuchezwa hovyo na kuchomwa hovyo mitaani ndio tunashuhudia kuibuka kwa Wasanii wapya kila siku.

Kilichoiua bongo Muvi ni ubinafsi ulioendekezwa na hao hao wanaojiita 'Waanzilishi' wa Bongo muvi....wao baada tu ya kuona Watanzania wamewapokea vizuri wao wakajifungia kwenye chumba chao kama Wasanii na kuamini kwamba sasa ndio wakati wa kuchuma mihela..walisahau kabisa kwamba sanaa ya filamu ni matokeo ya team work, kwa maana ya Wapiga picha, Waandishi, Waongozaji n.k ndio maana mlishuhudia kina Ray wakijipa majukumu yote ya kuandaa filamu, muandishi yeye, Cameraman yeye, Muigizaji yeye, na wenzake walifuata mkumbo huo huo.....Wao waliamini kuwa Wasanii wangeweza kusafiri kivyao na kufaidi mihela ya Watanzania milele.

Wana kazi kubwa ya kurudisha imani ya Watanzania tena kwani sio kazi rahisi sana...kuna usemi maarufu kuwa 'bahati huwa haiji mara mbili' ila upo uwezekano wa kurudi tena iwapo tu watakaa chini na kutaka kujifunza Filamu ni nini..

.....Sanaa ya Filamu/burudani huwa haifi, bali husinzia au kuwa kwenye coma hata kwa miaka mia moja iwapo kutakosekana ubunifu na uelewa, mpaka hapo watakapojitokeza watu sahihi wa kuirudishia uhai.
umesema kila kitu mkuu.
 
Bongo movies sijui bongo flavor ni wakuupuzwa tuu hamjitambui ndio maana mnatumiwa kama toilet paper
 
Na ikifika wakati wa uchaguzi wanazunguka na ccm nchi nzima,,pumbavu sana na sanaa itawalipa mtakapo pata akili.
 
Hebu tuache mboyoyo...kuna uhusiano gani kati ya kudorora soko na kushiriki kampeni za chama?

Basi na mhusianishe mafanikio ya Diamond na kampeni...maana naye si alishiriki?

Nadhani mmekosa tu cha kushauri na sasa mnatafuta njia ya mkato.

Hao Wasanii waliounga mkono upinzani ni wangapi sasa wanakula matunda ya mafanikio kutokana na kufanya hivyo?
Pole kada naona imekuuma
 
Acheni utani, hivi niache kuangalia 24 niangalie movie ya cheni sijui..
 
Tumehamia kwenye series hata bongo movie za buku buku sichukuiii
 
Bongo movie na wanamuziki mlijifanya mna akili sana, mlitumika kuwapa maujiko ccm mwaka jana kwahiyo tutaendelea kununua kazi bandia hadi mtakaposhtuka.
 
Pole kada naona imekuuma
Kwa kuwa Bavicha mna vipaji vya kuporomosha mitusi basi mmegeuza huu uzi ni wa kutoa mapovu yenu...ila kwa mtu mwenye kufikiri hamna hoja yoyote mnayoitoa yenye maana.

Hata Chibu angebuma mngeongea haya haya...ameshiriki kampeni, amevaa jezi za Chama pendwa na bado anawakalisha.

Video yake sasa hivi You tube inaenda view 7.5m, anavunja rekodi aliyoiweka yeye mwenyewe...hao wenu waliovaa kama Migambo kwenye kampeni zenu wako wapi? wengine ndio kwanza wanawatoroka na kurudi Chama Dume.

Chibu anasapoti Chama number one na yeye ni msanii number one...mmechooooka hamna hamu...mnapambana kila kukicha kutengeneza mpinzani wake lakini wapi.

Hata Fiesta ingebuma mngejazana humu kuinanga Clouds...lakini wapi jamaa wamewaziba midomo...mlisubiri kwa hamu kama Fisi anayevizia mkono wa Binadamu uanguke.

Kitakachowanufaisha hawa Wasanii ni kazi nzuri tu na sio huu utumbo mnaojaza humu kwenye uzi...hizi hoja zenu ni mufilisi.
 
Back
Top Bottom