Bumbuli saccos ni kina nani? hii nchi kila mfanya kazi wa umma mwenye kacheo kidogo ni mwizi sijui ni kwa nini? kikwete aliizinisha wizi nchini kama kazi ya kujipatia kipato kwa wafanyakazi wa umma. Na nchi hii Tanzania wasomi ndo wanaliangamiza Taifa, hawako pale kusaidia Taifa wako pale kuiba tu,wasomi wanatakiwa wajue kuwa ukitaka pesa za haraka na nyingi ni kufanya biashara sio kuiwaibia watanzania, binafsi naona katika nchi za Afrika mashariki Tanzania tunaongoza kwa ufisadi kwa sasa, maana kila sehemu ni wizi wizi tu,sio wanasiasa, sio watumishi wa umma , imefikia wakati serikali itoe adhabu kali kwa hawa mafisadi, ikibidi tuanze kuwanyoga ,tutoe adhabu kali ili liwe fundisho kwa kizazi hiki na kichajo, lasivyo watu hawataongopa rushwa, watachukulia ni swala la kawaida ,watu wanaiba wanatumia hizo pesa kwenda mahakamani kuendesha kesi na wanashinda. Ifike mahali hata maafisa wa Takururu/DPP waanze kuchunguzwa na kupewa adhabu kali wanaposhindwa kesi hizi za ufisadi. Huu mchezo wa kuwasimamisha au kuwafukuza kazi bila kufunga au kunyonga watu hatuwezi kufika, hakuna mtu atakae ogopa rushwa kwa mchezo huu tunaocheza kwa sasa.