Dr. Diallo: Katiba inatengenezwa na Wananchi siyo Wanasiasa, 2014 tuliikosa katiba mpya kwa ubinafsi wa wanasiasa CCM ikiwemo!

Design ya Iddi Amin, alikua anakuchekea na dakika tano mbele mood inabadilika. Wataalam wanaotaka hali hiyo schizophrenia
 
Nimekuwa nahubiri hiyo ambapo conflict of interest lazima iangaliwe. Njia ya kufanya ni kubadili kwanza sheria na kuhakikisha yeyote atakayehusika na katiba mpya asigombee kwa muda wa miaka 20. Hapo tutapata katiba konki.
 
Mpaka kadamu kamwagikepo ndio katiba ipatikanepo
Samaki mkunje angalia mucho, akikauka ukimkunja atavunjika, hivyo njia nyingine rahisi ni "kumloweka" ili Madhara ya kuvunjika yasiwe mabaya sana. Kwa wahunzi wanasema kikunje chuma kikiwa cha moto kinakuwa kama uji uni.

Sasa kama nchi sijui kama huyu samaki bado mbichi au ameisha kauka au kwa lugha ya wahunzi sijui hichi chuma mpaka kiwe cha moto ndio tukikunje au kipo katika hali ya kukunjwa
 
Nimefatilia interview ya Diallo, inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii akiishutumu serikali ya JPM, serikali iliyopambana kwa ajili ya wananchi. Naenda kujibu hoja zake kwa niaba ya JPM. Rais ambaye ntampigania mpaka kufa...
Jinyonge au kaombe interview startv
 
CCM ni chama cha kishetani kabisa, mwaka 2015 kikatuletea mgombea mwenye matatizo makubwa ya kiakili na ugonjwa mbaya wa moyo ambao wataalamu walishasema huufai kwa kiongozi mkubwa wa nchi kuwa nao (maana itabidi awe anazurula na hospitali inayotembea kila atakapokuwepo maisha yake yote) na bado kikalazimisha awe rais 2015 na 2020 pamoja na wananchi walio wengi kumkataa. Na bado CCM ikajipanga kubadilisha katiba ili atawale milele.

Asante kwa Covid, pamoja na kuitesa dunia, lakini kuna jambo jema moja kwa watanzania imelifanya. Covid iliweza kumzima Dikteta kimya kimya.
 
Arudi kusoma vitabu vya Civics topic ya direct and indirect democracy!
View attachment 1847692
Mbona ameeleweka sana kwamba hao representative wanaangalia maslahi yao sasa wewe hapo kigumu kukielewa nini nini . Je katika kuzisoma hizo njia, ulijifunza uzuri wake na ubaya wake? Sasa katika ubaya wake ulielewa nini???
 
Mara tu baada ya uchuguzi ghushi wa 2015 wapinzani kwa maana ya CHADEMA wakaanza kushughulikiwa vilivyo na mtesi mkuu aliyeapa kuifuta CHADEMA kwenye ramani ya siasa za Tanzania ifikapo 2020...
Your browser is not able to display this video.
 

Dhalimu alikuwa ni mpika data fullstop.
 
Diallo ametema nyongo ya madhila tuliyopata katika awamu ya Magufuli! Amesema kamwe tusije rudia kuchagua mtu ambaye hatuna historia yake...
Mbona hajasema alivyo nyanyaswa na Severe Mkurugenzi wa Utalii , wakati Yeye ni Naibu waziri wa Utalii, na EL ndio waziri mkuu. N.a. haya yanawezeshwa na katiba mbovu ambayo ina dekeza upendeleo
 
Na amesema tulikuwa na kiongozi mwenye matatizo ya akili. Hivyo tusirudie tena kupata viongozi wa aina ile. Anasema huyo jamaa alikuwa ni mlevi wa madaraka.
Kwakuwa sahara midia ilifungwa kwa kutolipa madeni ya zaidi ya bilion. Halafu shujaa akamlazimisha kulipa fedha ilikujenga miundombinu ya maendeleo ya watanzania. Kumbe utawala ulikua mbovu kwa namna hiiiii??
 
Pumbavuuuuuuuu
 
Na amesema tulikuwa na kiongozi mwenye matatizo ya akili. Hivyo tusirudie tena kupata viongozi wa aina ile. Anasema huyo jamaa alikuwa ni mlevi wa madaraka.
Naiona Katiba Mpya ileee inakaribia.
 
Huyu mwenye legacy ya sanamu la shaba kawaachia nini watanzania cha kujivunia?
Vingi mnoo ni nyie wapumbavu wachache mliovaa miwani ya mbao na kutia pamba masikioni ila soon muda haujulikani ni saa ngapi usipoongea wewe ata mawe yatasema uzuri na mema ya magufuli
 
Tuseme kama Bwana Diallo angekingiwa kifua na Raisi Magufuli kukwepa kulipa kodi labda asingesema yote haya.
Bwana Diallo ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza naona amejilipua kichama au amezaliwa upya kifikra.
Huko nyuma Horace Kolimba aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM alienda mbele zaidi kudai CCM imekosa muelekeo lakini hata alivyoitwa Dodoma kujieleza mbele ya kamati,akiwepo Mwalimu Nyerere, kilichotokea hakikubadirisha CCM.
Raisi Jakaya Kikwete alipoamua kutupa katiba mpya na kumteua Jaji Sinde Warioba aongoze mchakato wa rasmi ya katiba.
Lakini baadae CCM ilingamua kuwa wangeweza wakapoteza madaraka,ndipo wakapiga about urn.
Tuseme tu,CCM ina wenyewe, na wale wenyewe hawapo tiyari kukabidhi madaraka kwa wapinzani,kwa yeyote ndani ya chama anaenda kinyume na hilo anaesabika ni msaliti. Haijalishi ni Mwenyekiti wa Chama wa taifa au Mwenyekiti wa Chama wa mkoa.
 
Nimekuwa nahubiri hiyo ambapo conflict of interest lazima iangaliwe. Njia ya kufanya ni kubadili kwanza sheria na kuhakikisha yeyote atakayehusika na katiba mpya asigombee kwa muda wa miaka 20. Hapo tutapata katiba konki.
Ndio inavyotakiwa kufanyika ili kupata katiba imara. Yaani mtu ukikubali kuwa mjumbe wa tume, kamati au taasisi yoyote ya mchakato wa katiba mpya unapaswa kutengwa kabisa kimadaraka yoyote ya nchi, iwe kuchaguliwa au kuteuliwa kwa miongo kadhaa ili kuondoa conflict interest.

Hilo halikufanyika kipindi kile cha katiba la Warioba, lilikuwa ni kosa kubwa mnoo.
 
Afadhali angalau umepatikana mmoja mwenye ufahamu si hawa akina Erythrocyte kupiga madebe katiba bila kuona hatari inayotukabili. Angalau ile ya Warioba ilikuwa na uhai kuliko draft ya JK na mifisadi myenzake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…