Dr. Diallo: Katiba inatengenezwa na Wananchi siyo Wanasiasa, 2014 tuliikosa katiba mpya kwa ubinafsi wa wanasiasa CCM ikiwemo!

Yani kumkomalia mtu alipe kodi hiyo ni siasa chafu!!!! Hivi hii nchi tunaenda wapi.leo hii tunafurahi kupokea misaada kutoka ulaya tokana na raia wao kulipa kodi kisawasawa sisi huku tukiomba kodi tunasema ni siasa chafu
 
Nimefatilia interview ya Diallo, inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii akiishutumu serikali ya JPM, serikali iliyopambana kwa ajili ya wananchi. Naenda kujibu hoja zake kwa niaba ya JPM. Rais ambaye ntampigania mpaka kufa...
Dialo mdaiwa sugu na wafanya kazi wake vip alisha mlipa marehemu Fred waaah au kamuachia zigo?
 
hhahaaa wameanza kumkana mwenzao wazi wazi
 
Diallo yuko sahihi sana. Katiba inatakiwa kutengenezwa na Wananchi, wataalamu. Ili tuwape wanasiasa kuitumia.
 
Alishazoea zile dezo alizokua anazipata tawala zilizopita za kukwepa kodi na misamaha isiyo na maana.
 
Bibi aliwahi kusema, moyo wa mtu ni msitu mnene. Mioyo ya watu ina mengi, kadiri ya fursa zinazojitokeza, yatawekwa hadharani. Ni suala la muda tu, huyu kaanza kwa sbb ya fursa aliyonayo kumiliki media, wako wengi wenye mengi kama yeye, nao wakipata fursa tutayasikia mengi. Mzee Lembeli kule kahama alipokosa ubunge alisema "upepo ukivuma, sharti nyeti za kuku zifunuke"
 
Haya Sasa MATAGA mnasikia?
Kama huyo kada aliyekua mstari wa mbele kimchango kwenye chama chenu chakavu anatema nyongo hivyo na kusema mtu pori toka chattle
Alikua na file Milembe

Wewe ni nani upinge tulikua tukiwaambia jiwe ni laana na anatumbukiza nchi shimoni mlikua mnabweka Kwa kutuita vibaraka wa mabeberu Leo Kiko wapi?
 
Kumbuka aliyetangaza matokeo ni Ndugai ambaye anafahamika kuwa bingwa wa kutangaza kura fake. Kura zilizo tangazwa hazikuwa halisi!
 
Mbona hajasema alivyo nyanyaswa na Severe Mkurugenzi wa Utalii , wakati Yeye ni Naibu waziri wa Utalii, na EL ndio waziri mkuu. N.a. haya yanawezeshwa na katiba mbovu ambayo ina dekeza upendeleo
Mjadala ulikuwa unahusu utawala wa awamu ya Magufuli!
 
Yaani unaongelea ajira upande wa sector moja tu ya construction ambayo nayo ilikuwa almost kwa suma JKT

Watu wanaongelea multiplayer economic activities!

Mtu anachota pesa kenye account za watu kwa nguvu na kuhamisha unasema alikuwa anakuza uchumi?

Kwanza nikukumbusha hakukuwa tena na data za kweli za uchumi toka BOT, NBS wala taasisi za serikali kama ATCL na wengine

Aisee ebu acheni ujinga basi ukweli umewekwa wazi na rais Uchumi ulianguka sasa wewe bado umuamini Rais aliyepo madarakani amabaye anasema uchumi ulidondoka?
 
Kila binadamu ana side A na B.
Kila kiongozi ana side A na B.
Side A ikiwa mazuri side B yanakuwa mabaya yake au kinyume chake.
Unaweza kuwa na mlolongo mkubwa wa matukio side A ambayo ni ya kawaida.
Lakini ukawa na matukio machache ya side B ambayo ni ya ajabu na kutisha.
Ukimgawia mtu chakula, nguo na kumlipia binti yake ada na nauli ya kwenda shule (side A);
Kisha mwaka wa pili ukampa mimba binti huyo (side B);
Unategemea mzazi akumbuke chakula, nguo, ada na nauli wakati kuna moja kubwa la ubakaji lilozaa mimba kwa binti yake?
Katika maisha ya kawaida au katika uongozi jitahidi uzito wa maovu yako usizidi uzito wa mema. Kinachogomba ni uzito siyo idadi.
 
Mjadala ulikuwa unahusu utawala wa awamu ya Magufuli!
Sio katiba yenye mapungufu ambayo inaweza kutumika vibaya ?? Au kwake katiba inakuwa mbovu inapomnyima kula yeye , ikiwanyima wengine ni sawa.
Na papo hapo kasema usimpe mwana siasa nafasi hiyo ni wa binafsi.
Kwa hiyo katika kutafakari jambo hilo unatakiwa kuchukua akili za kuambiwa changanya na zako
 
Kwakuwa sahara midia ilifungwa kwa kutolipa madeni ya zaidi ya bilion. Halafu shujaa akamlazimisha kulipa fedha ilikujenga miundombinu ya maendeleo ya watanzania. Kumbe utawala ulikua mbovu kwa namna hiiiii??
Maendeleo ya uwanja wa ndege chattle.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…