hata mimi naamini hivyo hivyo, Dr Dre ndio kazingua, kwa sababu mbili:
moja, mwanamke alipoomba divorce alitaja masaibu ya ndoa yake ikiwemo matusi na kuwekewa pistol kichwani mara mbili.... Dr. Dre akajitetea mahakamani kwamba mbona hata siku moja mke hakusema kwa polisi, mama yake, dada zake, social media au popote kwamba anasulubiwa ndani ya ndoa ?
ambacho kimenifunza kitu kimoja, hii conventional wisdom ya kusema tutunze matatizo yetu ndani kwa ndani kuna siku utaambiwa we muongo, kwa nini hukusema hata kwa dada yako kwamba kunawaka moto humo ndani
na pili, mtu yeyote ambae anafurahi ndoa ikivunjika most likely yeye ndio alikuwa tatizo manake hakumaanisha kuishi ndani ya ndoa milele
Nimepoteza heshima yote kwa Dr Dre, nilidhani ame move past his NWA bravado. Mtu mzima unaandikaje bango la DIVORCED AS F@CK ?