Nimesoma uchambuzi alio wahi kuufamya Ndg. J.Mtatiro kuhusu Magufuli. Kuna baadhi ya aya amejaribu kufananisha misimamo ya Mwalimu John Magufuri na ile ya Mwalimu Nyerere kwamba wote wanasifa ya kutoyumbishwa katika misimamo yao. Japo ki ukweli nina mashaka na Magufuri, lakini wengi tunajua kuwa yeye ndiye Rais ajaye hata tufanyeje. Na pia anauwezo wa kukiuza chama chake na kupata wabunge wa kutosha kuunda balaza lake la mawaziri. Rais peke yake hatoshi bila kuwa na balaza thabiti la mawaziri. Je, atakuwa na uwezo wa kuwakemea mawaziri wake pindi uzembe utakapo tokea kama alivyofanya Mwalimu mwenzie Nyerere? UJue Mwalimu wa ngazi yoyote ile anasifa ya kukemea na uso wake uonekane kweli kuwa amekemea na anachukia kilichotendeka na hataki kitokee tena si kwa aliyekitenda lakini pia na kwa wengine pia. Je, mwalimu Magufuri atafanya hayo au na yeye ataishia kuwafukuza waliovurunda na kuiba wakale kwa amani? kwa taifa lilipofikia linahitaji Rais mkali kabisa asiyetayari kucheka na wazembe. Nakutakia kila la kheri Mwalimu Magufuri lakini katika safari yako jifunze kutafakari kwanza kwa kina kabla ya kutoa maamuzi ya haraka haraka!