Elections 2015 Dr. John Pombe Magufuli achaguliwa kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM 2015

Elections 2015 Dr. John Pombe Magufuli achaguliwa kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM 2015

Kwa kuwa magufuli atakuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM, napendekeza mgombea mwenza awe Amina Salum ili kubalance bara na visiwani, na pia suala la ukristo na uislamu. Alafu Lowasa awe waziri mkuu. Ukizingatia, Magufuli amebebwa na kura za Lowasa baada ya team Lowasa kumpigia Magufuli kama namna ya kumkomoa Membe.

Mnaonaje wadau huu mchanganuo? Karibuni tujadili

Hii imekaa poa

Watajibeba hii nchi mwaka huu ccm hairudi amin hivyo .
 
Kwa kuwa magufuli atakuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM, napendekeza mgombea mwenza awe Amina Salum ili kubalance bara na visiwani, na pia suala la ukristo na uislamu. Alafu Lowasa awe waziri mkuu. Ukizingatia, Magufuli amebebwa na kura za Lowasa baada ya team Lowasa kumpigia Magufuli kama namna ya kumkomoa Membe.

Mnaonaje wadau huu mchanganuo? Karibuni tujadili

Vip Mzee wa mkasi (Dr. Bilali)?
 
Mimi siyo ccm na wala sitarajii kuwapa kura yangu. Lakini Waziri mkuu awe mwakyembe
 
tutakukumbuka kikwete kwa kuliacha taifa letu kwa mtu sahihi,
 
Flag bearer of Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye uchaguzi mkuu wa Tanzania kuwania kiti cha uraisi tarehe 25 October 2015

Dr. John Pombe Joseph Magufuli
Amezaliwa - 29 October 1959
Constituent: Chato
Current -Minister of Works

Kazi yake kubwa sasa ni kuwania kiti cha uraisi mwaka 2015

Mungu awe nae.

Karibuni kumfurahia, kumpa ushauri na mengineyo ili apae na kupaaView attachment 267559

Nina Matarajio Makubwa Sana Nae Na Namwomba Tu Asituangushe SISI TULIOKUBALI KUTUKANWA, KUDHIHIHAKIWA, KUKEJELIWA Na KUDHARAULIWA Juu Yake Lakini Bado TUKAWA HATUJAKATA Tamaa Dhidi Yake Na Binafsi NIMEATHIRIKA Mno Na Kumuunga Kwangu Mkono Dr. Magufuli ILA Sitaki FADHILA YOYOTE Kwake Zaidi Ya KUMTAKA Rais Wetu Ajaye ATUTOE WATANZANIA Hapa Tulipo Na Atupeleke Katika Mafanikio Na Nchi Yetu IPAMBANE Na MATATIZO Makubwa Ya UMASIKINI, MAGONJWA, MIUNDO MBINU, UDINI Na UKABILA Na KIKUBWA Rais Wetu Ajaye Dr. John Pombe Magufuli AFANYE KILA AWEZALO Na ATUUNGANISHE WATANZANIA Na Namshauri Avae Viatu Vya WATANGULIZI Wake Wote ILA AFUATE Miiko Ya Chama Cha Mapinduzi Kuwa Ni Chama Cha WAKULIMA Na WAFANYAKAZI Na Nitazidi Kumuombea Kwa Mwenyezi Mungu AONGOZE Kwa MAFANIKIO. Nina Furaha ILIYO Ya Ajabu Na Nasubiri Tu Kuvuliwa KOFIA Na Kupigiwa SALUTE Na Wale Wote Waliokuwa WAKINIBEZA Humu. NIMEFANIKIWA KULIKOTUKUKA Kwa 100% Na USHINDI Wa Dr. Magufuli UMEKUWA NI FIMBO Yangu NZURI Kwa Wale Wote WALIOKUWA WAKINIPUUZA, Akhsante Magufuli.
 
Huo ndo ukweli.....Kamwe hawezi kua bora kwa kua zao la kiwanda chakavu,kinachoongoza kuzalisha bidhaaa feki kila wakati.Tutakua waajabu wateja kukiamini kiwanda hiki,kuwa sasa kinazalisha bidhaa bora.Ndio!!!!!! ni kiwanda kile kile miaka hamsini imepita,Kilipendwa hapo mwanzo kwa bidhaa zake.Wateja tulijitokeza kwa wingi hata kununua na kusikiliza matangazo ya bidhaa zake.Leo hii hatuendi mpaka kitoe magari yatubebe na hata chakula tuleee pia.....Ndo hicho hicho,bidhaa feki kila kukicha.MABEHEWA FEKI,BOAT YA BAGAMOYO FEKI,NDEGE YA RAISI FEKI,RADA YA JESHI FEKI ,BALA BALA FEKI,MAJENGO FEKI NA MIKATABA FEKI ni baadhi ya bidhaa zake.

Jina la kiwanda halikuwahi kubadilika,nembo yake na hata kanuni zake.Huwezi kua bora Dr kwa kuzalishwa na kiwanda chakavu.Fungeni mkikalabati kiwanda chenu na hata mkibadilishe jina na majengo.Itasaidia wateja kuziamini bidhaa zake tena.Huwezi kuwa bora kamwe,watu wanataka kiwanda kipya na bidhaa mpya.Wako tayari kutojari radha,upya utasaidia.


Hakika huwezi kuwa bora
 
Ni tunaotaka kumuongelea uteam ni ushabiki au kumkubali

Amefurahisha wengi hasa jana alipotoa speech yake.

Nani huyo? Pombe? Akiwa Rais atakuwa anaendeshwa na pombe kichwani..
 
Magufuli ni kiongozi bora lakini siwez kuharibu kura yangu kuipigia CCM..... hell no
 
... Ngoja Tutafte Kashfa Za Magufuli, Tulitegemea Lowasa Awe Mgombea Sasa Tumepigwa Chenga Ya Mwili.!
 
Kwa wengi imekuja kama suprise, kwa wengi imekuja kama taarifa ambayo still hawaiamini na bado wanashindwa kuelewa kama ni wanaota au wako macho.
Ila ni kweli, ni uhalisia kuwa CCM wameamua kutupa John Pombe Magufuli kuwa mgombea wao na inshalah Mungu mkubwa ndo atakuwa raisi wa awamu ya 5 ya Jamuhuri yetu pendwa.
Kwa ma critical analyist mlio humu wengi tulilidiscuss hili kwamba kwa nchi ilipofika hapa tunaitaji nani? Tunaitaji raisi wa namna gani?? Na wote ingawa tulitofautiana kidogo kwa watu ila tulikuwa kwenye kundi moja yani Magufuli, Muhongo, Mwigulu na wengine walikuja na option ya Makongoro. Ila kikubwa tulikuwa tunacheza sehemu moja.

Mimi mmoja wapo niliandika thread mbalimbali ya kwanza nikasema CCM ichague kati ya Muhongo na Makamba(ingawa nilimtoa Makamba kwa kuwa hakuwa na hiki kigezo cha a wise dictator alichoprove kwenye utendaji wake). Niliandika thread nyingine nikasema kama system ilikuwa inamtaka Jaji Agusto Ramadhani basi ilikuwa imekosea kutokana na kuwa kwa nchi yetu ilipofika inaitaji a wise dictator kipengele ambacho muadilifu Ramadhani alikuwa amekikosa, kwenye ile thread nilisema inabidi waamue kati ya Muhongo na Magufuli kwenye michango niliyoitoa mle.
Kuna watu waliniunga mkono akiwemo GENTAMYCINE, KANONE, RWEYE, PASCO na wengine wengi siwezi kuwamention wote.

Kulikuwa na watu wachache sana humu walioweza kuelewa point yetu sie tuliosimama huku tukiwa hatulipwi, hatuhongwi wala hatuna maslahi ya vyeo vyovyote vile kwa hawa watu.
Nilisema wazi kuwa nchi hii ina shida kubwa ya wizi, siasa kila kona, uvivu, porojo porojo, watu kutopenda kujishughulisha na kutolipa kodi na siasa za fitna chuki bila kusahau ushirikina. Nilisema juu ya syndicate kubwa iliyojijenga na kuuyumbisha sana utawala wa kikwete ikiongozwa na Media tycoon fulani akiwa supported na wanasiasa fulani ivi ambao wameiyumbisha sana serikali na hata kuifanya ishindwe kuperform vizuri kutokana na maslahi yake binafsi.

Nilisema wazi kuwa hakuna mtu atakayeweza kushindana na hivi vitu kama huyo mtu sio wise dictator na nilisema wise dictator ni mmoja kati ya hawa watu Magufuli na Muhongo. Nilielezea pia juu ya wagombea wawili EL na BM ambao walikuwa wamejijenga sana kuanzia kwenye system na nje ya system ili waweze kuloby na kupitishwa mmoja wapo na nilisema ikiwa mmoja kati ya hawa atapita nchi itapita kwenye kipindi kigumu sana ambacho watu hawajawai kukiona nacho ni kipindi cha visasi, wizi wa maliasili za taifa ikiwamo gesi na madini kutokana na hizi kambi mbili kuwa supported kwa kiwango kikubwa na wafanyabiashara ma opportunist. Na hili lilidhihirika tu pale mmoja wa hawa watu kukatwa na mwingine kubakishwa yaani kwa masaa machache sana chama chao kilipata wakati mgumu hakijapata kuu experience hadi walipoamua kuwatosa wote.

Na jana nilisema humu kuwa kosa kubwa walilolifanya ni kumuacha mmoja yaani BM na kumkata mmoja na nilisema jana kuwa suluhisho la ile tension ya jana ni kumkata na kumtoa pia BM na ilionekana kuwa nae alipokatwa tu mambo yakatulia na wakaweza kuendelea.

Sasa ndugu zangu tumeshampata a wise dictator ambaye atakuja kuitoa hii nchi kwenye hizi challenges na kitu kikubwa kilichopo hapa ni kumuweka mikononi mwa Mungu huyu mtu John Pombe Magufuli ili aweze kumtumia vizuri kuibadirisha hii nchi yetu. Kikubwa kingine ni kuwa tuzidi kumuomba Mungu amchague Waziri Mkuu strong kama yeye yaani hapa kwangu mimi napendekeza Prof Sospeter Muhongo ili waweze kuwa na kasi ya pamoja kwenye kuifikia ile Tanzania tunayoitaka.

Namaliza kwa kusema the best combination ambayo hii nchi itapata na itakuja kuikumbuka hadi mwisho wa hii dunia ni Dr John Pombe Magufuli as the president and Prof Sospeter Muhongo as the Prime Minister.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Back
Top Bottom