Elections 2015 Dr. John Pombe Magufuli achaguliwa kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM 2015

Me nawaambia wa Tanzania amin bado xana kwa mfumo wa ccm akuna rais mpya labda wangemuacha tu lowasa maana yeye kaiba mpka bas ila huyu magufuli kuwa rais ni haeri mkolon angerud mcbweteke na lami na madaraja feki jiulizen wap aliwai kemea ubadhilifu wa Mali za umma utaona apo mwenyewe kwamba ni lazma akae kimya ndo xababu kachaguliwa ila me c mchukii tuamke kma Kenya ndo kilichobaki kma ni Ukawa nao ni wakati wa kuwapima je wanayosema ni kweli bhasiii.
 
CCM itashinda kote kote. Imeshinda kwenye serikali za mitaa haitashindwa kwenye uchaguzi Mkuu
 
Kura za kanda ya ziwa pekee zinatosha kumpa ushindi magufuli, nawajua wale jamaa zangu wa kina ngosha lazima wampe magufuli tu
 
Bahati nzuri ni sisi Wananchi ndio tunamchagua Rais. Na tuna imani na magufuli. Slaa anadhani mamlaka ya Rais ni mepesi kama kupora wake za watu?

kama ilivyo kwa magufuli kumjaza mimba mwanafunzi wa Geology pale UDSM...Itafahamika tu mwaka huu
 
SLAA anajua Maghufuli ni jembe na ndiyo maana ameomba asitangazwe kuwa mgombea wa UKAWA kwenye kkkao cha juzi na kuomba apewe muda atafakari kwanza.
Kweli kabisa Mkuu. Slaa anatamani tumkutaka kugombea kwa vile anapata ruzuku ya mberere na chama chake
 
Hawez kupambana na mfumo uliomfikisha hapo alipo, ndio mzizi wa matatzo yetu tz.... kwahiyo hyo ni epson nyngne tu lkn season tunayochek ni ileile.....
sijui inaitwaje hii season???
Tutumie ujinga wao kujinufaisha..may b
 

Hizo Ni Porojo Tu Za Kutaka Kulichafua Ili Jembe.Husichanganye Mabarabara Za Magufuli Na Hizo Zenu Zilizojengwa Na Manispaa.Ebu Tembea Ujionee Jinsi Hili Jembe Lilivyotandaza Mikeka Nchi Nzima.
Magufuli Sio Mwanasisa Ni Mchapakazi.Huwezi Kumfananisha Na Mwanasiasa Yeyote Katika Ukawa Yetu.Huyo Dk.Silaa(Mswati) Tunaepanga Kumsimamisha Kama Mgombe Wetu.Uongozi Tu Wa Jimbo(Padre) Ulimshinda Na Hata Mkewe Wa Ndoa Alishindwa Kuishi Nae.Ataenda Ikulu Akafanye Nini.Ili Aende Akaongeze Mke Mwingine Au ?
 

Mkuu ebu tueleze maana ya akili nyingi? Na ukifanikiwa kueleza tupe faida za kuwa na akili nyingi?
 
Naona kama sielewi post! Kwa maana nyingine alifaa Asha au Amina? Au ndo Lowassa? Briefly I don't get it!
 
Mkuu ebu tueleze maana ya akili nyingi? Na ukifanikiwa kueleza tupe faida za kuwa na akili nyingi?

Kua Na Akili Nyingi Ni Kua Na Uwezo Wa Kujitambua Na Kujua Udhaifu Ulionao Pamoja Na Pontential Uliyonayo.Kua Na Uelewa Wa Kusoma Alama Za Nyakati Na Kujua Ni Njia Ipi Inafaha Na Ni Nyepesi Kupita Kwa Wakati Uliopo Na Kwa Changamoto Zilizopo.Ili Kutimiza Malengo Yako Uliyojiwekea.
Faida Kubwa Ya Kua Na Akili Nyingi Ni Kufanya Maamuzi Sahihi Kwa Wakati Sahihi Na Kwa Faida Sahihi Ya Walio Wengi.Nadhani Nimeeleweka Mkuu Japo Kwa Kifupi.
 
Ki ukweli ninamkubali sana magufuli katika utendaji wake lakini sitarajii kama atafanya kitu kipya akiwa chini ya ccm.ccm ni chama kilichojaa viongozi wengi legelege,wala rushwa na watoa rushwa,chama kisicho na maono thabiti ya taifa hili na kizazi kijacho.namtazama magufuli ni kama lita moja ya maji ya moto inayotaka kuchanganywa kwenye pipa la maji ya baridi halafu itegemewe kuwa hilo pipa la maji ya baridi ligeuke kuwa maji ya moto kwa sababu eti ya hiyo lita moja ya moto.

Chama ni mfumo.mfumo unapokuwa mbovu sharti huwa ufumuliwe na kusukwa upya.nitolee mfano wa mfumo wa mnyororo wa baiskeli.mnyororo wa baiskeli unapokuwa umeisha au kuchakaa sharti huwa ni kuubadilisha na kuweka mpya.suruhisho la kuweka vipande vipande vipya kwenye mnyororo uliochoka huwa halisaidii kitu.waliowahi kutumia baiskeli kwa muda mrefu wanajua hili.

Chini ya ccm tumetumainishwa vitu vingi lakini hatujaviona.waliingia viongozi wengi wazuri lakini hawakufanikiwa kubadili kitu.kumbuka sokoine,akina mwakyembe nk.

kweli sitarajii jipya
 
Magufuli hawezi kushinda, nilisema humu... CCM furaha yao imeishia pale DODOMA jana... hali ni ngumu CCM kushinda, Lowassa ndio ilikuwa tegemeo lao, sasa ni Dr. Slaa UKAWA TU... watu siku hizi wanachagua mtu sio chama...!!!
 
Na bado mtaweweseka sana jipeni moyo muishi kwa matumaini kama ili safari yenu ya matumaini wakati sisi tunahitaji safari ya uhakika
Hivi ni kweli zile 700m alizokutwa nazo "Rostam" pale Dodoma zilikuwa za membe? Anayejuwa lile sakata limeishaje atujuze.
 
Bahati nzuri ni sisi Wananchi ndio tunamchagua Rais. Na tuna imani na magufuli. Slaa anadhani mamlaka ya Rais ni mepesi kama kupora wake za watu?
Bahati nzuri pia Magufuli anafahamika kwa uropokaji, ubabe, ujivuni na ukosefu wa hekima!!

Wananchi hatuwezi kurudia kumpa mtu nchi ambaye hashauriki! Tulifanya makosa ya kumpa nchi mtu dhaifu na asiye na maamuzi!!!

Hakika hatufanyi makosa hayo tena!!!
 
Mi naona kama ukawa wamepagawa hawakutegemea kama ccm watatoa mtu safi.sasa kila mwana ukawa anajaribu kumchusha hadhi magufuli kinguvu.muhimu ni kujipanga tu jinsi ya kuomba kura jamaa hachafuliki
Nilimsikia babu akitapatapa kwamba sasa watashinda kiulaini wakati hata mgombea hawana. Wakati ule alisema wakimuweka EL watatangaza ushindi saa 4 ash, leo kawekwa JPM bado anang'ang'ana eti watashinda! Akili za bavicha hovyo kabisa.
 
Unaanzaje kampeni kabla ya muda kutangazwa na tume ya uchaguzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…