Dr. Joyce Ndalichako, Katibu Mtendaji wa NECTA! "It's Time To Go!.

.Mkuu Sifongo, tukubali tukatae, NECTA, wamekaza uzi, kama ni geme ya football, wamekaba mpaka kona!, kama ni mkanda, wamekaza na kubana mpaka tundu la mwisho!. The motive behind ni kuwabania "wakina fulani" ili kuwakomoa!, na kiukweli, wamekomoleka!. Nimeuliza jee mnaijui long term impact ya ukomoaji huu?!. Watu hamuoni mbali, ukifika muda wa kutokea ya kutokea ndipo mtawatafuta CIA, FBI na Scortland Yard, kuja kutafuta chanzo!. Jee wewe unawajua wengi waliozungusha ni kutoka kundi gani?!. Pasco.
 
Kabla sijachangia mkuu pasco naomba jibu, nakiri sijui wanatoka kundi lipi. Tafadhali funguka
 
Na masters yako bwana mushi..mawazo yako bado ni butu! kisaikolojia mwalimu toka moyoni anauwezo mkubwa wakumwezesha mwanafunzi yeyote..kitaalamu!!

Huyo mwalimu usipo mwezesha ni kazi bure
 
We unamfahamu sana hadi uone si Pasco aliyeandika? si ndio huyu huyu huwa anaona kuwa ccm ni watawala wazuri? kawambwa ndio!

Kwa mawazo yangu hapa ametoka mno nje ya uwanja. Kwamba tatizo ni mtihani mgumu kwa lengo la kufelisha kundi.....je. na zile za kata kwetu masai...ukiacha udini.
 
Badala ajiuzulu Raisina serikali yakekwa kushindwa kuweka facilities za maana kwenye mfumo wa elimu nchini mnataka mama Ndalichako astep down? Nendeni kwenye chanzo achana na ubabaishaji wa kisiasa!!!!
 
Hivi NECTA hakuna rufaa? Kama ipo si Pasco usonge mbele na mwanao kichwa cha hisabati mkajiridhishe?
 
Last edited by a moderator:
Hivi NECTA hakuna rufaa? Kama ipo si Pasco usonge mbele na mwanao kichwa cha hisabati mkajiridhishe?
Mkuu Dina, huku ndiko ninakoelekea, hapa naandika tuu ili kupunguza machungu!, hivyo kushusha ressure na hasira na maumivu!.
P.
 
Yaani Ndalichako aachie ngazi kwa sababu mwanao kibogoyo? acha masikhara shehe.
 
kwa ufupi nadhani wengi hawafahamu kuwa mtihani hautungwi NECTA. Waalimu hawa wanaofundisha mashuleni ndio wanatunga maswali halafu maswali yanapelekwa NECTA kwenye question bank.
Baada ya hapo jopo la kila somo wanachagua maswali na kutunga paper 4 kwa kila somo.
Baada ya hapo jopo lingine linakaa kuangalia hayo maswali kama yanaendana na syllabus na mengineyo.

Basi baada ya hapo linabaki jopo la siri la kuchagua paper ipi ifanywe na wanafunzi.

Sasa mkimlaumu Ndalichako mtakuwa mnakosea maana utungaji mtihani una taratibu zake.
 

NECTA inahusika vipi na uwepo wa shule bora na hafifu?

NECTA inahusika vipi kuwanyang'anya kidogo walichonacho hao watoto wasionacho?

Hicho ilichowanyang'anya ni kipi?.

Naamini ndugu Pasco ni mwandishi wa habari wa siku nyingi na hiki unachoandika hapa unakijua na sio bahati mbaya au ndo staili ya kutafuta ukuu wa wilaya?

Hakuna mtu anayefikiri sawa sawa ambaye atailaumu NECTA.

Wambie hao ambao unawajua wewe warudishe morali iliyopotea ya walimu, wambie waajiri walimu wa kutosha katika hizo shule unazoziita za wasionacho, wambie wapeleke vifaa vya elimu na wajenge mazingira mazuri ya kutolea elimu.

NECTA haiwezi kuwapa daraja la kwanza wanafunzi waliochora zombi, na wala Huyo Mkurugenzi hasahihishi mitihani wala hatungi mitihani yeye anaratibu tu, mitihani inatungwa na walimu kulingana na mitaala iliyopo iwe halali au feki si swala lake.

Tatizo la elimu nchi hii si NECTA hata NECTA ikifutwa hao watoto watakuwa wajinga tu iwapo hawatajengewa mazingira bora ya elimu, na hata NECTA ikiwapa wote hao 95% waliofeli daraja la kwanza haitawafanya wawe na elimu ujinga wao utaendelea tu.

Tuisaidie jamii kuondoa tatizo kwa kukemea kiini cha tatizo sio kusafisha uozo na kujaribu kuwaaminisha watu suluhisho lisilo na mashiko
 
Kila mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi yake, amesikitishwa sana na hali inayoendelea hata kama mtoto wake si miongoni mwa waliofeli lakini huenda mtoto wa dada yake au wa shemeji yake na pengine mwakani naye mtoto wake atajiunga na kundi hili kubwa la wahanga wa mfumo mbaya na kutowajibika kwa wenye dhamana.

Matatizo yaliyopo kwenye elimu hayapo katika ngazi za chini tu bali yameenea hadi vyuo vikuu vya umma.

Watoto wanaofeli si kwamba hawana uwezo bali wamenyimwa fursa kwa makusudi na viongozi wabinafsi na wasiojali.

Hatuwezi kuondoa tatizo bila kusema ukweli, mficha ugonjwa kifo kitamuumbua. Kila mtanzania awajibike kwa nafasi yake, na amwajibishe mwenzake.

Vinginevyo mwakani na miaka ijayo hata hao 5% waliofaulu hawatakuwepo.
 

Pasco, umetumia kipimo gani kujua mitihani ilitungwa kuwakomoa wanafunzi? Maana elimu tusiifanyie utani...tutajazana vilaza watupu tukijidai wasomi na hakuna lolote tutakuwa tunafanya maana hatukusoma tukaelimika.
 
Kabla sijachangia mkuu pasco naomba jibu, nakiri sijui wanatoka kundi lipi. Tafadhali funguka
Mkuu Nguruvi3, hili nililijibu katika uzi wangu mwingine Opinion: Matokeo Mabaya ya Form IV, Jee?, Is It "Real?F" or there ...

 

mbona pepa ilikuwa easy tu
 
Pasco kuna mtu kaingilia account yako sio wewe! Kama ni wewe ama sijakuelewa au umefilisika mawazo
 
Thanks Bamukunda kwa appreciation.
Unajua watz tumezoea kulalamika tu. Hivi mtoto akifaulu si unatamba mitaani? Je, unampelekea kitenge Ndalichako au kreti ya soda Dr Shukuru Kawamba? Si unatamba kuwa mtoto wangu kipanga? Akifeli unatafuta mchawi. Je, Ndalichako kasema wachore mazombi? Inauzi baadala ya kuudhi. Kwa mtindo huu wa kutaka watu wajiuzulu, basi na wazazi watoto wao waliofeli wajiuzulu.
 
Hii nimeikuta mahali nikaona niilete na humu ili wale wote wasio niealewa angalau waanze kuelewa kuwa matokeo haya sio bure, iko namna!.


Pasco.
 
Pasco,
uissahau utamaduni mbaya/mbovu wa baadhi ya wanafunzi kutokufanya kazi moja tu ya kusoma.....wanafunzi wanajihusisha na mambo mengi yanayowanyima muda wa kusoma kwa bidii
Usihau adabu mbaya za wanafunzi....mwanafuzi yuko darasani, mwalimu anafundisha yeye anatuma meseji kwenye simu au anachati kwenye fesubuku...(kumbuka kuna tangazo la HAKIELIMU kuhusu wanafunzi kukosa adabu wakiwa darasani...hata mbele ya mwalimu) Katika tangazo hilo anaonekana mwanafunzi akikaripiwa na mwalimu kwa sababu ya kuchezea simu darasani...mwanafunzi alijibuje? MMHH MWALIMU MNOKO....nk. Haya matangazo si ya kuzusha...haya mambo yanatokea huko madarasani.

Usisahau wazazi ambao wanaungana na watoto wao kuwashambulia walimu kwa sababu tu...mwalimu anamfuatilia nyendo/tabia zake

TUMEPOTEZA DIRA YA ELIMU NA DHIMA YA MWALIMU
LAZIMA TURUDISHE TRENI KWENYE RELI
WAKATI WA MWALIMU NYERERE...WALIMU WALIPEWA HADHI YAO YA KUWALEA WATOTO...NA KUWAFUNZA ADABU NJEMA
LEO HII WALIMU WAMEPOKONYWA MAMLAKA HAYO...WALIMU WANAOGOPA KUWAKOSOA WATOTO..MAANA WAKIFANYA HIVYO WANAKUMBANA NA KICHAPO MTAANI/ KULAZWA NJE KIUSHIRIKINA KAMA MDAU HAPO JUU ALIVYODOKEZA/ USISAHAU WANAFUNZI WA KIUME KUWATONGOZA WALIMU WA KIKE NA KUWABAKA....WALIMU WAKISHITAKI JAMBO HILI WAZAZI WANAWATETEA WATOTO WAO.......(KAMA KWELI WEWE NI MTANZANIA MWENYE KUFUATILIA MAMBO YA NCHI YAKO, ITAKUWA HILI UMELISIKIA.LIMETOKEA MWAKA HUU MWANZONI/MWAKA JANA MWISHONI HAPO PWANI...SHULE MOJAWAPO BAGAMIYO)

YOTE HAYO PASCO HUYAONI?
HUONI KILA UPANDE UNA MATATIZO?
KATIKA TABIA ZOTE NILIZOZIANDIKA HAPO JUU...USITEGEMEE MWANANFUNZI MWENYE MAADILI MABAYA ATAKUWA NA AKILI YA KUFAULU....NI SIFURI TU AKIFAULU SANA NI FOUR.
KIBURI, DHARAU, KUKOSA ADABU NI MAMBO YANAYOCHANGIA KUFELI MWANAFUNZI...TUBADILIKE WATANZANIA...TUTAFUTE TIBA YA KWELI KWA MATATIZO YETU YA KIELIMU NA MENGINEYO...TUSIKATE MATAWI...WAKATI MZIZI WA TATIZO TUNAUPALILIA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…