Dr. Joyce Ndalichako, Katibu Mtendaji wa NECTA! "It's Time To Go!.

Dr. Joyce Ndalichako, Katibu Mtendaji wa NECTA! "It's Time To Go!.

Mkuu Pasco nadhani hapa umeenda pembeni ya mstari, sidhani kama NECTA walifanya hicho ulichoandika, na unavyosema hivyo ni unawakosea hao unaodhani ni wajinga mpaka NECTA wawe na uhakika kuwa kwa mtihani huu wakina fulani watashinda na kina fulani watashindwa.
.Mkuu Sifongo, tukubali tukatae, NECTA, wamekaza uzi, kama ni geme ya football, wamekaba mpaka kona!, kama ni mkanda, wamekaza na kubana mpaka tundu la mwisho!. The motive behind ni kuwabania "wakina fulani" ili kuwakomoa!, na kiukweli, wamekomoleka!. Nimeuliza jee mnaijui long term impact ya ukomoaji huu?!. Watu hamuoni mbali, ukifika muda wa kutokea ya kutokea ndipo mtawatafuta CIA, FBI na Scortland Yard, kuja kutafuta chanzo!. Jee wewe unawajua wengi waliozungusha ni kutoka kundi gani?!. Pasco.
 
.Mkuu Sifongo, tukubali tukatae, NECTA, wamekaza uzi, kama ni geme ya football, wamekaba mpaka kona!, kama ni mkanda, wamekaza na kubana mpaka tundu la mwisho!. The motive behind ni kuwabania "wakina fulani" ili kuwakomoa!, na kiukweli, wamekomoleka!. Nimeuliza jee mnaijui long term impact ya ukomoaji huu?!. Watu hamuoni mbali, ukifika muda wa kutokea ya kutokea ndipo mtawatafuta CIA, FBI na Scortland Yard, kuja kutafuta chanzo!. Jee wewe unawajua wengi waliozungusha ni kutoka kundi gani?!. Pasco.
Kabla sijachangia mkuu pasco naomba jibu, nakiri sijui wanatoka kundi lipi. Tafadhali funguka
 
Na masters yako bwana mushi..mawazo yako bado ni butu! kisaikolojia mwalimu toka moyoni anauwezo mkubwa wakumwezesha mwanafunzi yeyote..kitaalamu!!

Huyo mwalimu usipo mwezesha ni kazi bure
 
We unamfahamu sana hadi uone si Pasco aliyeandika? si ndio huyu huyu huwa anaona kuwa ccm ni watawala wazuri? kawambwa ndio!

Kwa mawazo yangu hapa ametoka mno nje ya uwanja. Kwamba tatizo ni mtihani mgumu kwa lengo la kufelisha kundi.....je. na zile za kata kwetu masai...ukiacha udini.
 
Badala ajiuzulu Raisina serikali yakekwa kushindwa kuweka facilities za maana kwenye mfumo wa elimu nchini mnataka mama Ndalichako astep down? Nendeni kwenye chanzo achana na ubabaishaji wa kisiasa!!!!
 
Hivi NECTA hakuna rufaa? Kama ipo si Pasco usonge mbele na mwanao kichwa cha hisabati mkajiridhishe?
Mkuu Dina, huku ndiko ninakoelekea, hapa naandika tuu ili kupunguza machungu!, hivyo kushusha ressure na hasira na maumivu!.
P.
 
Yaani Ndalichako aachie ngazi kwa sababu mwanao kibogoyo? acha masikhara shehe.
 
kwa ufupi nadhani wengi hawafahamu kuwa mtihani hautungwi NECTA. Waalimu hawa wanaofundisha mashuleni ndio wanatunga maswali halafu maswali yanapelekwa NECTA kwenye question bank.
Baada ya hapo jopo la kila somo wanachagua maswali na kutunga paper 4 kwa kila somo.
Baada ya hapo jopo lingine linakaa kuangalia hayo maswali kama yanaendana na syllabus na mengineyo.

Basi baada ya hapo linabaki jopo la siri la kuchagua paper ipi ifanywe na wanafunzi.

Sasa mkimlaumu Ndalichako mtakuwa mnakosea maana utungaji mtihani una taratibu zake.
 
Wanabodi,

Kwa maoni yangu, kitendo cha NECTA kutunga mtihani ambao siyo ili kuwakomoa "watu fulani " kulikopelekea wanafunzi kufeli vibaya ili kujustify hao kina "fulani" ni wajinga!, na kuyapeleka makaratasi halisi ya mtihani kuuanika uthibitisho wa jinsi hao kina fulani walivyo jibu utumbo yakiwemo matusi ili kupata public sympathy kujustify tatizo sio NECTA, sio mitihani wall sio usahihishaji bail ni wanafunzi ndio wajinga na vibonde, hakipaswi kuachwa bila kupingwa!.

Wengi waliangalia hili kwa jicho la juu juu juu tuu bila kujiuliza wajinga halisi ni kina nani na long impact ya ukomoaji huu wa NECTA utalifikisha wapi taifa letu in a long run baada ya matokeo hayo kujenga matabaka ya wenye nacho na wasionacho!.

Kwa sio jua Wengi wa waliofaulu ni watoto wa wenye nacho ambao wana uwezo wa kuwalipia watoto wao shule bora, na wengi wa waliofeli ni watoto wa wa wasionacho hivyo Mama Ndalichako kupitia NECTA anawanyanganya hata hicho kidogo walichonacho, unategemea mini after a long time ?!.

I think it's time up for Mama, Dr. Joyce Ndalichako to go!, not withstanding madhaifu mengine yote wenye mfumo wetu wa elimu.

Pasco.

NECTA inahusika vipi na uwepo wa shule bora na hafifu?

NECTA inahusika vipi kuwanyang'anya kidogo walichonacho hao watoto wasionacho?

Hicho ilichowanyang'anya ni kipi?.

Naamini ndugu Pasco ni mwandishi wa habari wa siku nyingi na hiki unachoandika hapa unakijua na sio bahati mbaya au ndo staili ya kutafuta ukuu wa wilaya?

Hakuna mtu anayefikiri sawa sawa ambaye atailaumu NECTA.

Wambie hao ambao unawajua wewe warudishe morali iliyopotea ya walimu, wambie waajiri walimu wa kutosha katika hizo shule unazoziita za wasionacho, wambie wapeleke vifaa vya elimu na wajenge mazingira mazuri ya kutolea elimu.

NECTA haiwezi kuwapa daraja la kwanza wanafunzi waliochora zombi, na wala Huyo Mkurugenzi hasahihishi mitihani wala hatungi mitihani yeye anaratibu tu, mitihani inatungwa na walimu kulingana na mitaala iliyopo iwe halali au feki si swala lake.

Tatizo la elimu nchi hii si NECTA hata NECTA ikifutwa hao watoto watakuwa wajinga tu iwapo hawatajengewa mazingira bora ya elimu, na hata NECTA ikiwapa wote hao 95% waliofeli daraja la kwanza haitawafanya wawe na elimu ujinga wao utaendelea tu.

Tuisaidie jamii kuondoa tatizo kwa kukemea kiini cha tatizo sio kusafisha uozo na kujaribu kuwaaminisha watu suluhisho lisilo na mashiko
 
Kila mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi yake, amesikitishwa sana na hali inayoendelea hata kama mtoto wake si miongoni mwa waliofeli lakini huenda mtoto wa dada yake au wa shemeji yake na pengine mwakani naye mtoto wake atajiunga na kundi hili kubwa la wahanga wa mfumo mbaya na kutowajibika kwa wenye dhamana.

Matatizo yaliyopo kwenye elimu hayapo katika ngazi za chini tu bali yameenea hadi vyuo vikuu vya umma.

Watoto wanaofeli si kwamba hawana uwezo bali wamenyimwa fursa kwa makusudi na viongozi wabinafsi na wasiojali.

Hatuwezi kuondoa tatizo bila kusema ukweli, mficha ugonjwa kifo kitamuumbua. Kila mtanzania awajibike kwa nafasi yake, na amwajibishe mwenzake.

Vinginevyo mwakani na miaka ijayo hata hao 5% waliofaulu hawatakuwepo.
 
Wanabodi,

Kwa maoni yangu, kitendo cha NECTA kutunga mtihani ambao siyo ili kuwakomoa "watu fulani " kulikopelekea wanafunzi kufeli vibaya ili kujustify hao kina "fulani" ni wajinga!, na kuyapeleka makaratasi halisi ya mtihani kuuanika uthibitisho wa jinsi hao kina fulani walivyo jibu utumbo yakiwemo matusi ili kupata public sympathy kujustify tatizo sio NECTA, sio mitihani wall sio usahihishaji bail ni wanafunzi ndio wajinga na vibonde, hakipaswi kuachwa bila kupingwa!.

Wengi waliangalia hili kwa jicho la juu juu juu tuu bila kujiuliza wajinga halisi ni kina nani na long impact ya ukomoaji huu wa NECTA utalifikisha wapi taifa letu in a long run baada ya matokeo hayo kujenga matabaka ya wenye nacho na wasionacho!.

Kwa sio jua Wengi wa waliofaulu ni watoto wa wenye nacho ambao wana uwezo wa kuwalipia watoto wao shule bora, na wengi wa waliofeli ni watoto wa wa wasionacho hivyo Mama Ndalichako kupitia NECTA anawanyanganya hata hicho kidogo walichonacho, unategemea mini after a long time ?!.

I think it's time up for Mama, Dr. Joyce Ndalichako to go!, not withstanding madhaifu mengine yote wenye mfumo wetu wa elimu.

Pasco.

Pasco, umetumia kipimo gani kujua mitihani ilitungwa kuwakomoa wanafunzi? Maana elimu tusiifanyie utani...tutajazana vilaza watupu tukijidai wasomi na hakuna lolote tutakuwa tunafanya maana hatukusoma tukaelimika.
 
Kabla sijachangia mkuu pasco naomba jibu, nakiri sijui wanatoka kundi lipi. Tafadhali funguka
Mkuu Nguruvi3, hili nililijibu katika uzi wangu mwingine Opinion: Matokeo Mabaya ya Form IV, Jee?, Is It "Real?F" or there ...

Wanabodi,

Naomba kuanza kwa kudeclare interest, mimi ni mhanga wa matokeo haya mabaya ya Form IV, nilikuwa na vijana wangu wawili, ambao walichaguliwa kujiunga na shule za kata, wife akashauri tuwahamishie shule za maana, kwa vile mimi ni mtu wa Nyerere type, nikamgomea, kwa hoja kuwa maadam watoto wa wananchi wa kawaida, wanasoma shule hizo za kata kwa sababu hawana jinsi, lets watoto wetu wasome shule hizo hizo za kawaida, "if they are bright, they are bright no matter wanasoma wapi!". Kiukweli kwa hili, tuligombana!.

Baada ya kufanya mitihani, wote wawili walituhakikishia Div 1 zisizo na mawaa!, wakasema kwa jinsi walivyoiona mitihani hiyo na jinsi walivyoifanya, "there is no way, watakosa first class!, matokeo yametoka, "No first class!", na kwa shule zao, first class ni nil!, yaani hakuna!.

Nazungumza haya kwa uchungu sana, kwa sababu nimeguswa!.
 
wanabodi,

kwa maoni yangu, kitendo cha necta kutunga mtihani ambao siyo ili kuwakomoa "watu fulani " kulikopelekea wanafunzi kufeli vibaya ili kujustify hao kina "fulani" ni wajinga!, na kuyapeleka makaratasi halisi ya mtihani kuuanika uthibitisho wa jinsi hao kina fulani walivyo jibu utumbo yakiwemo matusi ili kupata public sympathy kujustify tatizo sio necta, sio mitihani wall sio usahihishaji bail ni wanafunzi ndio wajinga na vibonde, hakipaswi kuachwa bila kupingwa!.

Wengi waliangalia hili kwa jicho la juu juu juu tuu bila kujiuliza wajinga halisi ni kina nani na long impact ya ukomoaji huu wa necta utalifikisha wapi taifa letu in a long run baada ya matokeo hayo kujenga matabaka ya wenye nacho na wasionacho!.

Kwa sio jua wengi wa waliofaulu ni watoto wa wenye nacho ambao wana uwezo wa kuwalipia watoto wao shule bora, na wengi wa waliofeli ni watoto wa wa wasionacho hivyo mama ndalichako kupitia necta anawanyanganya hata hicho kidogo walichonacho, unategemea mini after a long time ?!.

I think it's time up for mama, dr. Joyce ndalichako to go!, not withstanding madhaifu mengine yote wenye mfumo wetu wa elimu.

Pasco.

mbona pepa ilikuwa easy tu
 
Pasco kuna mtu kaingilia account yako sio wewe! Kama ni wewe ama sijakuelewa au umefilisika mawazo
 
Thanks Bamukunda kwa appreciation.
Unajua watz tumezoea kulalamika tu. Hivi mtoto akifaulu si unatamba mitaani? Je, unampelekea kitenge Ndalichako au kreti ya soda Dr Shukuru Kawamba? Si unatamba kuwa mtoto wangu kipanga? Akifeli unatafuta mchawi. Je, Ndalichako kasema wachore mazombi? Inauzi baadala ya kuudhi. Kwa mtindo huu wa kutaka watu wajiuzulu, basi na wazazi watoto wao waliofeli wajiuzulu.
 
Hii nimeikuta mahali nikaona niilete na humu ili wale wote wasio niealewa angalau waanze kuelewa kuwa matokeo haya sio bure, iko namna!.


WAKATI mjadala wa matokeo mabaya ya kidato cha nne ukiendelea kulitikisa taifa, kashfa mpya ya matokeo hayo imeibuliwa.

Kashfa hiyo mpya imeibuliwa na Mkurugenzi wa Shule ya Green Acres, Julian Bujugo, kwamba matokeo ya baadhi ya shule nchini ikiwamo yake yamechakachuliwa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Bujugo alisema kuwa baadhi ya wanafunzi kwenye shule yake hawakufanya mitihani ya kidato cha nne, lakini matokeo yanaonesha wamefaulu kwa kupata alama za juu.

Alitaja mfano wa mwanafunzi, Humphrey Sanga, mwenye namba 01197/148, ambaye hakufanya mitihani hiyo lakini matokeo yanaonesha amefaulu kwa kupata alama nzuri.

“Huyu mwanafunzi tulimsimamisha na hakufanya mitihani, lakini matokeo yake yanaonekana amepata hivi; Civics D, Historia D, Jiografia C, Kiswahili D, English C, Physics D, Chemistry C, Biology C, Basic Mathematics D, ambapo amepata daraja la tatu pointi 24,” alisema Bujugo.

Alimtaja mwanafunzi mwingine, Martin Rushaigwa, namba 01197/0173, ambaye alifanya masomo ya ‘Arts’.
Alisema matokeo ya mwanafunzi huyo yanaonesha kuwa ameongezewa alama za masomo ya biashara ya Bookeeping na Commerce, ambayo hakuyafanya kabisa.

Alimtaja mwanafunzi mwingine aliyefanya mtihani huo lakini matokeo yake yanaonesha amewekewa ‘absent’ na mwanafunzi mwingine, Mbazi Volta, hakufanya mitihani lakini amepewa alama za ufaulu.

“Matokeo hayo yananipa wasiwasi kwamba yanaweza kuwa yamechakachuliwa,” alisema Bujugo.

Mkurugenzi huyo anaiomba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kurudia kusahihisha mitihani hiyo ili kuondoa ukungu ulioligubika taifa kwa sasa kuhusu matokeo ya kidato cha nne.

“Naomba usahihishaji urudiwe, maana huu ni ubabaishaji mkubwa…matokeo hayo yamewaathiri watoto kisaikolojia na sijui watakwenda wapi?,” alihoji.

Alisisitiza kuwa usahihishaji urudiwe kwani katika shule hiyo wanafunzi wenye uwezo mkubwa tangu walipoanza kidato cha kwanza ndio waliofanya vibaya wakati waliokuwa wakifanya vibaya, wameibuka na alama za juu.

Mkurugenzi huyo alisema wazazi wa watoto hao wanatarajiwa kukutana mwishoni mwa wiki hii kujadiliana kuhusu matokeo hayo na hatua za kuchukua.
Akitolea ufafanuzi suala hilo, Msemaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), John Nchimbi, alisema si kweli kuwa matokeo hayo yamechakachuliwa bali ni matokeo halisi ya shule hiyo.

Alisema iwapo mkurugenzi wa shule hiyo ana shaka na matokeo hayo, alitakiwa kufika katika ofisi za baraza hilo ili apatiwe taarifa sahihi kabla ya kutoa taarifa katika vyombo vya habari.

“Mi nimeangalia hayo majina, naona yapo sawa na hata huyo mwanafunzi ambaye anasemekana hakufanya mitihani na akapewa alama…napenda kusema kuwa alama alizopewa si zake na hata katika orodha yetu anaonekana kuwa hakufanya mitihani,” alisema.

Katika hatua nyingine, Waziri wa wizara hiyo, Dk. Shukuru Kawambwa na wenzake, wamekuwa bubu kueleza endapo wako tayari kujiuzulu au la.

Tanzania Daima ilifika wizarani hapo jana kutaka kuonana na Waziri Kawambwa ili atoe msimamo wake, mwandishi alijibiwa kuwa waziri huyo alikuwa kikaoni na asingeweza kutoka.

Hata waziri alipopigiwa simu pamoja na kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno, hakupokea wala kujibu ujumbe huo.
Kwa upande wake, katibu mkuu wa wizara hiyo naye hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwa madai kuwa alikuwa kikaoni.

Naye Naibu Waziri, Philipo Mulugo, alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi kueleza msimamo wake, simu yake iliita bila kupokewa na hata hakuwa tayari kujibu meseji ya ujumbe mfupi.


[TD="bgcolor: #FFFFFF"]
Matokeo kidato cha nne ‘feki’
• Mkurugenzi Green Acres afichua siri nzito

na Betty Kangonga
Tanzania Daima



[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]

Pasco.
 
Pasco,
uissahau utamaduni mbaya/mbovu wa baadhi ya wanafunzi kutokufanya kazi moja tu ya kusoma.....wanafunzi wanajihusisha na mambo mengi yanayowanyima muda wa kusoma kwa bidii
Usihau adabu mbaya za wanafunzi....mwanafuzi yuko darasani, mwalimu anafundisha yeye anatuma meseji kwenye simu au anachati kwenye fesubuku...(kumbuka kuna tangazo la HAKIELIMU kuhusu wanafunzi kukosa adabu wakiwa darasani...hata mbele ya mwalimu) Katika tangazo hilo anaonekana mwanafunzi akikaripiwa na mwalimu kwa sababu ya kuchezea simu darasani...mwanafunzi alijibuje? MMHH MWALIMU MNOKO....nk. Haya matangazo si ya kuzusha...haya mambo yanatokea huko madarasani.

Usisahau wazazi ambao wanaungana na watoto wao kuwashambulia walimu kwa sababu tu...mwalimu anamfuatilia nyendo/tabia zake

TUMEPOTEZA DIRA YA ELIMU NA DHIMA YA MWALIMU
LAZIMA TURUDISHE TRENI KWENYE RELI
WAKATI WA MWALIMU NYERERE...WALIMU WALIPEWA HADHI YAO YA KUWALEA WATOTO...NA KUWAFUNZA ADABU NJEMA
LEO HII WALIMU WAMEPOKONYWA MAMLAKA HAYO...WALIMU WANAOGOPA KUWAKOSOA WATOTO..MAANA WAKIFANYA HIVYO WANAKUMBANA NA KICHAPO MTAANI/ KULAZWA NJE KIUSHIRIKINA KAMA MDAU HAPO JUU ALIVYODOKEZA/ USISAHAU WANAFUNZI WA KIUME KUWATONGOZA WALIMU WA KIKE NA KUWABAKA....WALIMU WAKISHITAKI JAMBO HILI WAZAZI WANAWATETEA WATOTO WAO.......(KAMA KWELI WEWE NI MTANZANIA MWENYE KUFUATILIA MAMBO YA NCHI YAKO, ITAKUWA HILI UMELISIKIA.LIMETOKEA MWAKA HUU MWANZONI/MWAKA JANA MWISHONI HAPO PWANI...SHULE MOJAWAPO BAGAMIYO)

YOTE HAYO PASCO HUYAONI?
HUONI KILA UPANDE UNA MATATIZO?
KATIKA TABIA ZOTE NILIZOZIANDIKA HAPO JUU...USITEGEMEE MWANANFUNZI MWENYE MAADILI MABAYA ATAKUWA NA AKILI YA KUFAULU....NI SIFURI TU AKIFAULU SANA NI FOUR.
KIBURI, DHARAU, KUKOSA ADABU NI MAMBO YANAYOCHANGIA KUFELI MWANAFUNZI...TUBADILIKE WATANZANIA...TUTAFUTE TIBA YA KWELI KWA MATATIZO YETU YA KIELIMU NA MENGINEYO...TUSIKATE MATAWI...WAKATI MZIZI WA TATIZO TUNAUPALILIA
 
Back
Top Bottom