Dr. Modestus Kipilimba astaafu rasmi utumishi wa umma

Dr. Modestus Kipilimba astaafu rasmi utumishi wa umma

Mkurugenzi wa zamani wa taasisi ya usalama wa Taifa, Dr. Modestus Kipilimba amestaafu utumishi wa umma baada ya uwepo wake Namibia kama balozi kuhitimishwa rasmi na Rais Samia.

Kipilimba alihudumu kama mkurugenzi wa usalama wa Taifa kwa miaka mitatu chini ya utawala wa Rais Magufuli(2016-19) kabla ya uteuzi wake wa kushtua kuwa balozi wa Tanzania nchini Namibia.

Uteuzi wake ulimfanya kuwa balozi wa kwanza wa Tanzania Namibia na kuwa mtu muhimu katika utengenezaji wa ubalozi huo jijini Windhoek.

Mwaka 2022 mwanasiasa Tundu Lissu alimtuhumu Kipilimba kuongoza kikosi kazi kilichompiga risasi mjini Dodoma, Lissu alisema wameua zaidi ya watu 400 maeneo ya Mkuranga, Kibiti Kilwa Rufiji.

Pia, soma
=>Rais Magufuli amteua Dkt. Kipilimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS)
=>Rais Magufuli amteua Diwani Athuman Msuya Mkurugenzi Mkuu (TISS), achukua nafasi ya Dr. Modestus Kipilimba
=>Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba



Mwanzo wa maisha ya Majuto, na masikitiko yatakayofuatwa na kifo kisicho na furaha
 
Apumzike ale maisha

Mengine haya ya wanadamu ni upumbavu tu usio na maana, hisia za kijinga haziwezi mfanya mtu akose kile Mungu kampa!

Hukumu za Mungu ni za haki na kweli

Za wanadamu ni upumbavu, ujinga, na husuda na wivu usio na maana
 
Ndio maana unajiita mtoto wa shule huyajui mengi! Huyu alipiga simu akiwa Namibia akaongea Magufuli yupo mzima bukheri wa afya Erythrocyte yuko sahihi.
Kumbukumbu zako ziko vizuri? Mwaka 2019 aliteuliwa kuwa Balozi Namibia. Mwamba Jiwe Magufuli alifarikia mwaka 2021 wakati Kipilimba yuko Namibia. Halafu wewe eti alidanganya! Unakurupuka na nini?
 
Kumbukumbu zako ziko vizuri? Mwaka 2019 aliteuliwa kuwa Balozi Namibia. Mwamba Jiwe Magufuli alifarikia mwaka 2021 wakati Kipilimba yuko Namibia. Halafu wewe eti alidanganya! Unakurupuka na nini?
Alitekeleza majukumu yake kama Balozi kuitangazia dunia kwamba Magufuli anachapa kazi !

IMG_20230817_154444.jpg
 
View attachment 2719872
The Originals. Look at how happy everyone was.
Kwny Hii picha aliebaki peke yake ni Madam Makakala

Huyo wa kushoto alistuka Dereva wake anamuonesha Message za Pongezi kutoka kwny group la Ofisini kuwa Rais karidhia ombi lake la kustaafu kwa hiyari wakati hajawahi kuomba kustaafu
 
Back
Top Bottom