Dr. Mwakyembe Vs. TAKUKURU

Hili la kulipwa mara mbili ni kosa, tena kubwa, lakini nila mlipwaji au mlipaji? Wote hawana kosa ila sytem ndiyo yenye makosa, serikali isiyo makini, lets vote it out.
 
Ewe mtoa mada nadhani una ubia na ufisadi. Unadandia mada. Hili tatizo halitaisha mapema. Hata kama mwakyembe sio safi, hao kina hosea umewazungumziaje? Tafuta kinga, usikimbilie kutibu
 
Swala la Posho ni kosa, lakini haliwezi ondolewa kwa kosa jingine la PCCB kuwahoji Wabunge wakati yaonyesha wazi kabisa kwamba Waziri mkuu alisha wasilisha malalamiko yake Bungeni na hayakupewa kipaumbele na wahusika..
Sote tunakubaliana na makosa haya ya Wabunge na yapo mengi sana lakini hatuwezi vunja sheria kwa sababu ya kuwafurahisha baadhi ya watu. Kama swala hili lingekuwa muhimu, bunge lingezungumzia na kuweka sheria dhidi ya posho hizi, lakini maadam Sitta na katibu wake walighairi barua ya waziri mkuu, wakashindwa kuonya vitendo hivyo wazi isipokuwa kwa kupitia mlango wa nyuma..wanaotakiwa kuhojiwa ni Spika Sitta na katibu wake.
Sheria inasema wazi kabisa kwamba wabunge wetu wamepewa kinga na sheria jambo ambalo nashindwa kuelewa viongozi wetu huitumia tu pale wao wanapokuwa ktk mshikemshike..
Haiwezi kuhalalisha tabia hii kumhukumu Mwakyembe ambaye amekataa kuhojiwa kwa sababu ni utaratibu mbovu uliotumika.
Two mistakes can't it right!
 
wazee hivi hili swala la posho mbili kwa wabunge limebeba uzito kuliko lile la richmonduli, EPA nk??? maana naona saa hizi attention inahamia pande nyingine. mimi naona waliendeleze kwanza la richmonduli , halafu lije la posho mbili.


nchi tatizo vipaumbele kidogo ni shida .. si unakumbuka watu walivyojadili kuhusu suti .. yani mjadala wa kitaifa kabisa na wasomi wa chuo kikuu walihojiwa.. sasa ndio haya ya posho posho tunasahau masuala makubwa yanayogusa maslahi ya wananchi wengi...... hakuna mtu anauliza kwa nini hadi sasas sualla la Richmind halipo kwenye ratiba ?Nasikia inapanga liishie kwenye kamati .. kuwa kamati imejadili na imeridhika na utekelezaji , mwisho wa issue.
 
ubovu wa nchi hii ni kuwa imeoza kila sehemu, cha muhimu ni kutafuta uhuru wa hii nchi ambao wanyonyaji wa kikoloni wamewaachia wanyonyaji wa Tanu na kisha CCM, kazi ya muhimu ni kuitoa ccm madarakanni na kuanza upya kama taifa jipya
 


Mkandara am with you kwenye hili . nawataa takukuru kuendelea na kazi yao na pia Wabunge waendelee na kazi yao .Hakuna kosa hapa kama unachukua posho 2 na huku unasema ufisadi maana yake nini ?Sitta yuko matatani sasa ngome yake inahubiri mengine na kutenda mengine .So kazi kubwa hapo .Harakati zote ziendelee hakuna kosa dogo wala kubwa wizi ni wizi tu
 
Ewe mtoa mada nadhani una ubia na ufisadi. Unadandia mada. Hili tatizo halitaisha mapema. Hata kama mwakyembe sio safi, hao kina hosea umewazungumziaje? Tafuta kinga, usikimbilie kutibu

Nina ubia upi na ufisadi? Hii mada inamhusu Dkt Mwakyembe, ya Dkt Hoseah unaweza kuianzisha hata wewe, hakuna aliyekukataza! Nikianzisha ya Dkt Hoseah utauliza tena mbona sijaanzisha mada ya Dkt Slaa! One thread at a time pls!
 
Nina ubia upi na ufisadi? Hii mada inamhusu Dkt Mwakyembe, ya Dkt Hoseah unaweza kuianzisha hata wewe, hakuna aliyekukataza! Nikianzisha ya Dkt Hoseah utauliza tena mbona sijaanzisha mada ya Dkt Slaa! One thread at a time pls!


Msamehe bure huyo yuko kazini . Mie I long refused to agree that Mwakyembe alikuwa a clean person. Namkumbuka kwa tamko lake kwamba Maalim Seif alikuwa haini akamatwe ndipo akaukwaa ubunge . I never trusted him nor agreed with him . Ni fisadi tu hakuna CCM mzima hakika .
 

Hata kama kupokea posho mara mbili ingekuwa ni kuvunja sheria, kwa nini mtu yeyote aamini utendaji wa TAKUKURU iliyowahi kuibariki Richmondgate hasa wakati huu wa kuijadili Ripoti ya Richmond?

Dr. Slaa amekosea na uamuzi wa Dr. Mwakyembe ni sahihi na wa hiari yake na haupaswi kujadiliwa kwa vile TAKUKURU ilishajivua uhalali wa kupambana na rushwa.
 
Makaaya mawe,
Mkuu Dr.Slaa hajakosea hata kidogo, as a fact anacheza siasa zinavyotakiwa kuchezwa ktk msemo ule usemao samaki mmoja alkioza basi kapu zima hawafai...Yeye ni mpinzani na madudu yote haya yamefanya na chama CCM, ni chama cha Mwakyembe yeye anaogopa nini?.. kama kuna mvurugano ndani ya chama ndio furaha ya Dr. Slaa na ataendelea kuwapa ganja wapute..
 


mKUU unafikiri nini kitatokea kuhusu mjadala wa Richmond amacho serikali inakikwepa?

Rudi nyuma angalia histroia ya bunge letu, then anticipate uone nini watafanya wabunge wa CMM kuhusu Richmond!watamwangusha JK?? SIAMINI BADO

Naona ishu imekuwa twisted
 
Hili swala posho mbili kwa wabunge kuwa tatizo hadi TAKUKURU kuwahoji wabung nadhani limeibuliwa ili kuficha mambo mengine yanayo fanywa na Serikali. Nafikiri kuna kikao kilichokaa kikakubaliana hizo posho mbili na ndo maana zinatolewa. Mimi naona kuwahoji wabunge si shuluhisho la jambo hili. Kikao kilicho panga kuwa wabunge wapewe hizo posho, kingekaa tena na kubadilisha huo mfumo, nad then kiwaarifu wabunge kuwa posho mbili zimeondolewa kwa sababu kadha wa kadha. Jambo hili lingefanyika na kuisha bila takukuru kuhusishwa.
Kwa uelewa wangu nadhani kunamgongano wa maslihi ndo kilichoibua haya yote. Je kwani ni wabunge tu ndo wanapokea posho mbili? na kama kuna watu/viongozi wengine ambao wanapokea posho mbili, je wao wamechukuliwa hatua gani?
Viongozi wengine yawezekana hawapokei posho mbili lakin wanapokea posho moja ambayo ni zaidi ya posho kumi kulingana na kazi/sababu zinazomfanya apokee posho hiyo.
TAKUKURU ianzie ngazi za juu hadi za chini kuchunguza hizo posho zianazotolewa na kama kuna kasoro, wawaoji walioziweka/wanaozitoa na si kumhoji anayepokea kwani yeye anapokea kulingana na utaratibu uliowekwa.
 
Haya yale yale ya hisia pole sana mzee. but tutajitahidi kuvumiliana, mimi siku hizi nimekuwa na mango tree.
Ugomvi ni kupigana au? kutofautiana si ugomvi. na tatizo kubwa ni tofauti ya elimu ni kubwa sana kati ya hao madiwani na huyu jamaa. Sasa kumuelewa ni kazi sana.
 
Duh! kweli vita ya ufisadi ni ngumu! adui na askari gumu tofautisha?
 
mimi naona hapa watu wanashindwa kuelewa maana ya kila mtu yupo chini ya sheria, mbona watu tena Watanzania waliomba raisi mstaafu Mkapa aitwe na Takukuru kuhojiwa mbona hao Takukuru wameshindwa kama kweli kila mtu yupo chini ya sheria? halafu kwani sheria ipo Takukuru? mimi nijuavo sheria ipo mahakamani na bwana Mwakyembe ametoa option nzuri tu kuwa kama mnaona amekataa kuhojiwa basi nendeni ambapo sheria inapatikana----------MAHAKAMANI. Mnajua hakuna aliye kamili hapa duniani, na sisi tunaoongea na kuchangia ndani ya Hii forums tujiulize kama kwa namna moja au nyingine hatujawahi kushiriki kutoa au kupokea rushwa?

Mmoja anihabarishe kuhusu hilo
 
Ama kweli, the vicious cycle of corruption haitaisha!! Tunaendelea kula rushwa na kupokea malipo yasiyo halali obviously kwa sababu tunajua kila mtu anapokea, na hatuwezi kukemeana kwa sababu kila atakayekemea naye ni mchafu.

We are corrupt because we are corrupt, TUFUNGE MJADALA TULALE TUSUBIRI TAIFA KUVUNJIKA!
 
majibu:
jambo moja umesahau ni haki yako kukataa kuhojiwa na chombo ambacho huna Imani nacho, inawezekanaje TAKUKURU ambayo kamati ya Mwakyembe imewanyoshea kidole kuja kumuhoji na kumtendea haki Harrison Mwakyembe(mb),
alichofanya ni sahihi, na ndio maana amemwambia Hosea akiwa tayari wakakutane mahakamani.

kumbuka Mengi aliwahi kumgomea Waziri Masha kua hawezi kutoa maelezo yake polisi akiweza atangulie mahakamani, ni haki yako Mtanzania mwenzangu kukataa kuhojiwa na vyombo unavyohisi havitakutendea haki.
 


Nakuunga mkono hata mimi simwelewi.
 
Siasa za Bongo ni kichekesho kitupu. Hivi msafi ni nani? Yesu hakusema urongo kuwa "ukuhukumu utahukumiwa" "toa boriti kwenye jicho lako ndipo utoe kibanzi kwenye jicho la mwenzako".

Kwa taarifa hizi hata mimi napata mashaka na nia ya wapiganaji wa ufisadi kama ni kweli wanapiga kelele kwa kutupenda walala hoi na nchi yao ama kuna ajenda nyuma ya pazia.
 

wanalinda matumbo ndugu,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…