Dr. Mwakyembe Vs. TAKUKURU

wahenga walisema kuchamba kwingi mwishowe kuondoka na mavi
 
Tunashangazwa na mpambambanaji mkuu aliyejifanya kuwa kamwe hawezi kuhojiwa na PCCB kwa kuwa yeye anaelewa sheria na pia na Mwalimu wa sheria.yeye kwa akili yake alifikiria kuwa anamgomea EH kumbe anafunja sheria ya nchi.Sheria ni msemeno hajali kuwa aliyefunja sheria ni Dr. wa sheria kosa ni kosa tu.Huo ubabe wake alioutangazia Dunia uko wapi?Kama kweli tume yake imefanya haki katika kuchunguza RM kwa nini aogope kuundwa Tume Huru ya kuchunguza ukweli kuhusu sakata la RM? Anawataka wa TZ.tukubaliane na kila jambo analosema eti kwa sababu yeye Mwalimu wa sheria.Yeye achunguze, ahukumu na atoeasi adhabu.haki iko wapi?Watuhumiwa hawapewi nafasi ya kujitetea sijui ni sheria zipi anazositui Dr.Sheria.Wasi wasi mkubwa unadhihirika pale Dr. wa sheria anapopinga kwa nguvu zote kuundwa kwa tume huru ya kupitia upya mapendekezo hayo.Anaogopa nini kama kweli tume yake haikumwonea mtu.Rm ndio ulikuwa mtaji wake kwa hiyo aliogopa kuumbuliwa mbinu zake
 

Well said MTM, tuko pamoja katika hili, tusipoanzia huku hatuwezi kamwe kutibu haka kaugonjwa
 
Pamoja na kuwa Dr. Mwakyembe ni mwanasheria mzuri lakini hakufanya research ya kutosha kabla ya kukutana na waandishi wa habari kutoa tamko kuwa kamwe hawezi kuhojiwa na PCCB.
 


Mada yako ni ipi?
ilete hiyo mada niliyoinukuu kwa rangi tuijadili! usidandie treni kwa mbele!
 
Hatimaye mpiganaji ameamua kutii Sheria ya Nchi ambayo ameshiriki mwenyewe kuitunga? Halafu siku hizi haongei sana kwa kuwa kitu kilichompatia umaarufu, Richmond, kimewekwa kapuni, kwa hiyo mtaji wa kisiasa ume-expire?
U are such a HATER tu wewe sasa hapo unataka kusema nini, hivi ulitaka kitu hii ishu inyamaziwe tuu kama wewe si kibaraka mchakavu wa hao walarushwa????!@#$%^&
 
je wewe kama wewe ulitaribu uthubutu alo utenda japo punje ya ulezi? Sifia panapostahili .ok mungu atakutoa huko gizini ulipo akulete kwenye mwanga ili upambanue cheupe na cheusi.
Bosi wa walinzi wa walarushwa (TAKUKURU) akiwa mchafu ahina maana ofisi imekufa na kwamba ukatae kwenda kuhojiwa..ni jukumu letu kupiga kelele hivi hivi ili boss aondoke na ofc iwe safi na ifanye kazi kwa makusudio yaliowekwa period!
 
hilim lijamaa liwe la kwanza kupelekwa mahakamani kwa nguvu ya Mungu alie hai kwa kuwa hili nalo ni jizi kama majizi mengine yote.
 

Mzee Mwanakijiji,

PCCB walivyotaka kumhoji Dr. Mwakyembe mara ya kwanza hakukuwa na kikao cha bunge na in fact yeye Dr. alikuwa jimboni kwake.

Nafikiri kukataa kwake kulikuwa ni kwasababu tofauti na hiyo uliyoiandika hapo juu.
 
.

Lakini Mwakyembe alipoitwa mara ya kwanza na kukataa kuhojiwa,Hakukuwa na kikao chochote cha Bunge kilichokuwa kikiendelea..Kama alivyofafanua yeye mwenyewe kuwa alikahidi kutokanna na kwamba hakuona sababu yeyote ya kuhojiwa.
 
Samwel unashangaza JF yote, maana inaonekana wazi unachuki na hawa wabunge mahiri tena wa kwanza nchini kutoka chama cha mafisadi. Tulia kidogo ungoje watakayoyafanya na kufichua pale TAKUKURU watapomaliza kuwahoji au kuwatishia. Itaanza movement ya aina yake ambayo hizi posho zote zitabidi zianikwe ndipo na Ikulu itakapochafuliwa. Wabunge hapa wamejikuta wameingizwa mjini lazima wote wakubali. Maana walizidiwa ujanja pale walipopitisha mswada wa kuanzisha TAKUKURU lakini hawakujua kuwa wamemwongezea tena mkono mrefu Rasi, hawakuweza kuweka hata kipengele kuwa wao ndiyo wamchague kiongozi wa hiyo taasisi, sasa imewageuka mara ya pili. Ya kwanza ni pale walipojaribu kufukia ukweli wa mambo ya Richmond na sasa kuwahoji kwa nia ya kuwatisha. Wakisha hojiwa wakaja wamepoa wakaacha mapambano kitakuwa kimeeleweka. Na wasipolifanyia kazi swala zima la posho mbili mbili serikalini na nyingine za aina hiyo tutajua kuwa wameshapatiwa kile alichopata mbunge mtegemewa akaanza kutetea Richmond.
 
Punguzeni jazba jamani yeye aligoma bse kulikuwa na conflict of interest pale as it was time to discuss the richmond alafu uyo uyo mnaetaka kumtia adabu anataka kuwahoji.Huoni kuwa alikuwa anataka kushusha munkari wa kuidiscus richmond bungeni which to me naiita UNDUE INFLUENCE au greasing wabunge waache kukomaa na Hosea ktk sakata la richmonduli
 
Hatimaye mpiganaji ameamua kutii Sheria ya Nchi ambayo ameshiriki mwenyewe kuitunga? Halafu siku hizi haongei sana kwa kuwa kitu kilichompatia umaarufu, Richmond, kimewekwa kapuni, kwa hiyo mtaji wa kisiasa ume-expire?
Avatar yako na hiyo comment , they do not tally.
 

Double payment ya hela za umma siyo rushwa, hayo ni masuala ya fedha na mtu anayepokea fedha mara au fedha bila kufanyia kazi adhabu zake zinajulikana na zipo wazi. PPCB wanashindwa kutekeleza majukumu yao na wanavamia wapiganaji baada kamati ya Mwakeyembe kependekeza Hosea atimuliwe. Wakitaka rushwa zinaumiza wananchi waende halmashauri, hospitali za umma, mikataba ya madini, watu wanaopanga bei kama EWURA (mafuta), BOT(exchange rate), nauli za ndege za ndani etc.
 

Mtu yeyote anayechukua posho mara mbili kwa kazi ile ile anafanya makosa bila kujali ni rais wa nchi, waziri, mbunge au diwani wa kata.

Tusitetee mtu hapa na badala yake tutetee sheria. Kama kwa kupambana na mtu mmoja serikali imefungulia mkondo wa maji, hilo ni jambo jema kwa taifa maana ni nafasi ya kuwaumbua wote wanaofanya hivyo.

Nashangaa kuna watu wanakuja hapa na kusema kuchukua posho mbili sio kosa, inaonyesha jinsi Watanzania tunavyoshindwa kuelewa na kuheshimu sheria na maadili.

Hata kama PCCB ni wabovu mno lakini kweli utawalaumu pale wanapoamua kumhoji mtu ambaye amefanya kosa?

Tunajua polisi ni wala rushwa, kweli utawalaumu siku wakiamua kukukamata kwasababu umekula rushwa?

Ukitenda kosa usitafute mchawi na badala yake mchawi ni wewe mwenyewe. Mtu yeyote anayepigania jambo fulani lazima ajiangalia kwenye kioo na kuona yeye mwenyewe ni msafi, vinginevyo wabaya wake watammaliza na hilo ni kila sehemu hapa duniani.
 
Afadhali amekubali maana angeendelea kubisha yangemkuta yaliyomkuta Sendeka wangempa kesi ya kukataa amri halai ya kuitwa kuhojiwa.

Bravo Mwakyembe umekwepa mtego wa mafisadi
 
 
Ni aibu kufika hapa tulipo kama Taifa,tumeonyesha udhaifu mkubwa mno katika mfumo wetu mzima wa kutafuta viongozi.Nafikiri tuelekeze utaalamu wetu,nguvu zetu na akili zetu kujadili mabadiliko ya kimfumo yanayohitajika sasa badala ya kupoteza wakati kuwajadili watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…