Dr. Mwele Malecela: Asiyekuumba, kukuumbua hawezi

Dr. Mwele ungekaa kimya mama!, ukishambuliwa ukatulia mimi huwa naona inakuwa bora zaidi kuliko kujibu...anyway watu tunatofautiana malezi!

..Dr.Mwele Ntuli Malecela katupa kombora lingine.

..amemnukuu mwandishi George Orwell ktk maneno haya," ...the further the society drifts from the truth, the more it will hate those that speak it..."
 
Thesis ya PhD ya Dr Mwele Malecela ipo hata uki google tu unaipata London School of Hygiene and Tropical Diseases.
Hahahhh PHD ya nani haipo
Ya Mzee Meko sijaionaga
Chapa kazi Dr Mwele vijembe vizidi kukusukuma mbele
Yale ni maneno ya mkosaji au maneno ya vijiwenongwa
 
Anaanzisha mijadala mingi mno isiyokuwa na tija.Niliona jinsi alivyokuwa anafanya kampeni ya kuwataka wananchi wachaguwe viongozi wanaotokana na chama chake.Nao ni mjadala.Ni ziara ya kiserikali au ya kichama(chama chake).
 
Profesa Magufuli hakupaswa kuongea hayo hadharani.
 
Thesis ya PhD ya Dr Mwele Malecela ipo hata uki google tu unaipata London School of Hygiene and Tropical Diseases.
Ile ya MSELA wetu sasa k ukipata, asise hadi uombe toba..... Ukiikosea hiyo toba, unapotezwa kama Ben Saanane...
 
Thank you.
 
Jamaa ana wivu umejaaa

Au alitaka Dr Mwele akamuombe msamaha?
 
Shetani anahangaika kweli kuwaharibia watanzania maisha yao lakini Mungu yuko pamoja nao na atashindwa malipo ni hapahapa duniani.
 

Ikibidi na Mh. Raisi aandikiwe hotuba pia ili kupunguza ups and down za kuhama kutoka mada kuu
 
Matatizo ya kuwa na rais mshamba.

Anaropoka kila siku.

Na washamba wenzake wanamshangilia.
 
Kwa mtindo huu, je nitakuwa nakosea nikitabili kuwa siku moja huko mbele tutakuja kuambiwa Benno Ndullu nae alifukuzwa kazi kama gavana wa BOT kwa kufanya kazi kwa maelekezo ya mabeberu? Na sasa hao hao wamemtafutia kazi huko aliko!!!
 
Ikibidi na Mh. Raisi aandikiwe hotuba pia ili kupunguza ups and down za kuhama kutoka mada kuu
Magufuli ana ushamba wa kujiona anajua kila kitu, hotuba kaandikiwa sana lakini hataki kusoma alizoandikiwa, kashasema hataki kupangiwa.

Sasa unaweza kulaumu waandishi wa hotuba bure, wakati rais mwenyewe hataki kusoma.

Sasa hivi ukiangalia katika miezi sita iliyopita, hakuna mwezi ambao Tanzania haijatoa kituko katika habari za kimataifa duniani.

Na watu wengi hawaelewi jinsi hizi habari zinavyoiaribu taswira ya nchi kinataifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…