Uchaguzi ndio umemaliza kwa upande wa Tanganyika aka Tanzania Bara ,CCM nawapa hongera kama ni mechi ndio imekwisha ,mbinu walizotumia ndio ziliowapatia ushindi na sio wananchi kwa ujumla.
Kwa UKAWA wao nawapa pongezi za dhati kabisa kwani kama ni kipimo basi kimeonekana na kujikwaa si kuanguka pia naweza kusema ,demokrasia inaonyesha kushika kasi ,na UKAWA imekubalika kuliko CCM muhimu ni kujipanga ,miaka mitano sio mingi kabisa ,ni umri wa mtoto kuzaliwa na kuanza kuenda shule,itapita kama jana.
Muhimu ni kuzidi kushikana na kuzidisha mtandao na pia kuhakikisha majimbo na vitongoji mlivyoshinda mnajijenga kwa uimara zaidi na kuvidhibiti.
CCM tuseme magufuli amepewa ushindi ni katika uchaguzi bado ushindi katika aliyoyaahidi ambayo ni muhimu kwa kila Mtanzania ,isije kuwa ya maisha bora.
Hali kadhalika kuna hekaheka za bunge .UKAWA wameongeza idadi ya wabunge ni mtihani mwengine kwa CCM wanaoshangilia,tusubiri ndani ya miezi mitatu ,tutaanza kuona ukali ama utamu wa ahadi,
Nawapa hongera CCM tena ,nikiongezea kama Magufuli ameshinda kihalali basi neema tutaiona la kama ni kama ushindi wa waliopita kwa kweli kutakuwa hakuna jipya na zaidi ni kuongezeka kwa tunayotaka kuyakimbia.