George Smiley
JF-Expert Member
- Oct 24, 2011
- 471
- 266
Kuna habari zimeenea kwenye mitandao ya kijamii toka juzi kuwa Waziri wa Kazi na ajira Jenista Mhagama na Katibu Mkuu wa hiyo wizara Eric Shitindi wametoa agizo kwa shirika la NSSF wasimwalike aliyekuwa DG wa shirika hilo Dr Ramadhani Dau kwenye sherehe za ufunguzi wa Daraja hilo wiki Ijayo.
Ikumbukwe kuwa Dr Ramadhani Dau amepigania hili daraja lijengwe kwa miaka yote aliyokuwepo kwenye hilo shirika mpaka aliopoondolewa wiki chache zilizopita.Sitaki kuingilia ugomvi na vita vinavyoendelea kati ya akina Magori, Eunice Chieume, Jenista Mgahama na Eric Shitindi lakini kama ni kweli bas sidhani kama Dr Dau alistahili kudhalilishwa kiasi cha kupigwa marufuku kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa hili Daraja. Pia sidhani kama Mheshimiwa Rais Magufuli atafurahia uamuzi huu wa uongozi mpya wa NSSF na Wizara.
====================
====================
Update;
Habari hii si Kweli kwani Dr Ramadhani Dau amehudhuria. Soma=>Dr. Ramadhan Dau aunguruma darajani kwake