Tetesi: Dr. Ramadhani Dau apigwa marufuku uzinduzi wa Daraja la Kigamboni

Tetesi: Dr. Ramadhani Dau apigwa marufuku uzinduzi wa Daraja la Kigamboni

Status
Not open for further replies.
Liyumba ajenge BOT twin towers? Na gavana je?

By the way usichanganye vimiradi vidogovidogo kama kujenga magorofa na miradi mikubwa yenye kuinvolve state of art technologies kama daraja la kigamboni.
Daraja hili halipo east and central Africa
 
Naona mmeumbuka Dr Dau kaongea na Kasifiwa kwa kazi yake nzuri iliyo tukuka...!
 
Dau alikuepo kaongea, aka pga na quotes flan hvi, so ata haikawa hvo
 
Dr Dau si ameishaondoka hapo na nafasi yake kachukua mtu mwingine sasa aende kwenye uzinduzi kama nani? Ingawa kama atakuwa free siku hiyo anaweza kwenda kama raia wa kawaida au kwa nafasi aliyonayo sasa kama inahusiana na madaraja....

Ikumbukwe kuwa muda wote ambao Dr Dau alikuwa pale NSSF alikuwa analipwa mshahara na kila alichokifanya hakufanya kwa hisani bali kutimiza wajibu. Jina la Dr Dau litakumbukwa kwa mchango wake kufanikisha ujenzi wa daraja miaka mingi ijayo lakini sherehe za ufunguzi ni siku moja tu
Haya maneno ndio wanatakia akina Mohamed Said wawe wanafikiria kwanza kabla ya kuanza kuandika habari za kiswahiba,hawajui kwamba wanazidi kumpaka matope Dr Dau kwa kujifanya wao ndio watetezi wake wakati yeye kakaa kimya tu.Ni wangapi wameifanyia mema nchi hii na wapo wapo tuna hatusikia wapambe wakiandika unafiki humu,huyu Dau ana kipi zaidi?msituletee mambo ya Saigon hapa.
 
Wamuue, wamfunge, walibomoe Daraja bado historia yake Itabaki pale pale!
Wamuue kwa kitu gani?Muumba peke yake ndio mwenye uwezo wa kutoa roho,acheni upambe na hakuna atakaye mjadili humu jua mazidi kuwaudhi watu kwa kutaka kumfanya Dr Dau malaika,unaweza ukatenda mengi mazuri na lakini baya moja ndio likakuchafua zaidi ,uatake usitake jamaa yako ni mchafu.
 
Kuna chuki kali sana dhidi ya Dr Dau, hilo liko wazi.
Hata wasipomualika, ukizungumzia ujenzi wa daraja la Kigamboni, JK, JPM na Dr Dau majina yao yataandikwa kwenye kurasa za dhahabu
Mpambe /mnufaika utamjua tu
 
CgMY_7bXIAAh3vy.jpg

Kuna habari zimeenea kwenye mitandao ya kijamii toka juzi kuwa Waziri wa Kazi na ajira Jenista Mhagama na Katibu Mkuu wa hiyo wizara Eric Shitindi wametoa agizo kwa shirika la NSSF wasimwalike aliyekuwa DG wa shirika hilo Dr Ramadhani Dau kwenye sherehe za ufunguzi wa Daraja hilo wiki Ijayo.

Ikumbukwe kuwa Dr Ramadhani Dau amepigania hili daraja lijengwe kwa miaka yote aliyokuwepo kwenye hilo shirika mpaka aliopoondolewa wiki chache zilizopita.Sitaki kuingilia ugomvi na vita vinavyoendelea kati ya akina Magori, Eunice Chieume, Jenista Mgahama na Eric Shitindi lakini kama ni kweli bas sidhani kama Dr Dau alistahili kudhalilishwa kiasi cha kupigwa marufuku kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa hili Daraja. Pia sidhani kama Mheshimiwa Rais Magufuli atafurahia uamuzi huu wa uongozi mpya wa NSSF na Wizara.





KWA THREAD HII INADHIHIRISHA WAZI CHUKI NA WIVU WA WATU FLANI KUHUSU DAU NAIMANI HUKO ULIKO UNAJUTIA SANA MUNGU HAMFICHI MTU MBAYA.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom