Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanaweza kwenye miradi mbalimbali ili kupata faida ya kuwalipa wanachama wao
Yaani hata mimi naweza kujenga barabara yangu ya lami nikawatoza salio ili mpite hapo?Wanaweza kwenye miradi mbalimbali ili kupata faida ya kuwalipa wanachama wao
Una uhakika michango Yao ndio imetumika kujenga Daraja.Wanachama wa NSSF ambao michango yao ndio imejenga hilo daraja nao wamealikwa?
![]()
Kuna habari zimeenea kwenye mitandao ya kijamii toka juzi kuwa Waziri wa Kazi na ajira Jenista Mhagama na Katibu Mkuu wa hiyo wizara Eric Shitindi wametoa agizo kwa shirika la NSSF wasimwalike aliyekuwa DG wa shirika hilo Dr Ramadhani Dau kwenye sherehe za ufunguzi wa Daraja hilo wiki Ijayo.
Ikumbukwe kuwa Dr Ramadhani Dau amepigania hili daraja lijengwe kwa miaka yote aliyokuwepo kwenye hilo shirika mpaka aliopoondolewa wiki chache zilizopita.Sitaki kuingilia ugomvi na vita vinavyoendelea kati ya akina Magori, Eunice Chieume, Jenista Mgahama na Eric Shitindi lakini kama ni kweli bas sidhani kama Dr Dau alistahili kudhalilishwa kiasi cha kupigwa marufuku kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa hili Daraja. Pia sidhani kama Mheshimiwa Rais Magufuli atafurahia uamuzi huu wa uongozi mpya wa NSSF na Wizara.
100% nina uhakika. NSSF haijakopa pesa bank kwenye uwekezaji huu. Inawezekana hata hujui Parastal fund ni nini.Una uhakika michango Yao ndio imetumika kujenga Daraja.
NLiyumba ajenge BOT twin towers? Na gavana je?
By the way usichanganye vimiradi vidogovidogo kama kujenga magorofa na miradi mikubwa yenye kuinvolve state of art technologies kama daraja la kigamboni.
Daraja hili halipo east and central Africa
Kwa hiyo Dau katoa mfukoni kwake?Una uhakika michango Yao ndio imetumika kujenga Daraja.
Well saidDr Dau si ameishaondoka hapo na nafasi yake kachukua mtu mwingine sasa aende kwenye uzinduzi kama nani? Ingawa kama atakuwa free siku hiyo anaweza kwenda kama raia wa kawaida au kwa nafasi aliyonayo sasa kama inahusiana na madaraja....
Ikumbukwe kuwa muda wote ambao Dr Dau alikuwa pale NSSF alikuwa analipwa mshahara na kila alichokifanya hakufanya kwa hisani bali kutimiza wajibu. Jina la Dr Dau litakumbukwa kwa mchango wake kufanikisha ujenzi wa daraja miaka mingi ijayo lakini sherehe za ufunguzi ni siku moja tu
ooh,kumbe analipiziwa kisasi,asee..!!Mbona yeye Dr Dau hskumualika JPM wakati akiwa waziri wa Ujenzi siku ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja na Kigamboni???
Hivi kwanini huyu Dr Dau anatetewa kwa nguvu hivyo? Ni nini kimejificha nyuma ya utetezi huu?
Jamaa alishasema akichukua nchi MTALIMIA MENO mkafikiri eti anatania